Beki wa Taifa Stars Haji Mnoga Kubaki Salford City kwa Mwaka Mwingine

Beki wa Taifa Stars Haji Mnoga Kubaki Salford City kwa Mwaka Mwingine

Beki wa Taifa Stars Haji Mnoga Kubaki Salford City kwa Mwaka Mwingine

BEKI wa kulia wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Haji Mnoga, ameongeza mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Salford City inayoshiriki League Two nchini England. Uamuzi huu umethibitisha kuendelea kwa huduma yake muhimu katika kikosi hicho kwa msimu mwingine wa mashindano. Mnoga, ambaye awali alijiunga na Salford City kwa mkataba wa mwaka mmoja, alipaswa kuhitimisha muda wake wa awali mwishoni mwa msimu uliomalizika.

Hata hivyo, kutokana na mchango wake mkubwa na uaminifu alioonesha ndani ya uwanja, uongozi wa klabu haukusita kumpa mkataba mpya. Taarifa kutoka kwa mtu wa karibu na mchezaji huyo zimeeleza kuwa beki huyo alisaini rasmi mkataba huo mpya siku ya Jumatatu jioni baada ya kufikia makubaliano mazuri na uongozi wa timu.

Beki wa Taifa Stars Haji Mnoga Kubaki Salford City kwa Mwaka Mwingine

Katika msimu uliopita wa League Two, Haji Mnoga amecheza jumla ya mechi 39 kati ya 46, akicheza dakika 3,306, idadi inayoonesha nafasi yake ya kuaminika katika kikosi hicho. Akiwa beki wa pembeni wa kulia, ameendelea kuwa nguzo muhimu ya safu ya ulinzi ya Salford City, ambapo amewapiku wachezaji wenzake katika nafasi hiyo na kuwafanya baadhi yao kukaa benchi.

Mbali na majukumu yake ya ulinzi, Mnoga pia alichangia kwenye mashambulizi ya timu kwa kufunga bao moja na kutoa asisti nne, hali inayoonyesha uwezo wake wa kucheza kwa ufanisi pande zote mbili za uwanja.

Kabla ya kujiunga na Salford City, Mnoga alikuwa anakipiga katika klabu ya Aldershot, ambako alicheza kwa misimu miwili. Uhamisho wake kwenda Salford ulionekana kama hatua muhimu ya maendeleo ya taaluma yake, ambapo kwa msimu mmoja tu, amethibitisha kuwa miongoni mwa wachezaji wa kuaminiwa na kocha wa timu hiyo.

Salford City na Msimamo wa Mwisho wa Ligi

Katika msimu uliomalizika, Salford City—ambayo inamilikiwa na wachezaji wa zamani wa Manchester United kama David Beckham na Garry Neville—iliweza kumaliza ligi ikiwa nafasi ya nane kwa pointi 69, baada ya kushinda mechi 18, kutoka sare 15 na kupoteza 13 kati ya mechi 46 walizocheza.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Fountain Gate Njia Panda Baada ya Kichapo Dhidi ya JKT
  2. Timu Zilizoshuka Daraja Ligi Kuu ya NBC 2024/2025
  3. Matokeo ya Yanga Vs Namungo FC Leo 13/05/2025
  4. Kikosi cha Yanga Vs Namungo FC Leo 13/05/2025
  5. Dickson Ambundo Ajiweka Sokoni Huku Fountain Gate Ikipambana Kubaki Ligi Kuu
  6. Yanga Yaanza Kutega Mitego ya Kumnasa Marcel Koller, Aliyekuwa Kocha Ahly
  7. Simba Yaendelea Kugawa Dozi Kwa Kila Anayekutana Naye Ligi Kuu
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo