Viingilio Yanga VS Dodoma Jiji 22/06/2025

Viingilio Yanga VS Dodoma Jiji 22/06/2025

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, Yanga SC, kesho Jumapili ya tarehe 22 Juni 2025, watashuka dimbani kuivaa Dodoma Jiji FC katika mchezo muhimu utakaofanyika kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar kuanzia saa 10:00 jioni. Huu ni mchezo wa raundi ya 30 ya ligi, na una umuhimu mkubwa kwa Yanga SC katika kuhakikisha wanaendelea kujiweka karibu na ubingwa wa ligi hiyo, huku wakiwa na mechi moja tu iliyosalia – kiporo dhidi ya Simba SC Juni 25, 2025.

Yanga SC inaingia katika mchezo huu ikiwa na jumla ya pointi 76 baada ya michezo 28, ikiwa mbele kwa alama moja dhidi ya wapinzani wao wa karibu Simba SC wenye pointi 75. Mechi dhidi ya Dodoma Jiji ni ya lazima kushinda kwa Yanga, ili kujiweka katika nafasi ya juu kabla ya kumaliza msimu kwa pambano la kiporo dhidi ya Simba litakalochezwa wiki ijayo.

Kwa upande wa Dodoma Jiji, huu ni mchezo wa mwisho kwao msimu huu, lakini kwa Yanga SC, huu ndio daraja la kuelekea katika mchezo wa fainali isiyo rasmi ya ligi dhidi ya Simba SC.

Viingilio Yanga VS Dodoma Jiji 22/06/2025

Kwa mujibu wa tangazo rasmi, viingilio kwa ajili ya mchezo huu muhimu baina ya Yanga SC na Dodoma Jiji vimepangwa kama ifuatavyo:

  • SAA: Tsh 5,000
  • ORBIT: Tsh 5,000
  • URUSI: Tsh 10,000
  • WINGS: Tsh 15,000
  • VIP: Tsh 30,000

Viingilio Yanga VS Dodoma Jiji 22/06/2025

Mashabiki wanaohudhuria wanashauriwa kununua tiketi mapema ili kuepuka msongamano na kuhakikisha wanapata nafasi zao uwanjani. Uwanja wa Amaan unatarajiwa kujaa kutokana na umuhimu wa mchezo huu kwa mashabiki wa Yanga SC.

Hatima ya Ligi Yakaribia Kufungwa

Baada ya mechi ya kesho, mchezo wa mwisho wa msimu wa Yanga SC utakuwa dhidi ya Simba SC tarehe 25 Juni 2025, mechi ambayo itakuwa ya kuamua bingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2024/2025. Tayari Azam FC imeshajihakikishia nafasi ya tatu, huku Singida Black Stars wakimaliza katika nafasi ya nne.

Wakati timu nyingine kama Fountain Gate, Tanzania Prisons, na Namungo zikihangaika kuepuka kushuka daraja au mtoano, macho yote yataelekezwa Zanzibar kesho kwa mechi ya Yanga dhidi ya Dodoma Jiji kama hatua ya mwisho kuelekea kiporo cha kuamua bingwa.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Tetesi Za Usajili Simba Leo 2025/2026
  2. Tetesi Za Usajili Yanga Leo 2025/2026
  3. Kaizer Chiefs Wavamia Dili la Yanga SC Kunasa Saini ya Percy Tau
  4. Mashujaa FC Yaanza Harakati za Kumsajili Beki wa Simba SC
  5. Mamelodi Yaanza Kwa Ushindi wa 1-0 Dhidi ya Ulsan HD Kombe la Dunia
  6. Ratiba ya Ligi Kuu England 2025/2026 EPL
  7. Man United Kufungua Msimu Mpya wa EPL 2025/2026 Dhidi ya Arsenal
  8. Wydad Yaanza Kombe la Dunia Kwa Kipigo Mikononi mwa Manchester City
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo