Yanga vs Dodoma Jiji Leo 22/06/2025 Saa Ngapi?
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC, leo watakuwa na kibarua kizito kulitetea taji lao la msimu huu, huku wakikabiliana na Dodoma Jiji FC katika mchezo wa mwisho kabla ya kukutana na Simba SC Juni 25. Mchezo huu wa leo unatazamwa kuwa wa maamuzi kwa mustakabali wa ubingwa wa Yanga, ukizingatia ushindani uliopo katika nafasi za juu za msimamo wa ligi.
Mchuano huu umepangwa kuchezwa katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar, kuanzia majira ya saa 10:00 jioni tarehe 22 Juni 2025, ambapo mashabiki wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia pambano hilo muhimu linaloweza kubadili mwenendo wa mbio za ubingwa wa ligi kuu ya NBC Tanzania bara.
Mchezo huu dhidi ya Dodoma Jiji si wa kawaida. Ni fursa ya mwisho kwa Yanga kuhakikisha wanajihakikishia nafasi ya ubingwa au kujiweka katika mazingira bora kuelekea mchezo wa mwisho dhidi ya Simba. Kwa mantiki hiyo, kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuingia dimbani kikiwa na ari ya juu, kikitambua kuwa makosa yoyote yanaweza kugharimu taji.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Tanzania Yashinda Ubingwa wa CECAFA Wanawake 2025 Kupitia Twiga Stars
- KMKM Mabingwa wa FA Cup Zanzibar 2025 Baada ya Ushindi wa 4-2 Dhidi ya Chipukizi
- Timu Zilizofuzu Hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia la Vilabu 2025
- Klabu ya Liverpool Yamwaga Mamilioni Kumnasa Florian Wirtz
- Viingilio Simba SC vs Kagera Sugar 22/06/2025
- Viingilio Yanga VS Dodoma Jiji 22/06/2025
- Tetesi Za Usajili Simba Leo 2025/2026
- Tetesi Za Usajili Yanga Leo 2025/2026
Leave a Reply