Ratiba ya Fainali ya CRDB Federation Cup 2025
Timu ya Wananchi Yanga SC leo itashuka tena dimbani kulitetea taji la CRDB Federation Cup baada ya kumaliza rasmi kampeni ya kuutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu ya NBC kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Simba SC, Jumatano ya tarehe 25 Juni 2025.
Sasa, macho yote yanaelekezwa New Amaan Complex, Zanzibar, ambako fainali ya kombe hili maarufu inatarajiwa kufanyika kwa kishindo mnamo Juni 29, 2025, saa 2:15 usiku.
Mahali na Muda wa Mchezo
- Tarehe: Jumamosi, Juni 29, 2025
- Muda: Saa 2:15 Usiku
- Uwanja: New Amaan Complex, Zanzibar
Hii ni mara nyingine tena kwa Zanzibar kuwa mwenyeji wa mechi ya fainali ya CRDB Federation Cup, na maandalizi yote yapo tayari kuwapokea maelfu ya mashabiki kutoka kila kona ya Tanzania.
Viingilio na Maeneo ya Kukaa
Kwa mashabiki wanaotaka kushuhudia mchezo huu wa kihistoria mubashara, viingilio rasmi vimetangazwa kama ifuatavyo:
- VIP: TZS 20,000
- Urusi: TZS 10,000
- Orbit & Saa: TZS 5,000
Hii ni fursa ya kipekee kwa mashabiki wa soka kufurahia burudani ya hali ya juu kwa bei nafuu, huku wakishuhudia timu bora kabisa zikichuana katika hatua ya mwisho ya mashindano haya makubwa.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Chelsea Yajipanga Kuzima Moto wa Di Maria Katika Mechi ya Usiku Dhidi ya Benfica
- Simba Yavizia Saini ya Issa Fofana Nchini Ivory Coast Kama Mrithi wa Camara
- Ratiba ya CHAN 2024/2025 | CAF African Nations Championship
- Ratiba ya Kombe la Dunia la Vilabu 2025 Hatua ya 16 Bora
- Form Five Selection 2025: Majina Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026 Yatangazwa!
- Timu Zilizofuzu Hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia la Vilabu 2025
- Wydad Casablanca Yafungashiwa Virago Kombe la Dunia Bila Pointi
Leave a Reply