Makombe ya Yanga 2024/2025
Timu ya Wananchi, almaarufu kama Yanga SC, leo imefanya rasmi paredi ya kusherehekea makombe walioweza kukusanya msimu wa 2024/2025, ikionyesha mafanikio makubwa waliopata katika mashindano mbalimbali ya kitaifa.
Msafara huu wa kishujaa ulioandaliwa jijini Dar es Salaam, ulivuta maelfu ya mashabiki huku ukiambatana na shamrashamra zilizositisha shughuli mbalimbali za mji, hasa katika maeneo ya Msimbazi makao ya wapinzani wao wa jadi, Simba SC.
Wakati gari lililobeba wachezaji, viongozi na makombe ya Yanga likipita eneo la Msimbazi, shughuli zote za usafiri na biashara zilisimama kwa muda. Mtaa mzima wa Msimbazi uligubikwa na umati mkubwa wa mashabiki wa soka waliokuwa wakifuatilia msafara huo kwa furaha na hamasa. Jengo la Simba SC, ambalo limepangishwa kwa shughuli za kibiashara, liliwashuhudia mashabiki wa timu zote mbili wakijikusanya – wengine wakishangilia, huku baadhi wakitoa ishara za kejeli.
Magorofa yaliyopo kandokando ya barabara yalishuhudia mashabiki kupanda juu ili kuona vyema paredi, huku mchezaji Clatous Chama, ambaye aliwahi kuichezea Simba, akiibua hisia kali kwa kunyanyua moja ya makombe hadharani mbele ya jengo la Simba.
Ali Kamwe Aonyesha Makombe Kwa Mashabiki wa Simba
Wakati msafara huo uliposimama mbele ya jengo la Simba, Afisa Habari wa Yanga SC, Ali Kamwe, alichukua fursa hiyo kuonyesha moja baada ya jingine kati ya makombe matano ambayo Yanga imekusanya msimu huu. Hatua hiyo ilionekana kama ujumbe wa moja kwa moja kwa watani wao wa jadi – ishara ya ushindi na ukuu wa Yanga katika soka la Tanzania kwa msimu wa 2024/2025.
Makombe ya Yanga 2024/2025
Katika msimu huu wa kipekee, Yanga SC imeandika historia kwa kutwaa mataji matano makubwa, hatua inayodhihirisha ubora na uimara wa timu hiyo katika mashindano yote waliyoshiriki. Makombe hayo ni:
- NBC Premier League (Ligi Kuu Bara) ✅🏆
- CRDB Federation Cup (Kombe la Shirikisho la CRDB) ✅🏆
- Ngao ya Jamii ✅🏆
- Toyota Cup ✅🏆
- Muungano Cup ✅🏆
Ushindi huu wa mataji matano umetengeneza historia mpya kwa Yanga, ikiweka rekodi ambayo inatarajiwa kuwa ya kumbukumbu kwa muda mrefu katika soka la Tanzania.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Yanga SC Kusherehekea Vikombe 5 Leo Jijini Dar – Paredi Kubwa Yatarajiwa
- Messi Aondolewa Kombe la Dunia la Klabu Baada ya PSG Kuicharaza Inter Miami 4-0
- Yanga SC Yaibuka Bingwa wa Kombe la CRDB Baada ya Kuicharaza Singida BS 2-0
- Kikosi cha Yanga vs Singida Black Stars Leo 29/06/2025 Fainali ya CRDB
- Ratiba ya Fainali ya CRDB Federation Cup 2025
- Chelsea Yajipanga Kuzima Moto wa Di Maria Katika Mechi ya Usiku Dhidi ya Benfica
- Simba Yavizia Saini ya Issa Fofana Nchini Ivory Coast Kama Mrithi wa Camara
- Ratiba ya CHAN 2024/2025 | CAF African Nations Championship
Leave a Reply