Namungo Yampigia Hesabu Ally Salim Kama Mrithi wa Beno Kakolanya

Namungo Yampigia Hesabu Ally Salim Kama Mrithi wa Beno Kakolanya

Namungo Yampigia Hesabu Ally Salim Kama Mrithi wa Beno Kakolanya baada ya kumalizana na Beno Kakolanya aliyesajiliwa kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Singida Black Stars.

Taarifa za ndani kutoka klabu hiyo zinaeleza kuwa uongozi wa Namungo uko kwenye mazungumzo ya moja kwa moja na uongozi wa Simba SC kuhusu uwezekano wa kumsajili kipa huyo mwenye uzoefu mkubwa katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Namungo Yampigia Hesabu Ally Salim Kama Mrithi wa Beno Kakolanya

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika ndani ya Namungo, mazungumzo kati ya klabu hizo mbili yanaendelea kwa utulivu na matumaini makubwa. Ingawa Ally Salim bado ana mkataba unaoendelea hadi mwaka 2027 na klabu ya Simba, taarifa zinaeleza kuwa kipa huyo hayupo kwenye mipango ya kocha kwa msimu ujao, hali inayowapa Namungo nafasi ya kutimiza azma yao ya kumleta kwenye kikosi chao.

“Mkataba wa Salim na Simba utafikia tamati mwaka 2027, lakini mazungumzo yanaendelea vizuri kwa sababu hatarajiwi kuwa sehemu ya mipango ya timu hiyo msimu ujao,” alithibitisha mmoja wa viongozi wa Namungo, na kuongeza kuwa:

“Tunamuhitaji Salim kwa sababu tunaamini ana uwezo mkubwa wa kuimarisha safu yetu ya ulinzi. Japokuwa hakupata nafasi ya kucheza mara kwa mara Simba, uzoefu wake ni wa kiwango cha juu na tunaamini atakapopata nafasi atafanya makubwa.”

Kwa mujibu wa taarifa zaidi, Ally Salim ni miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kuachwa na Simba SC katika dirisha hili la usajili. Katika mabadiliko yanayotarajiwa ndani ya kikosi cha Simba kwa msimu ujao, jina la Salim limekuwa kati ya yale yanayozungumzwa, huku klabu hiyo pia ikihusishwa na mpango wa kuachana na kipa wao namba moja Moussa Camara baada ya mazungumzo ya mkataba wake mpya kusitishwa.

Aidha, taarifa zinaeleza kuwa kipa wa JKT Tanzania, Yakubu Suleiman, ametajwa kuwa mmoja wa makipa wanaoweza kuchukua nafasi ya Salim ndani ya kikosi cha Simba SC, jambo linalozidi kuashiria nafasi finyu kwa Ally Salim kubaki klabuni hapo.

Ally Salim alianza safari yake ndani ya Simba kupitia timu ya vijana kabla ya kupandishwa kikosi cha wakubwa mwaka 2018 akitokea Simba B. Tangu wakati huo, ameweza kuwa sehemu ya mafanikio ya klabu hiyo kwa kushinda mataji manne ya Ligi Kuu Bara kwa misimu ya 2017/18, 2018/19, 2019/20, na 2020/21. Uzoefu huu umeifanya Namungo kumuona kama chaguo bora na mrithi sahihi wa Beno Kakolanya.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Tetesi Za Usajili Simba Leo 2025/2026
  2. Wallace Karia Abaki Bila Mpinzani Baada ya Wagombea Watano Kuenguliwa
  3. Ibenge Atua Tanzania Kujiunga Rasmi na Azam FC kwa Msimu wa 2025/26
  4. Tetesi Za Usajili Yanga Leo 2025/2026
  5. Makombe ya Yanga 2024/2025
  6. Florent Ibenge Aaga Rasmi Al Hilal Sudan, Aelekea Kujiunga na Azam FC
  7. Lionel Messi anukia Ligi Kuu ya Uingereza EPL
  8. Miloud Hamdi Ajiunga na Ismaily ya Misri Baada ya Kuipa Yanga Mataji 3
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo