Kikosi cha Taifa Stars Kinaendelea Kujifua Nchini Misri kwa Ajili ya CHAN 2025
Kikosi cha Timu ya Soka ya Taifa ya Tanzania almaarufu kama Taifa Stars kinaendelea kujinoa vikali nchini Misri, ambako ndiko kambi rasmi ya maandalizi kuelekea michuano ya Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) 2025, zitakazoanza rasmi kuanzia Agosti 2 hadi 30 mwaka huu. Taifa Stars imeweka makazi yake ya maandalizi katika viwanja vya Mercure, Jijini Ismailia, tangu Julai 8, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika mashindano haya makubwa ya bara la Afrika.
Maandalizi Rasmi ya CHAN 2025 Yaanza kwa Kasi
Kikosi cha Taifa Stars kipo chini ya uongozi wa Kocha Mkuu Hemed Suleiman Ali ‘Morocco’, ambaye anasaidiwa na makocha wazawa Juma Ramadhani Mgunda ‘Pep Guardiola Mnene’ na Jamhuri Mussa Kihwelo ‘Julio’. Makocha hawa wamejizatiti kuandaa timu yenye ushindani mkubwa, hasa ikizingatiwa kuwa CHAN 2025 ni fursa muhimu kwa Tanzania kuonesha uwezo wake wa soka katika ngazi ya bara.
Kikosi cha Taifa Stars CHAN 2025: Wachezaji 27 Walioitwa
Katika maandalizi haya, jumla ya wachezaji 27 kutoka vilabu mbalimbali vya ndani wameitwa na kuungana kambini nchini Misri. Kikosi hicho kimeundwa kwa umakini ili kuhakikisha uwiano sahihi wa mabeki, viungo na washambuliaji wenye uwezo wa kupambana katika michuano ya kimataifa.
Walinda Mlango:
- Aishi Salum Manula ‘Air Manula’ – Simba SC
- Hussein Masalanga – Singida Black Stars
- Yakoub Suleiman Ali – JKT Tanzania
Mabeki:
- Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Abdurazak Mohamed – Simba SC
- Lusajo Mwaikenda, Pascal Msindo – Azam FC
- Dickson Job, Ibrahim Hamad ‘Bacca’ – Yanga SC
- Wilson Nangu – JKT Tanzania
- Vedastus Masinde – TMA Stars
- Lameck Lawi – Coastal Union
- Viungo wa Katikati:
Ahmed Pipino – KMC - Mudathir Yahya – Yanga SC
- Yusuph Kagoma – Simba SC
Viungo Washambuliaji:
- Feisal Salum, Nassor Saadun, Iddi Suleiman ‘Nado’, Abdul Suleiman ‘Sopu’ – Azam FC
- Kibu Dennis – Simba SC
- Jammy Simba – KMC
- Sabri Kondo – Coastal Union
- Shekhan Khamis – Yanga SC
- Washambuliaji:
Clement Mzize – Yanga SC - Mishamo Michael – Ken Gold
- Ibrahim Hamad Hilika – Tabora United
Kundi la Taifa Stars CHAN 2025
Katika droo ya upangaji wa makundi, Taifa Stars imepangwa Kundi B sambamba na mataifa ya Madagascar, Mauritania, Burkina Faso, na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR). Hili ni kundi lenye ushindani mkubwa, na maandalizi ya kina ni muhimu kwa Tanzania kuhakikisha wanapambana kwa mafanikio.
Makundi Mengine ya CHAN 2025:
- Kundi A: Kenya, Morocco, Angola, DR Congo, Zambia
- Kundi C: Uganda, Niger, Guinea, Algeria, Afrika Kusini
- Kundi D: Senegal, Kongo, Sudan, Nigeria
Mapendekezo ya Mhariri:
- Kibabage Akaribia Kujiunga Singida Bs Baada ya Kumaliza Mkataba Yanga
- Simba Yamalizana na Kiungo Balla Moussa Conte Kutokea CS Sfaxien
- Kocha Mpya wa Yanga 2025/2026: Siri Yafichuka Jangwani!
- Singida BS Yamnyatia Kipa wa Simba Hussein Abel Baada ya Kumaliza Mkataba
- Wachezaji 6 wa KMC Wasubiri Hatima Yao Kufuatia Mikataba Kumalizika
- Kennedy Musonda Atimkia Israel Baada ya Kumaliza Mkataba na Yanga
- Tetesi Za Usajili Yanga Leo 2025/2026
Leave a Reply