CV ya Moussa Balla Conte Mchezaji Mpya wa Yanga Sc 2025/2026
Klabu ya Yanga imekamilisha dili la kiungo wa ulinzi mwenye uwezo mkubwa, Moussa Balla Conte, ambaye anatokea CS Sfaxien ya Tunisia, kwa mkataba wa miaka miwili unaotarajiwa kudumu hadi Juni 30, 2028. Conte ni mchezaji wa kwanza kutambulishwa rasmi na Yanga SC katika dirisha la usajili la msimu wa 2025/2026, hatua inayodhihirisha dhamira ya klabu hiyo kuimarisha safu ya kiungo kufuatia kuondoka kwa Khalid Aucho.
Taarifa Binafsi za Moussa Balla Conte
- Jina kamili: Moussa Balla Conte
- Tarehe ya kuzaliwa: 15 Aprili, 2004
- Umri: Miaka 21 (2025)
- Uraia: Guinea
- Mji wa kuzaliwa: Kamsar, Guinea
- Urefu: Mita 1.86
- Mguu anaotumia zaidi: Kulia
- Nafasi: Kiungo wa Ulinzi (Defensive Midfield)
Safari ya Conte Kabla ya Kujiunga na Yanga
Conte alikuwa sehemu muhimu ya kikosi cha CS Sfaxien, klabu ya Tunisia ambayo ilishiriki Kombe la Shirikisho Afrika 2024/2025, ambako ilifika hatua ya makundi. Katika michuano hiyo, Conte alicheza dhidi ya Simba SC katika uwanja wa hapa nyumbani, mechi ambayo CS Sfaxien ilipoteza kwa mabao 2-1.
Katika msimu wa ligi kuu ya Tunisia 2024/2025, Moussa Balla Conte alicheza mechi 23, akipokea kadi saba za njano. Pia alishuka dimbani kwenye mechi sita za Kombe la Shirikisho Afrika, pamoja na mechi mbili kwenye Kombe la Klabu Bingwa kwa Nchi za Kiarabu.
Licha ya kuwa bado kijana, Conte alijidhihirisha kama mmoja wa wachezaji wa kuaminiwa katika kikosi cha CS Sfaxien. Uwepo wake ulihisiwa hasa katika safu ya kiungo wa ulinzi, akiwa chaguo la kwanza kwa kocha wa timu hiyo.
Mbio za Kumwania Conte: Vita Kati ya Yanga na Simba
Awali, Simba SC ndiyo ilikuwa klabu ya kwanza kuonesha nia ya dhati ya kumsajili Conte. Hata hivyo, Yanga waliingia kwa kasi kwenye mazungumzo, na hatimaye wakamshinda hasimu wao huyo wa jadi. Taarifa zinaeleza kuwa dau la usajili halikuwekwa wazi, lakini Yanga walimalizana na CS Sfaxien kwa makubaliano rasmi kabla ya kupata kibali cha kumalizana na mchezaji huyo binafsi.
Conte aliwasili nchini juzi usiku kabla ya utambulisho rasmi kupitia kurasa za mitandao ya kijamii za klabu hiyo. Picha zilimuonesha akiwa na rais wa klabu ya Yanga, Hersi Said, jambo lililothibitisha kuwa kiungo huyo sasa ni sehemu ya familia ya Wananchi.
Nafasi ya Conte Katika Kikosi cha Yanga 2025/2026
Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani ya klabu, Moussa Balla Conte amesajiliwa maalum kuziba pengo lililoachwa na kiungo wa zamani, Khalid Aucho. Aidha, Conte anatajwa kuwa ni miongoni mwa viungo wa kisasa wenye uwezo wa kuhimili mikikimikiki ya ligi ya Tanzania Bara na mashindano ya kimataifa. Kwa mujibu wa taarifa, kocha mpya wa Yanga SC, ambaye anatarajiwa kutangazwa hivi karibuni, ndiye aliyependekeza Conte kupewa kipaumbele katika usajili wa dirisha hili.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Tetesi za Usajili Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara 2025/2026
- Tetesi Za Usajili Yanga Leo 2025/2026
- Tetesi Za Usajili Simba Leo 2025/2026
- Rasmi: Namungo FC Yathibitisha Kuachana na Mshambuliaji Meddie Kagere
- Kikosi cha Taifa Stars Kinaendelea Kujifua Nchini Misri kwa Ajili ya CHAN 2025
- Kocha wa Yanga Miloud Hamdi Ashinda Tuzo ya Kocha Bora wa NBC June 2024
- Simba Yathibitisha Kumtoa Omary Omary kwa Mkopo kwenda Mashujaa FC
Leave a Reply