Picha za Wachezaji Wapya wa Simba 2025/2026
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wamefungua ukurasa mpya kuelekea msimu wa mashindano wa 2025/2026 kwa kutangaza rasmi wachezaji wapya watakaojiunga na kikosi hicho maarufu. Huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kuona mabadiliko ndani ya kikosi cha “Mnyama”, klabu hiyo yenye historia kubwa ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano ya kimataifa imeanza kutoa orodha ya nyota wapya waliotia saini kuwatumikia. Hapa habariforum.com tumekuandalia picha za wachezaji wapya wa Simba 2025/2026 pamoja na wasifu mfupi wa kila mchezaji waliotangazwa hadi sasa. Pia tutakuwa tukisasisha orodha hii kila mara Simba itakapowatangaza rasmi nyota wapya.
1. Hussein Daudi Semfuko – Kiungo Mkabaji (Tanzania)
📍 Kutoka: Coastal Union
📅 Tarehe ya kuzaliwa: Mei 17, 2004
🧍♂️ Umri: Miaka 21
📝 Mkataba: Miaka 3 (Mpaka Juni 2028)
Klabu ya Simba SC imethibitisha kumsajili Hussein Daudi Semfuko, kiungo mkabaji chipukizi mwenye uraia wa Tanzania. Akitokea Coastal Union ya Tanga, Hussein amejiunga rasmi na Simba kwa mkataba wa miaka mitatu hadi mwaka 2028.
Ni mchezaji anayesifika kwa uwezo wa kuzuia mashambulizi na kuunganisha mipira kati ya safu ya ulinzi na ushambuliaji. Ujio wake unatazamiwa kuimarisha kiungo wa ulinzi wa Simba kuelekea msimu mpya.
2. Morice Michael Abraham – Kiungo Mshambuliaji (Tanzania)
📍 Kutoka: Serbia (Akiwa huru)
📅 Tarehe ya kuzaliwa: Agosti 13, 2003
🧍♂️ Umri: Miaka 21
🦶 Mguu anayotumia: Kushoto
📏 Urefu: 1.70m
Morice Abraham ni kiungo mshambuliaji mwenye historia ndefu na sifa ya kuwa mchezaji mwenye nidhamu ya hali ya juu. Alikulia katika kituo cha Alliance Academy jijini Mwanza na aliwahi kuwa nahodha wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, iliyoshiriki michuano ya AFCON 2019. Baada ya kurejea kutoka Serbia, Morice alifanya mazoezi na Simba ambapo aliridhisha benchi la ufundi chini ya Kocha Fadlu na kusajiliwa rasmi. Kwa sasa anasubiri kukamilishiwa vibali vya usafiri ili kujiunga na kambi ya timu iliyopo nchini Misri.
3. Alassane Maodo Kanté – Kiungo wa Kati (Senegal)
📍 Klabu ya awali: Huru (Amesajiliwa Julai 23, 2025)
📅 Tarehe ya kuzaliwa: Desemba 20, 2000
🧍♂️ Umri: Miaka 24
📏 Urefu: 1.85m
🦶 Mguu anayotumia: Kulia
🗺️ Mahali alikozaliwa: Ziguinchor, Senegal
Alassane Kante ni kiungo wa kati mwenye uwezo mkubwa wa kutuliza mchezo, kusambaza mipira na kuunganisha safu ya kati. Amejiunga na Simba SC akiwa mchezaji huru, akitarajiwa kuongeza uthabiti na uzoefu katika eneo la kati. Urefu wake na mbinu zake za kiufundi ni faida kubwa kwa mfumo wa Simba.
4. Rushine De Reuck – Beki wa Kati (Afrika Kusini)
📍 Klabu ya awali: Huru (Amesajiliwa Julai 30, 2025)
📅 Tarehe ya kuzaliwa: Februari 9, 1996
🧍♂️ Umri: Miaka 29
📏 Urefu: 1.83m
🦶 Mguu anayotumia: Kulia
🗺️ Mahali alikozaliwa: Cape Town, Afrika Kusini
Rushine De Reuck ni beki kisiki mwenye uzoefu mkubwa wa kucheza soka la ushindani. Akiwa na umri wa miaka 29, ujuzi wake wa kusoma mchezo, kuongoza safu ya ulinzi, na uwezo wa angani vinampa nafasi kubwa kuwa chaguo la kwanza kwenye beki ya kati ya Simba. Usajili wake ni sehemu ya mkakati wa Simba kujenga safu madhubuti ya ulinzi inayoweza kuhimili mashindano ya ndani na nje ya nchi.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Ratiba ya Mtihani wa Darasa la Nne 2025
- Tarehe Ya Kuripoti Shuleni Kidato cha Tano 2025
- Matokeo ya Kidato cha Sita 2025 Yametangazwa Rasmi na NECTA: Ufaulu Waendelea Kupanda!
- Sheria Za Shule Za Sekondari Tanzania
- Jinsi Ya Kuangalia Matokeo Ya Kidato Cha Sita 2025
- Kozi za Diploma Zenye Mkopo 2025/2026
Leave a Reply