Ratiba 16 Bora Ndondo Cup 2025
Mashindano ya Ndondo Cup 2025 yamefikia hatua ya 16 Bora, hatua ambayo inatarajiwa kua yenye ushindani mkali na burudani ya aina yake kwa mashabiki wa soka la mitaani. Hii ndiyo hatua inayoleta pamoja vilabu vyenye historia ndefu katika michuano hii na timu changa zenye kiu ya kuandika historia. Ratiba rasmi imetangazwa, ambapo mechi zitaanza 14 Septemba 2025 na kumalizika 19 Septemba 2025.
Kwa mujibu wa Ratiba 16 Bora Ndondo Cup 2025, michezo yote itachezwa katika viwanja viwili maarufu jijini Dar es Salaam ambavyo ni Uwanja wa Kinesi na Uwanja wa Bandari, huku mashabiki wakitarajiwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia vipaji vya vijana wakipambana kwa nafasi ya kuingia robo fainali.
Tarehe | Timu Zinazokutana | Uwanja | Saa |
---|---|---|---|
14.09.2025 | Azimio FC vs Weekend Team | Kinesi | 10:00 Alasiri |
14.09.2025 | Mshikamano Talent vs Bahari FC | Bandari | 10:00 Alasiri |
15.09.2025 | Buza Mabegani vs Mask FC | Bandari | 10:00 Alasiri |
15.09.2025 | Friends Rangers vs Tandika City | Kinesi | 10:00 Alasiri |
18.09.2025 | Gomz United vs Haipotei Jogging | Bandari | 10:00 Alasiri |
18.09.2025 | Madenge FC vs Keko Furniture | Kinesi | 10:00 Alasiri |
19.09.2025 | Mabibo Market vs Kagera Boys | Kinesi | 10:00 Alasiri |
19.09.2025 | Soccer City vs Makuburi FC | Bandari | 10:00 Alasiri |
Mapendekezo ya Mhariri:
- Mashabiki Wa Soka Wakimbizana na Tiketi za Kombe la Dunia 2026
- Vituo vya Kununua Tiketi za Siku ya Yanga DAY 2025
- Yanga VS Bandari 12/09/2025 Saa Ngapi?
- Romain Folz Aitaja Simba Katika Maandalizi ya Mechi ya Yanga na Bandari
- Kocha Ken Odhiambo Asema Bandari Imejipanga Kumkabili Bingwa Yanga
- Bakari Mwamnyeto Atoa Wito Kwa Mashabiki Kujitokeza Kwa Mkapa
- Mbosso Avunja Rekodi za Burudani Simba Day Kwa Performance Bora Zaidi
Leave a Reply