Kocha Folz Aahidi Ushindi Mkubwa Mechi ya Marudiano Dhidi ya Wiliete
Kuelekea mchezo wa kesho wa Klabu Bingwa Afrika, Kocha wa Yanga SC, Romain Folz, amesema kikosi chake kipo tayari kikamilifu kwa mtihani wa marudiano dhidi ya Wiliete kutoka Angola. Mchezo huo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika unatarajiwa kupigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Folz alisisitiza kuwa hana presha yoyote kuhusiana na mchezo huo kwa kuwa kikosi chake kipo kwenye mwenendo bora na kimekuwa kikishinda mechi zote za awali. Hata hivyo, amewaonya wachezaji wake kutobweteka kwa ushindi wa awali walioupata dhidi ya Waangola hao.
“Matokeo ya mchezo wa kwanza tumeshayaweka kando. Nimewaambia wachezaji hii ni mechi tofauti na mpya, tunatakiwa kutafuta ushindi mwingine ili tufuzu,” alisema Folz.
Mabadiliko Yanaendelea kwa Ratiba Ngumu
Kwa mujibu wa Folz, ratiba ngumu ya michezo ya Yanga SC imekuwa ikihitaji mabadiliko ya kikosi ili kuwapa nafasi wachezaji wote na kuhakikisha wanabaki katika hali nzuri ya ushindani. Kocha huyo alibainisha kuwa kila mchezaji ndani ya kikosi ana uwezo mkubwa wa kupambania timu.
“Kuhusu mabadiliko ya kikosi, yataendelea. Kwa hizi mechi zilizo karibu njia salama ni kuwapa nafasi wachezaji na kuwapumzisha wengine. Kila mchezaji aliye hapa ana kipaji kikubwa,” aliongeza.
Kikosi Kamili Kesho Mkapa
Kocha huyo alisisitiza kuwa katika mchezo wa kesho, mashabiki wa Yanga watashuhudia kikosi kamili kitakachoingia dimbani kwa lengo la kuhakikisha ushindi unapatikana. Alibainisha kuwa mabadiliko madogo yatafanyika lakini msimamo wake ni wazi – Yanga itashuka uwanjani kwa dhamira ya kuendeleza kasi ya ushindi.
“Kesho tutakuwa na timu kamili. Tutakuwa na mabadiliko lakini tutakuwa na kikosi kitakachoendeleza kasi yetu ya ushindi,” alisisitiza Folz.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2025/2026
- Wafungaji Bora Ligi Kuu ya NBC Tanzania 2025/2026
- Uwanja wa Jamhuri Dodoma Kuwa Makazi Mapya ya Mtibwa Sugar
- Simba Yaanza Ligi Kuu 2025/26 Kwa Ushindi wa 3-0 Dhidi ya Fountain Gate
- Matokeo ya Simba vs Fountain Gate Leo 25/09/2025
- Ibenge Afungua Kampeni za Ligi Kuu kwa Ushindi wa 2-0 Dhidi ya Mbeya City
- Simba vs Fountain Gate Leo 25/09/2025 Saa Ngapi?
- Vilabu Bora Afrika 2025 (CAF Club Ranking 2025)
Leave a Reply