Kikosi cha Yanga vs Wiliete SC Leo 27/09/2025

Kikosi cha Yanga vs Wiliete SC Leo 27/09/2025

Timu ya Wananchi Yanga SC leo 27/09/2025 inashuka dimbani kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kuwakaribisha Wiliete SC ya Angola katika mchezo wa marudiano wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League).

Mchezo huu ni wa kihistoria kwa Wananchi, ambapo mashabiki wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi kuisapoti klabu yao pendwa, huku swali kubwa likiwa ni “Yanga vs Wiliete SC Leo 27/09/2025 Saa Ngapi?” Huu ni mchezo wa marudiano baada ya Yanga SC kupata ushindi wa mabao 3-0 jijini Luanda, Angola, wiki iliyopita. Licha ya kuwa na faida ya ushindi mkubwa, kikosi cha Yanga kimeweka wazi kwamba hakitachukulia mchezo huu kirahisi, bali kitashuka dimbani kuhakikisha kinalinda heshima yake mbele ya mashabiki.

Kikosi cha Yanga vs Wiliete SC Leo 27/09/2025

Kauli ya Kocha Romain Folz kuelekea Mchezo

Kocha wa Yanga SC, Romain Folz, amesisitiza kwamba wachezaji wake wako tayari kwa changamoto ya leo na wamejipanga kushusha burudani safi kwa mashabiki wa nyumbani.

Folz amesema hana presha kubwa kwa sababu kikosi chake kipo katika mwenendo mzuri wa ushindi, lakini ameweka msisitizo kuwa mchezo wa kwanza umeshapitwa na wakati na sasa lengo kuu ni kushinda tena ili kufanikisha safari ya kufuzu hatua inayofuata ya mashindano.

Amesema pia kutokana na ratiba ngumu ya mashindano, ataendelea kufanya mabadiliko ndani ya kikosi ili kuwapa nafasi wachezaji wote kuonyesha uwezo wao, huku akiwahakikishia mashabiki kwamba Yanga itashuka na kikosi kamili kitakachopambana kuhakikisha matokeo mazuri.

“Kesho (leo) tutakuwa na timu kamili. Tutakuwa na kikosi ambacho kitaendeleza kasi yetu ya ushindi. Matokeo ya kwanza tumeyaweka kando, hii ni mechi mpya na lengo ni kushinda tena,” alisema Folz.

Kikosi cha Yanga vs Wiliete SC Leo 27/09/2025

Mashabiki wengi wanatazamia kwa hamu orodha ya wachezaji ambao Kocha Folz atawapanga leo. Kwa kawaida, katika michezo ya kimataifa ya CAF, kikosi cha kwanza hutangazwa rasmi saa moja kabla ya mchezo kuanza.

Hivyo basi, kikosi rasmi cha Yanga SC dhidi ya Wiliete SC Leo 27/09/2025 kitapangwa na kuthibitishwa na benchi la ufundi kabla ya kipenga cha kwanza. Habariforum itakuletea mara moja kikosi kamili cha Yanga pindi kitakapotangazwa rasmi.

Kikosi cha Yanga vs Wiliete SC Leo 27/09/2025

Kauli ya Kocha wa Wiliete SC, Bruno Ferry

Kwa upande mwingine, kocha wa Wiliete SC ya Angola, Bruno Ferry, amekiri kwamba timu yake haina cha kupoteza. Amedai wanatambua udhaifu uliojitokeza kwenye mchezo wa kwanza walipokubali kipigo cha 3-0 nyumbani, lakini wamejipanga kurekebisha makosa yao.

Ferry alisema moja ya changamoto kubwa kwa kikosi chake ni ukosefu wa uzoefu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini ameahidi wachezaji wake wataingia dimbani wakiwa na morali ya kuonyesha kitu kipya na kupambana hadi mwisho.

“Tunakwenda kukutana na wapinzani wenye uzoefu mkubwa. Yanga ikicheza nyumbani sio rahisi kupoteza, lakini tumejipanga kuonyesha utofauti,” alisema Ferry, ambaye aliwahi kufundisha Azam FC hapa Tanzania.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Viingilio Mechi ya Yanga vs Wiliete SC 27/09/2025
  2. Sergio Busquets Atangaza Kustaafu Soka Mwishoni Mwa Msimu Huu
  3. Kocha Folz Aahidi Ushindi Mkubwa Mechi ya Marudiano Dhidi ya Wiliete
  4. Yanga SC Yazindua Jezi Mpya Ili Kulinda Mapato Dhidi ya Jezi Feki
  5. Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2025/2026
  6. Wafungaji Bora Ligi Kuu ya NBC Tanzania 2025/2026
  7. Uwanja wa Jamhuri Dodoma Kuwa Makazi Mapya ya Mtibwa Sugar
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo