Matokeo ya Yanga vs Mbeya City Leo 30/09/2025
Mashabiki wa soka nchini wanatarajia burudani ya kipekee leo Jumanne, Septemba 30, 2025, pale Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, ambapo wenyeji Mbeya City watawakaribisha mabingwa watetezi Young Africans SC (Yanga) katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League). Mchezo huu unatarajiwa kuanza majira ya saa 10:15 jioni, ukiwa kivutio kikuu cha wiki na kuibua msisimko mkubwa kwa mashabiki kutokana na historia ya timu hizi mbili.
Kwa mujibu wa tangazo la viingilio, mashabiki wataingia kwa gharama zifuatazo:
- VIP A: Tsh 30,000/=
- VIP B, C na Mzunguko: Tsh 10,000/=
Yanga wakiwa mabingwa watetezi, wanaingia kwenye mtanange huu wakiwa na morali ya juu baada ya kuanza msimu kwa kishindo. Katika mchezo wao wa kwanza wa ligi, waliifumua Pamba Jiji FC kwa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Matokeo hayo yaliashiria wazi kuwa wapo tayari kuendeleza utawala wao ndani ya soka la Tanzania.
Ushindi leo dhidi ya Mbeya City unaweza kuwapandisha kileleni mwa msimamo, kwani wapinzani wao wakubwa kama Dodoma Jiji, JKT Tanzania, Namungo na Mashujaa FC wote wakiwa na pointi nne baada ya michezo miwili au mitatu.
Kwa upande wa Mbeya City, mchezo huu ni nafasi ya kurekebisha mwanzo wao wa msimu. Baada ya kukusanya pointi tatu katika michezo miwili ya awali, kikosi hicho kimeonyesha mchanganyiko wa matokeo.
Hata hivyo, ushindi wao wa kuvutia wa 3-1 katika mechi ya mwisho unaonesha kuwa wana uwezo wa kuwasumbua hata vigogo wakipewa nafasi. Leo wakiwa nyumbani mbele ya mashabiki wao, Mbeya City watalenga kusababisha pigo na kukomesha kasi ya mabingwa watetezi.
Fuatilia Hapa Matokeo ya Yanga vs Mbeya City Leo 30/09/2025
Yanaga Sc | VS | Mbeya City |
- 🏆 #nbcpremierleague
- Mbeya City 🆚 Yanga Sc
- 🗓️ 30 Sept 2025
- 🏟️ Sokoine
- ⏱️ Saa 10:15 Jioni
Historia ya Michezo ya Yanga vs Mbeya City
Historia inaonesha kuwa mara nyingi Yanga hutawala wanapokutana na Mbeya City. Katika mechi zao 20 zilizopita, Yanga imekuwa ikipata ushindi mara nyingi zaidi, japo mara nyingi kwa tofauti ndogo ya mabao. Hata hivyo, kumbukumbu ya Desemba 2022 bado ipo akilini mwa mashabiki, pale Mbeya City walipoishangaza Yanga kwa ushindi wa 3-2, moja ya mechi kali zaidi katika misimu ya hivi karibuni.
Aidha, kwenye msimu wa 2022/23, Yanga walifanikiwa kushinda mchezo mmoja na kutoka sare katika mwingine dhidi ya Mbeya City, jambo linaloonyesha uimara wao lakini pia mapungufu ya mara kwa mara kwenye safu ya ulinzi.
Mbeya City, maarufu kwa mfumo wao wa kushambulia kwa kushitukiza (counter-attack) hasa nyumbani, wamekuwa mwiba kwa Yanga mara kadhaa. Mashabiki bado wanakumbuka sare tasa ya Mei 2022, ambapo mabingwa walishindwa kabisa kuvunja ukuta wa Mbeya City.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Kikosi cha Yanga vs Mbeya City Leo 30/09/2025
- Ratiba ya Mechi za Leo 30/09/2025 Ligi Kuu ya NBC
- Ratiba ya Kombe la Shirikisho Afrika CAF 2025/2026
- Mbeya City vs Yanga sc Leo 30/09/2025 Saa Ngapi?
- Arsenal yapata ushindi wa dakika za mwisho dhidi ya Newcastle United
- Wapinzani wa Simba Raundi ya Pili Ligi ya Mabingwa Afrika CAF
- Azam FC Yafuzu Raundi ya Pili CAFCC Baada ya Ushindi wa 4-0 Dhidi ya El Merriekh
- Singida Black Stars Yatinga Raundi Ya Pili Kombe la Shirikisho Afrika
- Real Madrid Yapoteza 2-5 Dhidi ya Atletico Madrid, Kichapo cha Kwanza kwa Xabi Alonso LaLiga
Leave a Reply