FIFA Yamteua Eng. Hersi Said Kuwa Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Vilabu ya Wanaume Duniani

FIFA Yamteua Eng. Hersi Said Kuwa Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Vilabu ya Wanaume Duniani

Rais wa Klabu ya Yanga SC na Mwenyekiti wa Chama cha Vilabu vya Afrika (African Club Association – ACA), Eng. Hersi Said, ameteuliwa rasmi na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kuwa Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Vilabu ya Wanaume Duniani kwa kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka 2025 hadi 2029.

Taarifa hiyo imethibitishwa na Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ali Kamwe, ambaye alieleza kuwa uteuzi huo ni hatua kubwa katika historia ya soka la Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Kwa mujibu wa Kamwe, Eng. Hersi anakuwa mtu wa kwanza kutoka Afrika Mashariki na Kati kuteuliwa kushiriki katika kamati kubwa ya mashindano ya vilabu ya wanaume chini ya FIFA — hatua inayoonesha namna jina lake linavyozidi kung’ara katika ngazi za juu za uongozi wa mpira wa miguu duniani.

FIFA Yamteua Eng. Hersi Said Kuwa Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Vilabu ya Wanaume Duniani

Uteuzi huu wa Eng. Hersi Said ni heshima ya kipekee kwa Tanzania na bara la Afrika kwa ujumla. Kama kiongozi anayeheshimika barani, Eng. Hersi amekuwa mstari wa mbele katika kuendeleza na kuboresha mfumo wa usimamizi wa vilabu kupitia nafasi yake kama Mwenyekiti wa ACA, taasisi inayoratibu shughuli na maslahi ya vilabu barani Afrika.

Kupitia nafasi hiyo, amekuwa akichangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza uwakilishi wa Afrika kwenye mashindano ya kimataifa na katika kuimarisha uhusiano wa vilabu vya Afrika na taasisi za juu za soka kama CAF na FIFA.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Djigui Diarra Ashinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Septemba 2025/2026
  2. Ahmad Ali Ashinda Tuzo ya Kocha Bora Mwezi Septemba 2025/2026
  3. Msimamo wa Ligi Kuu Zanzibar PBZ 2025/2026
  4. Cv ya Dimitar Pantev Kocha Mpya wa Simba Sc 2025
  5. Singida BS Yaendeleza Ubabe Mbele ya Mashujaa na Kubaki Kinara wa Ligi Kuu Bara
  6. Ratiba ya Ligi Kuu Zanzibar PBZ 2025/2026
  7. Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2025/2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo