Zimbabwe Yainyima Nafasi Afrika Kusini Kufuzu Kombe la Dunia

Zimbabwe Yainyima Nafasi Afrika Kusini Kufuzu Kombe la Dunia

Mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia 2026 kati ya Zimbabwe na Afrika Kusini umemalizika kwa suluhu ya bila kufungana, matokeo yaliyokuwa pigo kubwa kwa matumaini ya Bafana Bafana kufuzu moja kwa moja michuano hiyo mikubwa ya dunia.

Ushindi katika mchezo huu ungeiweka Afrika Kusini kileleni mwa Kundi C kwa pointi 17, ikiizidi Benin kwa tofauti ya magoli, lakini suluhu hiyo imewaacha wakitegemea matokeo ya timu nyingine.

Zimbabwe Yainyima Nafasi Afrika Kusini Kufuzu Kombe la Dunia

Katika michezo mingine ya kundi hilo, Benin ilijipatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Rwanda na kufikisha pointi 17, ikienda kileleni, huku Nigeria ikiibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Lesotho, na kufufua matumaini yao ya kutinga fainali. Hali hiyo sasa inailazimisha Afrika Kusini kutegemea matokeo ya mchezo kati ya Nigeria na Benin utakaochezwa Jumanne, ili kuamua hatma yao ya kufuzu.

Licha ya kutawala mchezo kwa kipindi kirefu, Bafana Bafana walishindwa kutumia nafasi walizopata, wakipiga mwamba mara mbili na kuona jitihada zao zikizimwa na uhodari wa kipa wa Zimbabwe, Washington Arubi. Lyle Foster na Mohau Nkota walikaribia kufunga, huku jitihada za Oswin Appollis na Sipho Mbule zikikosa matokeo chanya.

Kocha Hugo Broos, ambaye amekuwa akitazamwa kwa makini baada ya timu hiyo kupokwa pointi tatu na FIFA mwezi uliopita kutokana na kosa la kumchezesha mchezaji aliyefungiwa, sasa anakabiliwa na shinikizo jipya. Uamuzi wake wa kumtoa Nkota kipindi cha pili na kushindwa kuongeza mshambuliaji baada ya Zimbabwe kubaki na wachezaji 10, umeibua maswali kutoka kwa wachambuzi.

Zimbabwe, licha ya kuwa nyuma kiuchezaji, walionesha nidhamu kubwa ya kiulinzi na kusimama imara hadi dakika ya mwisho, wakishangilia kwa nguvu baada ya kusikika kwa filimbi ya mwisho matokeo yaliyowanyima majirani zao nafasi ya mapema ya kufuzu.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Matokeo Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars vs Zambia Leo Oktoba 8 2025
  2. Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2025/2026
  3. Msimamo wa Ligi Kuu Zanzibar PBZ 2025/2026
  4. Tanzania vs Zambia Leo Oktoba 8 2025 Saa Ngapi?
  5. FIFA Yairuhusu Fountain Gate Kufanya Usajili Nje ya Dirisha la Usajili
  6. FIFA Yamteua Eng. Hersi Said Kuwa Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Vilabu ya Wanaume Duniani
  7. Djigui Diarra Ashinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Septemba 2025/2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo