Kikosi cha Simba Vs Nsingizini Hotspurs Leo 19/10/2025

Kikosi cha Simba Vs Nsingizini Hotspurs Leo 19/10/2025

Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, leo Jumapili tarehe 19 Oktoba 2025, watakuwa na jukumu kubwa la kuipeperusha bendera ya taifa la Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League).

Hii ni baada ya watani wao wa jadi Yanga SC kufungua raundi ya pili kwa kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Silver Strikers kutoka Malawi, hali iliyoweka mzigo mkubwa wa matumaini kwa Simba kufanya vizuri. Timu hiyo itakuwa mgeni wa Nsingizini Hotspurs kutoka Eswatini, mchezo utakaochezwa katika Uwanja wa Somhlolo kuanzia saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Kikosi cha Simba Vs Nsingizini Hotspurs Leo 19/10/2025

Maandalizi ya Simba SC kuelekea mechi ya leo

Simba SC inaingia katika mchezo huu ikiwa chini ya usimamizi wa kocha mpya Dimitar Pantev, aliyepokea mikoba baada ya kipindi kifupi cha uongozi wa Fadlu Davids na Hemed Suleiman ‘Morocco’.

Pantev, ambaye awali alikuwa akiinoa Gaborone United ya Botswana, timu ambayo Simba iliiondoa hatua ya awali kwa jumla ya mabao 2-1, sasa anakabiliwa na mtihani wake wa kwanza mkubwa katika klabu hiyo ya Msimbazi.

Akizungumza kuelekea mchezo wa leo, Pantev alieleza kuwa maandalizi yamekamilika vizuri na wachezaji wako tayari kwa pambano hilo, japokuwa changamoto kubwa ni aina ya uwanja wa nyasi bandia na hali ya hewa baridi nchini Eswatini.

“Maandalizi yako sawa, ingawa mazingira ni tofauti kidogo kwa sababu tunatumia uwanja wenye nyasi bandia. Timu imepata motisha ya kutosha na tunatarajia kucheza kwa nidhamu na ufanisi mkubwa,” alisema Pantev.

“Hatutabadilisha mbinu zetu. Tutacheza soka letu kama tulivyojiandaa, na naamini kila kitu kitaenda sawa. Ni kweli kuna baridi sana, lakini hiyo ni changamoto kwa pande zote mbili.”

Hata hivyo, Simba itakosa huduma za wachezaji wawili muhimu Mohammed Bajaber na Moussa Camara ambao wote wanakabiliwa na majeraha, kama ilivyothibitishwa na meneja mkuu wa timu hiyo, Dimitar Pantev.

Kikosi cha Simba Vs Nsingizini Hotspurs Leo 19/10/2025

Kikosi cha Simba kinatarajiwa kuongozwa na nyota wake wa kimataifa wakiwa na lengo la kupata matokeo chanya kabla ya mchezo wa marudiano utakaofanyika Oktoba 26, 2025, jijini Dar es Salaam. Mshindi wa jumla wa michezo hiyo miwili atafuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2025/2026. Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo, wachezaji wapo katika hali nzuri ya kiafya na morali iko juu, isipokuwa Bajaber na Camara ambao wataendelea kuwa nje kutokana na majeraha.

Hapa chini Tutakuletea kikosi cha Simba Sc kitakachoanza dhidi ya Nsingizini Hotspurs mara tu baada ya Kutangazwa.

Kikosi cha Simba Vs Nsingizini Hotspurs Leo

Historia ya Simba nchini Eswatini

Mara ya mwisho Simba SC kucheza nchini Eswatini ilikuwa mnamo Desemba 4, 2018, ambapo iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Mbabane Swallows. Katika mchezo huo, nyota Clatous Chama alifunga mabao mawili (dakika ya 28 na 32), Emmanuel Okwi (dk 51), na Meddie Kagere (dk 62).

Simba iliondosha Mbabane Swallows kwa jumla ya mabao 8-1, baada ya kushinda 4-1 katika mchezo wa kwanza uliochezwa jijini Dar es Salaam. Wafungaji katika mchezo huo walikuwa John Bocco (dk 8, 33), Meddie Kagere (dk 84), na Clatous Chama (dk 90+1).Historia hii inatoa matumaini kwa mashabiki wa Simba kuwa timu yao inaweza kurudia ubora uleule inapocheza ugenini dhidi ya wapinzani wa Eswatini.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Matokeo ya Silver Strikers vs Yanga SC Leo 18/10/2025
  2. Timu Zilizofuzu Kombe la Dunia 2026
  3. Msimamo wa Ligi Kuu Zanzibar PBZ 2025/2026
  4. Majina Ya Usaili Kusimamia Uchaguzi 2025 Jimbo La Temeke, Mbagala na Chamazi
  5. Pacome Anukia Kombe la Dunia Baada ya Ushindi 7-0 Dhidi ya Shelisheli
  6. Zimbabwe Yainyima Nafasi Afrika Kusini Kufuzu Kombe la Dunia
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo