Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Mikoa Yote (NECTA PSLE Results)

Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Mikoa Yote (NECTA PSLE Results)

Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2025 yanatarajiwa kutangazwa siku yoyote kuanzia sasa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA). Huu ni mtihani wa kitaifa unaohusisha maelfu ya wanafunzi wa shule za msingi kote nchini, na matokeo yake ndiyo yatakayoamua ni nani ataendelea na Kidato cha Kwanza kwa mwaka wa masomo 2026. Kwa mujibu wa ratiba ya NECTA, mtihani wa mwaka huu ulifanyika kuanzia tarehe 10 hadi 11 Septemba 2025, ukihusisha shule za umma na binafsi katika mikoa yote ya Tanzania Bara.

Kwa sasa, wazazi, walimu na wanafunzi wanasubiri kwa hamu kubwa Matokeo ya Darasa la Saba 2025 NECTA, ambayo mara nyingi hutolewa kati ya miezi miwili hadi mitatu baada ya kukamilika kwa mitihani. NECTA imethibitisha kuwa mchakato wa usahihishaji na uhakiki wa mitihani unaendelea kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha ubora na uadilifu wa matokeo kabla ya kutangazwa rasmi.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Katibu Mtendaji wa NECTA, Prof. Said A. Mohamed, alisisitiza kuwa taarifa rasmi za matokeo zitapatikana tu kupitia tovuti ya Baraza: www.necta.go.tz . Alionya dhidi ya kusambazwa kwa taarifa zisizo sahihi mitandaoni akisema, “Matokeo ya Darasa la Saba 2025 bado hayajatangazwa, na yatatolewa mara tu baada ya mchakato wa uhakiki kukamilika.”

Kwa hiyo, wazazi na wanafunzi wanashauriwa kufuatilia taarifa rasmi pekee. Tovuti hii (Habariforum) itakuletea viungo vya matokeo kwa kila mkoa mara tu NECTA itakapotangaza rasmi.

Historia Fupi ya NECTA na Majukumu Yake

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) lilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na. 21 ya mwaka 1973, likiwa na jukumu kuu la kusimamia na kuendesha mitihani yote ya kitaifa nchini Tanzania. Uamuzi wa kuanzisha NECTA ulifuatia hatua ya Tanzania Bara kujiondoa katika Baraza la Mitihani la Afrika Mashariki (EAEC) mwaka 1971, ili iweze kuendesha mitihani yake kwa kujitegemea.

Kabla ya hapo, mitihani ya sekondari na shule za msingi ilikuwa ikifanywa chini ya Cambridge Local Examinations Syndicate kwa ushirikiano na East African Syndicate. Kuanzia mwaka 1947 hadi 1971, wanafunzi wa Tanzania walishiriki mitihani ya kigeni kama School Certificate na Higher School Certificate, kabla ya mfumo wa ndani wa Tanzania kuanzishwa rasmi.

Baada ya kuanzishwa kwa NECTA, masuala ya mitaala yaliendelea kushughulikiwa na Wizara ya Elimu na Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam, hadi pale Taasis ya Kuendeleza Mitaala (ICD) ilipoanzishwa mwaka 1975, ambayo baadaye ilibadilishwa jina na kuwa Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) mwaka 1993.

Kwa sasa, NECTA ina zaidi ya wafanyakazi 350, na makao yake makuu yako Kijitonyama, karibu na Mwenge – Dar es Salaam.

Ni Lini NECTA Itatangaza Matokeo ya Darasa la Saba 2025?

Kwa sasa, Matokeo ya Darasa la Saba 2025 bado hayajatangazwa. Hata hivyo, taarifa rasmi kutoka NECTA zinaonesha kuwa matokeo yanatarajiwa kutolewa muda wowote kuanzia mwezi Novemba 2025, mara tu baada ya mchakato wa usahihishaji kukamilika.

Katibu Mtendaji wa NECTA, Prof. Said A. Mohamed, amewataka wananchi kuwa watulivu na kusubiri tangazo rasmi:

“Kuhusu yanayoenea mitandaoni, taarifa hizo si sahihi. Matokeo ya Darasa la Saba 2025 bado hayajatangazwa, na yatatolewa mara tu baada ya mchakato wa uhakiki kukamilika. Wananchi wasome taarifa rasmi kupitia tovuti au mitandao ya kijamii ya NECTA pekee.”
— Prof. Said A. Mohamed, Katibu Mtendaji wa NECTA.

Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Mikoa Yote (NECTA PSLE Results)

Chanzo rasmi: Akaunti Rasmi ya NECTA – Instagram @necta_tanzania

Lengo Kuu la Mtihani wa Darasa la Saba

Mtihani wa Darasa la Saba (PSLE) umeundwa ili:

  1. Kupima maarifa na ujuzi walioupata wanafunzi katika kipindi cha miaka saba ya elimu ya msingi.
  2. Kuthibitisha uwezo wa mwanafunzi katika kutumia maarifa hayo kutatua changamoto za kimaisha.
  3. Kutambua wanafunzi wenye uwezo wa kuendelea na elimu ya sekondari au taasisi za mafunzo ya ufundi.

Kwa maneno mengine, matokeo haya si tu kipimo cha darasani ni kiashiria cha jinsi mfumo mzima wa elimu unavyotekelezwa nchini.

Masomo Yanayopimwa Katika Mtihani wa Darasa la Saba

Mtihani wa PSLE unahusisha masomo sita muhimu ambayo ni msingi wa elimu ya msingi:

  1. Kiswahili
  2. English Language
  3. Hisabati (Mathematics)
  4. Sayansi na Teknolojia (Science and Technology)
  5. Uraia na Maadili (Civic and Moral Education)
  6. Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi (Social Studies and Vocational Skills)

Kupitia masomo haya, NECTA hupima ujuzi wa kitaaluma na kitabia, ikiweka msingi wa mwanafunzi kuelekea elimu ya sekondari.

Jinsi Matokeo ya Darasa la Saba 2025/2026 NECTA Yatatangazwa

Baada ya kukamilika kwa uchambuzi wa mitihani, NECTA hutangaza matokeo rasmi kupitia tovuti yake ya https://www.necta.go.tz
.
Matokeo ya shule zote huonyeshwa kwa mpangilio wa:

  • Majina ya shule na namba za usajili (mfano: PS0205005)
  • Jinsia ya mwanafunzi (M au F)
  • Alama za kila somo na wastani wa ufaulu
  • Daraja la ufaulu (A–E)

Mfano halisi wa matokeo unaweza kuonekana kwenye matokeo ya shule ya Buyuni I (PS0205005) ya mwaka 2024, ambapo NECTA ilionesha taarifa kama:

  • “Kiswahili – B, English – C, Hisabati – C, Sayansi – B, Uraia – A, Wastani wa Daraja B (Nzuri).”

Shule pia hupatiwa Wastani wa Shule (kwa alama na daraja), kwa mfano:

  • “Wastani wa Shule: 145.22 – Daraja C (Nzuri).”

Kwa mwaka 2025, matokeo yatatolewa kwa mfumo huo huo wa kidigitali, yakipatikana kupitia tovuti rasmi ya NECTA au kwa njia ya SMS kupitia mitandao ya simu.

Jinsi Matokeo ya Darasa la Saba 2025/2026 NECTA Yatatangazwa

Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Mikoa Yote (NECTA PSLE Results)

Baada ya NECTA kutangaza rasmi Matokeo ya Darasa la Saba 2025, wanafunzi na wazazi wanaweza kuyapata matokeo ya shule zilizopo mikoa yote Tanzania kupitia njia mbili kuu ambazo zimeandaliwa kwa urahisi na usalama wa taarifa.

1. Kuangalia Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Kupitia Tovuti Rasmi ya NECTA

Njia hii ndiyo ya kitaaluma na ya kuaminika zaidi. Matokeo yote ya PSLE huchapishwa katika tovuti rasmi ya Baraza la Mitihani mara tu baada ya kutolewa. Fuata hatua hizi kuangalia matokeo yako:

  1. Tembelea tovuti rasmi ya NECTA: www.necta.go.tz
  2. Bonyeza sehemu ya “Matokeo” au “Results” kwenye ukurasa wa mwanzo.
  3. Chagua kipengele “Matokeo ya Darasa la Saba 2025 (PSLE 2025)”.
  4. Chagua mkoa na wilaya unakotoka.
  5. Tafuta jina la shule yako kisha bonyeza kuona orodha ya majina ya wanafunzi.
  6. Tafuta jina lako au namba ya mtihani kuona alama zako.
  7. Unaweza kupakua au kuchapisha matokeo yako kwa kumbukumbu.
Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2025/2026 NECTA
Kuangalia Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Kupitia Tovuti Rasmi ya NECTA

Kuangalia Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Mikoa Yote – Njia Fupi (Shortcut)

Ili kurahisisha zaidi mchakato wa kuangalia Matokeo ya Darasa la Saba 2025 (PSLE), hapa Habariforum tutakuwezesha kupata matokeo yako kwa urahisi kupitia viungo rasmi vya moja kwa moja.

Mara tu baada ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) kutangaza rasmi matokeo, viungo vya kila mkoa vitapatikana hapa chini. Unachohitajika kufanya ni:

  1. Bofya jina la mkoa ambako shule yako ya msingi ipo.
  2. Utaelekezwa moja kwa moja kwenye ukurasa wa mkoa husika wenye orodha ya wilaya zote.
  3. Chagua jina la wilaya yako, kisha bofya ili kufungua orodha ya shule zote zilizopo katika wilaya hiyo.
  4. Tafuta jina la shule yako, kisha bofya kuona matokeo kamili ya wanafunzi wa shule hiyo.

Njia hii imeundwa kurahisisha upatikanaji wa matokeo bila kupitia hatua nyingi au tovuti zisizo rasmi. Habariforum itahakikisha viungo hivi vinapatikana mara tu NECTA itakapoweka matokeo mtandaoni kupitia tovuti yake rasmi www.necta.go.tz

Bofya Jina la Mkoa Kuangalia Matokeo kwa shule zilizopo ndani ya mkoa husika:

ARUSHA PWANI
DAR ES SALAAM RUKWA
DODOMA RUVUMA
IRINGA SHINYANGA
KAGERA SINGIDA
KIGOMA TABORA
KILIMANJARO TANGA
LINDI MANYARA
MARA GEITA
MBEYA KATAVI
MOROGORO NJOMBE
MTWARA SIMIYU
MWANZA SONGWE

2. Kuangalia Matokeo Kupitia Shule Uliyofanyia Mtihani

Kwa wazazi na wanafunzi wanaopendelea njia ya kawaida, shule zote za msingi ambazo zilitumika kama vituo vya mitihani hupokea nakala rasmi za matokeo mara baada ya kutolewa. Wanafunzi wanaweza kwenda shuleni na kuangalia majina kwenye orodha ya matokeo inayobandikwa kwenye ubao wa matangazo. Njia hii ni muhimu hasa kwa maeneo yenye changamoto ya upatikanaji wa mtandao.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Mambo 5 ya Muhimu Kujua Wakati Wa Kusubiri Kutangazwa kwa Matokeo ya Darasa la Saba 2025
  2. NECTA Standard Seven Results 2025: Updates on PSLE Results for All Regions in Tanzania
  3. Bodi ya Mikopo HESLB Yatangaza Awamu ya Kwanza ya Wanafunzi Waliopata Mkopo 2025/2026
  4. Majina ya Waliopata Mkopo 2025/2026 HESLB
  5. Jinsi ya Kuangalia kama Umepata Mkopo wa HESLB 2025/2026
  6. Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Mkoa wa Kilimanjaro
  7. Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Mkoa wa Mbeya
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo