Matokeo ya Yanga Vs Silver Strikers Leo 25/10/2025

Matokeo ya Yanga Vs Silver Strikers Leo 25/10/2025

LEO, Wananchi Yanga SC watakuwa dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kuwakaribisha Silver Strikers kutoka Malawi katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League).

Mechi hii itapigwa kuanzia saa 11:00 jioni na itarushwa mubashara kupitia AzamSports3HD. Wananchi wanaingia uwanjani wakiwa na kiu ya kupata ushindi wa zaidi ya bao moja ili kufuzu hatua ya makundi ya michuano hii mikubwa barani Afrika.

Katika Mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Malawi ulimalizika kwa mabingwa wa ligi kuu ya NBC Yanga SC kupoteza kwa bao 1–0, hivyo katika mchezo wa leo, mabingwa hao wa Tanzania Bara wanahitaji ushindi wa angalau mabao 2–0 ili kutinga hatua ya makundi. Iwapo watashinda 1–0, matokeo yataamuliwa kwa mikwaju ya penalti.

Tathmini ya Mchezo na Matarajio

Baada ya kipigo cha awali, Yanga SC ilifanya mabadiliko ya benchi la ufundi na sasa inakuwa chini ya Kaimu Kocha Mkuu Patrick Mabedi, ambaye alichukua nafasi hiyo baada ya kuondoka kwa Romain Folz. Mabedi, ambaye ni raia wa Malawi, ameahidi kuingia kwenye mchezo huu kwa nidhamu ya juu na kasi katika kushambulia, huku akisisitiza umuhimu wa kutoruhusu bao lolote nyumbani.

Akizungumza kuelekea mchezo huu muhimu, Mabedi alisema:

“Tupo nyumbani na tutakuwa mbele ya mashabiki wetu. Tunatakiwa kuonyesha njaa ya ushindi, kumaliza mechi mapema, na kuhakikisha kila nafasi tunayoipata tunaitumia vizuri.”

Kwa upande mwingine, nahodha msaidizi Dickson Job ameahidi kuwa timu itapambana kwa nguvu zote kuhakikisha inarejesha heshima ya klabu hiyo kubwa barani Afrika. Job alisema:

“Tunajua umuhimu wa mchezo huu. Tutapambana kwa jasho na damu ili tuingie hatua ya makundi. Nawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kutusapoti.”

Matokeo ya Yanga Vs Silver Strikers Leo 25/10/2025

Kikosi cha Yanga Vs Silver Strikers Leo 25/10/2025

Kocha Patrick Mabedi ametangaza kikosi cha kwanza (Starting XI) kitakachoanza dhidi ya Silver Strikers kama ifuatavyo:

Kikosi cha Kuanza:

  1. Diarra (Kipa)
  2. Israh
  3. Hussein
  4. Job (Nahodha Msaidizi)
  5. Bacca
  6. Abuya
  7. Maxi
  8. Mudathir
  9. Dube
  10. Doumbia
  11. Pacome

Wachezaji wa Akiba: Msheiry, Mwamynyeto, Boka, Kibwana, Andabwile, Houma, Chikola, Edmund, Boyeli.

Waamuzi na Maandalizi ya Mchezo

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limewapanga waamuzi kutoka Benin kusimamia mchezo huu. Mwamuzi wa kati atakuwa Adissa Abdul Raphiou Ligali, akisaidiwa na Lucien Todégnon Hontonnou (Benin) na Lamien Dofinte Adolphe (Burkina Faso).

Yanga SC imetangaza kuwa hakutakuwa na kiingilio, hatua inayolenga kuwapa mashabiki fursa ya kuujaza Uwanja wa Benjamin Mkapa na kuipa timu nguvu ya ziada ya kusaka ushindi.

Matokeo ya Yanga Vs Silver Strikers Leo 25/10/2025

Yanga Sc VS Silver Strikers
  • 🏆 #CAFCL
  • 🆚 Silver Strikers 🇲🇼 (H)
  • 🗓️ 25 October 2025
  • 🏟️ Benjamin Mkapa
  • ⏱️ 5:00PM

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Singida BS VS Flambeau Leo 25/10/2025 Saa Ngapi?
  2. Yanga Vs Silver Strikers Leo 25/10/2025 Saa Ngapi?
  3. Matokeo ya Azam vs KMKM Leo 24/10/2025
  4. Yanga SC Yatangaza Kuachana na Kocha Wake Romain Folz
  5. Timu Zilizofuzu Kombe la Dunia 2026
  6. Msimamo wa Ligi Kuu Zanzibar PBZ 2025/2026
  7. Matokeo ya Azam vs KMKM Leo 24/10/2025
  8. Pacome Anukia Kombe la Dunia Baada ya Ushindi 7-0 Dhidi ya Shelisheli
  9. Kaizer Chiefs Ya Thibitisha Kuachana na Kocha Nasreddine Nabi
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo