Matokeo ya Simba SC VS Nsingizini Leo 26/10/2025

Matokeo ya Simba SC VS Nsingizini Leo 26/10/2025

Leo Mnyama Simba SC anarejea katika dimba la Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam, kuikaribisha Nsingizini Hotspurs kutoka Eswatini katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League). Mchezo huu unatarajiwa kuanza saa 10:00 jioni, ukirushwa mubashara kupitia Azam Sports 1 HD.

Simba SC inaingia dimbani ikiwa na mtaji wa mabao 3-0, baada ya ushindi mnono walioupata kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Eswatini mnamo Oktoba 19, 2025. Ushindi huo umeipa Simba nafasi nzuri kuelekea hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika, lakini benchi la ufundi limesisitiza kuwa bado kazi haijaisha.

Kocha Msaidizi wa Simba SC, Selemani Matola, ameeleza kuwa licha ya ushindi wa ugenini, timu yake haijaridhika na matokeo hayo na inalenga kuendeleza ubora huo nyumbani.

“Ni kweli tuna uzoefu mkubwa katika hii michuano, lakini hatutaki kurudia makosa ya misimu kadhaa iliyopita. Hii ni mechi nyingine yenye uhitaji mkubwa kama ile ya awali ugenini,” alisema Matola wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.

Ameongeza kuwa timu inahitaji kuonyesha ubora zaidi mbele ya mashabiki wake, hasa kwa kuwa kila mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika una umuhimu wa kipekee katika kujenga historia ya klabu hiyo.

Matokeo ya Simba SC VS Nsingizini Leo 26/10/2025

Fuatilia Matokeo ya Simba SC VS Nsingizini Leo 26/10/2025 Hapa

Simba Sc  VS Nsingizini

Hali ya Kikosi: Wachezaji Wote Wapo Fiti

Akizungumzia hali ya wachezaji kabla ya mchezo wa leo, Matola alithibitisha kuwa beki Wilson Nangu, ambaye alipata majeraha katika mechi ya kwanza, yupo tayari kurudi uwanjani. Vilevile, kiungo mshambuliaji Mohamed Bajaber ameendelea vizuri chini ya programu maalumu ya matibabu na anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachopambana dhidi ya Nsingizini.

Kapombe: “Tunataka kuandika historia mpya”

Nahodha wa Simba SC, Shomari Kapombe, amesema wachezaji wamejiandaa kikamilifu kuhakikisha wanadumisha ubora waliouonyesha katika mechi ya kwanza.

“Niwaombe mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi, kwa sababu mechi ya kwanza hawakupata nafasi hiyo. Hii ni fursa nyingine nzuri ya kuendelea kuandika historia mpya kwa umoja wetu,” alisema Kapombe.

Aidha, Kapombe alisisitiza dhamira yake binafsi kama nahodha kuhakikisha Simba inasonga mbali zaidi msimu huu.
“Nina majukumu mazito ya kuipeleka Simba mbali zaidi ya hapa. Naamini kwa umoja na ushirikiano wetu tutafikia malengo tuliyoyapanga kwa msimu huu,” aliongeza.

Simba SC inahitaji sare au ushindi wowote ili kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Droo ya hatua hiyo inatarajiwa kufanyika Novemba 3, 2025, jijini Johannesburg, Afrika Kusini.

Nsingizini: “Kila kitu kinawezekana uwanjani”

Kwa upande wa wapinzani wao, Kocha Mkuu wa Nsingizini Hotspurs, Mandla Qhogi, amesema pamoja na kupoteza kwa mabao 3-0 katika mechi ya kwanza, kikosi chake bado kina imani ya kupambana kwa nguvu zote katika mchezo wa leo.

“Kabla ya mechi yetu ya kwanza hakuna aliyetarajia kama Simba ingeshinda ugenini kwa idadi kubwa ya mabao. Hii ni mechi nyingine ngumu, lakini tutapambana kadri ya uwezo wetu,” alisema Qhogi.

Ameongeza kuwa licha ya ugumu wa kupindua matokeo hayo, wachezaji wake wameahidi kupigania heshima ya taifa lao.

“Unapotaja miongoni mwa timu tano bora Barani Afrika huwezi kuiacha Simba. Tunajua tunakwenda kucheza kwenye uwanja mkubwa wenye mashabiki zaidi ya 60,000, hivyo tunajua tunakabiliwa na kazi ngumu,” alisema Qhogi.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kikosi cha Simba SC VS Nsingizini Leo 26/10/2025
  2. Simba SC VS Nsingizini Leo 26/10/2025 Saa Ngapi?
  3. Timu Zilizofuzu Makundi Kombe la Shirikisho Afrika CAF 2025/2026
  4. Timu Zilizofuzu Makundi Klabu Bingwa Afrika 2025/2026
  5. Cv ya Pedro Gonçalves Kocha Mpya wa Yanga Sc 2025/2026
  6. Yanga SC Yamtangaza Pedro Gonçalves Kama Kocha Mkuu Mpya wa Timu
  7. Matokeo ya Yanga Vs Silver Strikers Leo 25/10/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo