Yaliyomo: Taarifa Kuhusu Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2025/2026 NECTA (Matokeo ya Darasa la Saba 2025) | NECTA PSLE Results 2025, Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Darasa la Saba, Matokeo ya Shule za Msingi Tanzania 2025
Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2025/2026 NECTA
Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba ni miongoni mwa matokeo yanayosimamiwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) na ambayo husubiriwa kwa hamu kubwa na Watanzania kila mwaka.
Matokeo ya Darasa la Saba 2025 ndiyo yatakayotumika kuamua ni wanafunzi gani watachaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza kwa mwaka wa masomo 2026, hivyo kupata matokeo mazuri ni ndoto ya kila mwanafunzi aliyehitimu elimu ya msingi.
Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba, unaojulikana pia kama Primary School Leaving Examination (PSLE), hufanyika kila mwaka katika wiki ya pili ya mwezi Septemba. Kwa mwaka 2025, mtihani ulianza tarehe 10 Septemba 2025 (Jumatano) na kukamilika tarehe 11 Septemba 2025 (Alhamisi), kwa mujibu wa ratiba rasmi ya NECTA.
Historia Fupi ya NECTA na Majukumu Yake
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) lilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na. 21 ya mwaka 1973, likiwa na jukumu kuu la kusimamia na kuendesha mitihani yote ya kitaifa nchini Tanzania. Uamuzi wa kuanzisha NECTA ulifuatia hatua ya Tanzania Bara kujiondoa katika Baraza la Mitihani la Afrika Mashariki (EAEC) mwaka 1971, ili iweze kuendesha mitihani yake kwa kujitegemea.
Kabla ya hapo, mitihani ya sekondari na shule za msingi ilikuwa ikifanywa chini ya Cambridge Local Examinations Syndicate kwa ushirikiano na East African Syndicate. Kuanzia mwaka 1947 hadi 1971, wanafunzi wa Tanzania walishiriki mitihani ya kigeni kama School Certificate na Higher School Certificate, kabla ya mfumo wa ndani wa Tanzania kuanzishwa rasmi.
Baada ya kuanzishwa kwa NECTA, masuala ya mitaala yaliendelea kushughulikiwa na Wizara ya Elimu na Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam, hadi pale Taasis ya Kuendeleza Mitaala (ICD) ilipoanzishwa mwaka 1975, ambayo baadaye ilibadilishwa jina na kuwa Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) mwaka 1993.
Kwa sasa, NECTA ina zaidi ya wafanyakazi 350, na makao yake makuu yako Kijitonyama, karibu na Mwenge – Dar es Salaam.
Lengo Kuu la Mtihani wa Darasa la Saba
Mtihani wa Darasa la Saba (PSLE) umeundwa ili:
- Kupima maarifa na ujuzi walioupata wanafunzi katika kipindi cha miaka saba ya elimu ya msingi.
- Kuthibitisha uwezo wa mwanafunzi katika kutumia maarifa hayo kutatua changamoto za kimaisha.
- Kutambua wanafunzi wenye uwezo wa kuendelea na elimu ya sekondari au taasisi za mafunzo ya ufundi.
Kwa maneno mengine, matokeo haya si tu kipimo cha darasani ni kiashiria cha jinsi mfumo mzima wa elimu unavyotekelezwa nchini.
Masomo Yanayopimwa Katika Mtihani wa Darasa la Saba
Mtihani wa PSLE unahusisha masomo sita muhimu ambayo ni msingi wa elimu ya msingi:
- Kiswahili
- English Language
- Hisabati (Mathematics)
- Sayansi na Teknolojia (Science and Technology)
- Uraia na Maadili (Civic and Moral Education)
- Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi (Social Studies and Vocational Skills)
Kupitia masomo haya, NECTA hupima ujuzi wa kitaaluma na kitabia, ikiweka msingi wa mwanafunzi kuelekea elimu ya sekondari.
Ni Lini NECTA Itatangaza Matokeo ya Darasa la Saba 2025?
Kufuatia uvumi ulioenea mitandaoni kwamba Matokeo ya Darasa la Saba 2025 (PSLE) yametangazwa, Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limejitokeza na kukanusha taarifa hizo rasmi.
Kupitia kwa Katibu Mtendaji wa NECTA, Prof. Said A. Mohamed, baraza limethibitisha kuwa hadi sasa matokeo hayo bado hayajatangazwa, na kwamba yatatolewa mara tu baada ya kukamilika kwa mchakato wa uhakiki na usahihishaji wa kitaalamu.
“Kuhusu yanayoendelea kwenye mitandao, taarifa hizo si sahihi. Ndugu waandishi wa habari, nitoe elimu kwamba taarifa zote za Baraza ni rasmi endapo zinatoka kwenye mitandao ya kijamii rasmi ya NECTA au tovuti rasmi ya Baraza la Mitihani. Matokeo hayo ya Darasa la Saba bado hayajatangazwa, na yatatolewa kwa mujibu wa taratibu za kisheria pindi yatakapokuwa tayari. Bloggers wapo wengi mitandaoni, nafikiri wanajaribu kuvutia watazamaji,”
— Prof. Said A. Mohamed, Katibu Mtendaji wa NECTA.
Tazama Taarifa Rasmi Kutoka NECTA: Hapa chini ni chapisho rasmi la NECTA kupitia ukurasa wao wa Instagram kuhusu taarifa ya matokeo ya Darasa la Saba 2025.
View this post on Instagram
(Chanzo: Akaunti Rasmi ya NECTA – Instagram @nectatanzania)
Taarifa hii imeweka wazi kwamba wazazi, wanafunzi na walimu wanapaswa kuwa makini na taarifa zisizo rasmi zinazochapishwa mitandaoni. NECTA imeeleza kuwa chanzo pekee cha taarifa sahihi kuhusu matokeo ni tovuti rasmi: www.necta.go.tz
Jinsi Matokeo ya Darasa la Saba 2025/2026 NECTA Yatatangazwa
Baada ya kukamilika kwa uchambuzi wa mitihani, NECTA hutangaza matokeo rasmi kupitia tovuti yake ya https://www.necta.go.tz
.
Matokeo ya shule zote huonyeshwa kwa mpangilio wa:
- Majina ya shule na namba za usajili (mfano: PS0205005)
- Jinsia ya mwanafunzi (M au F)
- Alama za kila somo na wastani wa ufaulu
- Daraja la ufaulu (A–E)
Mfano halisi wa matokeo unaweza kuonekana kwenye matokeo ya shule ya Buyuni I (PS0205005) ya mwaka 2024, ambapo NECTA ilionesha taarifa kama:
- “Kiswahili – B, English – C, Hisabati – C, Sayansi – B, Uraia – A, Wastani wa Daraja B (Nzuri).”
Shule pia hupatiwa Wastani wa Shule (kwa alama na daraja), kwa mfano:
- “Wastani wa Shule: 145.22 – Daraja C (Nzuri).”
Kwa mwaka 2025, matokeo yatatolewa kwa mfumo huo huo wa kidigitali, yakipatikana kupitia tovuti rasmi ya NECTA au kwa njia ya SMS kupitia mitandao ya simu.
Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Darasa la Saba 2025/2026
Baada ya NECTA kutangaza rasmi Matokeo ya Darasa la Saba 2025, wanafunzi na wazazi wanaweza kuyapata kupitia njia tatu kuu ambazo zimeandaliwa kwa urahisi na usalama wa taarifa.
1. Kuangalia Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Kupitia Tovuti Rasmi ya NECTA
Njia hii ndiyo ya kitaaluma na ya kuaminika zaidi. Matokeo yote ya PSLE huchapishwa katika tovuti rasmi ya Baraza la Mitihani mara tu baada ya kutolewa. Fuata hatua hizi kuangalia matokeo yako:
- Tembelea tovuti rasmi ya NECTA: www.necta.go.tz
- Bonyeza sehemu ya “Matokeo” au “Results” kwenye ukurasa wa mwanzo.
- Chagua kipengele “Matokeo ya Darasa la Saba 2025 (PSLE 2025)”.
- Chagua mkoa na wilaya unakotoka.
- Tafuta jina la shule yako kisha bonyeza kuona orodha ya majina ya wanafunzi.
- Tafuta jina lako au namba ya mtihani kuona alama zako.
- Unaweza kupakua au kuchapisha matokeo yako kwa kumbukumbu.

Ili kurahisisha zaidi mchakato wa kuangalia Matokeo ya Darasa la Saba 2025 (PSLE), hapa Habariforum tutakuwezesha kupata matokeo yako kwa urahisi kupitia viungo rasmi vya moja kwa moja.
Mara tu baada ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) kutangaza rasmi matokeo, viungo vya kila mkoa vitapatikana hapa chini. Unachohitajika kufanya ni:
- Bofya jina la mkoa ambako shule yako ya msingi ipo.
- Utaelekezwa moja kwa moja kwenye ukurasa wa mkoa husika wenye orodha ya wilaya zote.
- Chagua jina la wilaya yako, kisha bofya ili kufungua orodha ya shule zote zilizopo katika wilaya hiyo.
- Tafuta jina la shule yako, kisha bofya kuona matokeo kamili ya wanafunzi wa shule hiyo.
Njia hii imeundwa kurahisisha upatikanaji wa matokeo bila kupitia hatua nyingi au tovuti zisizo rasmi. Habariforum itahakikisha viungo hivi vinapatikana mara tu NECTA itakapoweka matokeo mtandaoni kupitia tovuti yake rasmi www.necta.go.tz
Bofya Jina la Mkoa Kupata Matokeo:
| ARUSHA | PWANI |
| DAR ES SALAAM | RUKWA |
| DODOMA | RUVUMA |
| IRINGA | SHINYANGA |
| KAGERA | SINGIDA |
| KIGOMA | TABORA |
| KILIMANJARO | TANGA |
| LINDI | MANYARA |
| MARA | GEITA |
| MBEYA | KATAVI |
| MOROGORO | NJOMBE |
| MTWARA | SIMIYU |
| MWANZA | SONGWE |
2. Kuangalia Matokeo Kupitia Shule Uliyofanyia Mtihani
Kwa wazazi na wanafunzi wanaopendelea njia ya kawaida, shule zote za msingi ambazo zilitumika kama vituo vya mitihani hupokea nakala rasmi za matokeo mara baada ya kutolewa. Wanafunzi wanaweza kwenda shuleni na kuangalia majina kwenye orodha ya matokeo inayobandikwa kwenye ubao wa matangazo. Njia hii ni muhimu hasa kwa maeneo yenye changamoto ya upatikanaji wa mtandao.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Mambo 5 ya Muhimu Kujua Wakati Wa Kusubiri Kutangazwa kwa Matokeo ya Darasa la Saba 2025
- NECTA Standard Seven Results 2025: Updates on PSLE Results for All Regions in Tanzania
- Bodi ya Mikopo HESLB Yatangaza Awamu ya Kwanza ya Wanafunzi Waliopata Mkopo 2025/2026
- Majina ya Waliopata Mkopo 2025/2026 HESLB
- Jinsi ya Kuangalia kama Umepata Mkopo wa HESLB 2025/2026
- Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Mkoa wa Kilimanjaro
- Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Mkoa wa Mbeya









Leave a Reply