Kariakoo Dabi Yapigwa Kalenda Kutoka Desemba 13 Hadi Machi Mwakani
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara imetangaza maboresho ya ratiba ambayo yamesababisha mabadiliko makubwa katika mchezo wa Kariakoo Dabi. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mechi ya mzunguko wa kwanza kati ya Yanga SC na Simba SC ambayo awali ilipangwa kuchezwa Desemba 13 mwaka huu, sasa itafanyika Machi 1 mwakani katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Marekebisho haya yametangazwa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kama sehemu ya upangaji upya wa ratiba ya msimu. Mabadiliko hayo yanafanya timu hizo mbili kukutana tena ndani ya kipindi cha miezi miwili, kwa kuwa mchezo wa marudiano umepangwa kuchezwa Mei 3, 2025.
Katika taarifa hiyo hiyo ya marekebisho, TPLB pia imeweka ratiba mpya kwa michezo mingine iliyokuwa imeahirishwa. Mchezo kati ya TRA United na Simba SC, uliotakiwa kufanyika Oktoba 30, sasa umepangwa kuchezwa Desemba 3 mwaka huu. Aidha, mchezo kati ya Singida Black Stars uliokuwa upigwe siku hiyo hiyo, nao umehamishiwa Desemba 3, huku Tanzania Prisons dhidi ya Yanga ukipangwa kuchezwa Desemba 2 mwaka huu.
Ratiba hio mpya inaonyesha pia kuwa msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2025/2026 utamalizika Mei 29, 2026 katika mechi za raundi ya 30. Msimu huo unatarajiwa kusimama kwa siku 46 kupisha Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika Morocco kuanzia Desemba 21 mwaka huu hadi Januari 18 mwakani.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo iliyoboreshwa, TPLB imeeleza pia kuwa hafla ya Tuzo za Ligi Kuu kwa msimu wa 2024/2025 itafanyika Desemba 5, 2025.
Marekebisho haya yamefanya mchezo wa Kariakoo Dabi uliopangwa kutimua vumbi Desemba 13 kusogezwa Hadi Machi Mwakani, na kuifanya Machi kuwa mwezi utakaoleta mvutano mpya kati ya miamba hiyo miwili ya soka nchini wakati mashindano ya Ligi Kuu yakiendelea kukimbiza msimu wa 2025/2026.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Pantev Aandaa Mbinu Kali za kuizamisha Petro de Luanda Ligi ya Mabingwa Afrika
- Hat-Trick za Fernandes na Neves Zaipeleka Ureno Kombe la Dunia Baada ya Kuichapa Armenia 9-1
- Lyon Karibu Kumsajili Endrick Kutoka Real Madrid
- Wachezaji wa Simba Walioitwa Timu za Taifa November 2025
- Matokeo ya Yanga vs KMC Leo 09/11/2025
- Ratiba ya Yanga Klabu Bingwa 2025/2026









Leave a Reply