Yanga vs As Far Leo 22/11/2025 Saa Ngapi?
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC, leo watashuka dimbani kuanza safari yao ya kuiwakilisha Tanzania katika hatua ya makundi ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika, ambapo watakuwa na kibarua cha kuvaana na AS Far katika uwanja wa New Amaan Complex. Mchezo huu unatarajiwa kuvutia mashabiki lukuki kutokana na umuhimu wake kwa safari ya Yanga katika kampeni za bara.
Hii ni mechi ya kwanza kwa klabu hiyo katika kundi lao, na mashabiki wamekuwa wakiusubili mchezo huu wa ufunguzi kwa hamu kubwa huku wakiangalia kwa matarajio makubwa namna kikosi cha Yanga kitakavyoanza kampeni zao za CAFCL msimu huu.
Muda wa Mchezo: Yanga vs AS Far Leo Saa Ngapi?
Kwa mashabiki wanaohitaji kufahamu muda rasmi wa mchezo, taarifa zinaonyesha kuwa:
- 🗓️ Tarehe: 22 Novemba 2025
- ⏱️ Saa ya Mchezo: 4:00 PM
- 🏟️ Uwanja: New Amaan Complex
- 🆚 Yanga SC vs AS Far
- 🏆 Michuano: CAF Champions League (CAFCL)
Hivyo, kwa swali kuu la mashabiki “Yanga vs As Far leo 22/11/2025 saa ngapi?” Jibu sahihi ni kwamba mchezo utaanza saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Umuhimu wa Mchezo kwa Yanga SC
Mchezo huu ni muhimu kwa Yanga kutokana na kuwa sehemu ya mikakati ya kuanza hatua ya makundi kwa kupata alama tatu muhimu. Mashabiki wanatarajia kuona kiwango cha juu, nidhamu ya mchezo, na mbinu mpya zitakazotumika katika uwanja wa nyumbani wa visiwani. Kwa kuwa huu ni mchezo wa nyumbani, matarajio ni makubwa zaidi kwa kikosi cha Yanga kuanza kwa ushindi ili kujipa nafasi nzuri ya kusonga mbele katika msimu huu wa michuano mikubwa ya vilabu barani Afrika.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Simba SC Yatambulisha Jezi Mpya Kwa Ajili ya Mechi za CAF 2025/2026
- Tuzo za CAF 2025 Kutolewa Leo Saa 3 Usiku Katika Hafla Kubwa Rabat Morocco
- Jezi Mpya za Yanga za Ligi ya Mabingwa Afrika CAF 2025/2026
- Kikosi cha Yanga Chawasili Zanzibar Kujiandaa na Mchezo wa AS FAR Rabat
- Kariakoo Dabi Yapigwa Kalenda Kutoka Desemba 13 Hadi Machi Mwakani
- Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Mikoa Yote (NECTA PSLE Results)
- Pantev Aandaa Mbinu Kali za kuizamisha Petro de Luanda Ligi ya Mabingwa Afrika








Leave a Reply