Kikosi cha Simba vs Petro De Luanda leo 23/11/2025
Baada ya Yanga SC kufungua pazia la michezo ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AS FAR, leo hii zamu inahamia kwa Simba SC ambao wataanza kutupa karata yao ya kwanza dhidi ya Petro de Luanda ya Angola. Mchezo huo wa kundi D unatarajiwa kuanza saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, ukiahidi ushindani mkali kutokana na uimara wa timu zote mbili. Hapa chini tunakuletea taarifa kamili pamoja na kikosi cha Simba vs Petro De Luanda leo 23/11/2025.
Muonekano wa Mchezo na Muktadha wa Kundi D
Mchezo huu wa kundi D unawakutanisha Simba, Petro Luanda, Esperance na Stade Malien. Ni kundi lenye ushindani mkubwa, na matokeo ya leo yana uzito wa moja kwa moja katika kupanga mwelekeo wa safari ya makundi.
Simba wanaingia kwenye mchezo huu wakitumia faida ya uwanja wa nyumbani, ambako wameonyesha uimara wa muda mrefu kwenye michuano ya CAF. Ingawa msimu huu wameambulia sare mbili mfululizo dhidi ya Gaborone (1-1) na Nsingizini (1-1), rekodi yao ya kutopoteza nyumbani kwenye CAF tangu Machi 29, 2024 inaendelea kuwa nguzo muhimu.
Tangu walipofungwa 1-0 na Al Ahly kwenye robo fainali ya 2024, Wekundu wa Msimbazi hawajapoteza tena wanapocheza Benjamin Mkapa wakicheza mechi nane, kushinda tano na kutoka sare tatu.
Kwa upande wa Petro Luanda, mchezo huu unawakuta wakiwa katika kiwango cha juu sana. Wameonyesha ukomavu wa kucheza popote wanapokwenda—ikiwa nyumbani au ugenini—na kufuzu hatua ya makundi kwa ushindi katika mechi zao zote nne za awali. Wamefunga jumla ya mabao 10 bila kuruhusu bao lolote, wakiwafunga Cercle de Joachim 6-0 na Stade d’Abidjan 4-0.
Kutokana na takwimu hizi, nguvu ya safu ya ushambuliaji ya Petro ndiyo inatajwa kuwa changamoto kuu kwa Simba, ingawa bado Simba wana faida ya rekodi imara katika michezo ya CAF pale nyumbani.
Kikosi cha Simba vs Petro De Luanda leo 23/11/2025
Wekundu wa Msimbazi wametangaza rasmi jeshi lao litakaloanza kuipambania jezi ya Simba leo dhidi ya Petro De Luanda katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Wachezaji wa Simba Watakao Anza Leo
- 22 Yakoub
- 5 Mlugo
- 7 Mutale
- 8 Kante
- 12 Kapombe (C)
- 18 Morice
- 23 De Reuck
- 30 Naby
- 31 Nangu
- 34 Mpanzu
- 35 Neo
Wachezaji wa Akiba: Abel, Duchu, Chamou, Semfuko, Ahuoa, Chasambi, Mwalimu, Sowah, Mkwala.

Kikosi hiki kinaashiria dhamira ya Simba kuanza kampeni zao za makundi kwa nguvu, huku Kapombe akiendelea kuongoza safu ya ulinzi kama nahodha, na viungo pamoja na washambuliaji wakitarajiwa kutoa kasi na ubunifu utakaohitajika kuwavunja wapinzani wao kutoka Angola.
Mapendekezo ya Mhariri:








Leave a Reply