Ratiba ya Mechi za Ligi Kuu NBC Leo 04/12/2025

Ratiba ya Mechi za Ligi Kuu NBC Leo 04/12/2025

Ligikuu ya NBC inaendelea leo ambapo miamba wawili wa soka la Tanzania, Simba SC na Yanga SC, wanarejea katika majukumu ya ligi baada ya kumaliza michezo yao ya awali kwenye hatua ya makundi ya CAF.

Kwa mashabiki wa soka nchini, hii ni siku muhimu kwani timu hizo zitashuka dimbani kusaka pointi muhimu katika harakati za kuimarisha nafasi zao kwenye msimamo wa ligi. Simba SC watakuwa na kibarua dhidi ya Mbeya City, huku Yanga SC wakipambana vikali na Fountain Gate katika mchezo utakaoamua mustakabali wa pointi tatu muhimu

1. Simba SC vs Mbeya City – Saa 1:00 Usiku, Meja Jenerali Isamuhyo

Simba SC, maarufu kama Wekundu wa Msimbazi, wanatarajiwa kushuka dimbani leo saa 1:00 usiku katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo kuwakaribisha Mbeya City, kikosi kinachotambulika pia kama The Purple Nation. Mchezo huu unatabiriwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na historia ya mikikimikiki kati ya timu hizi mbili ndani ya ligi.

Kwa mashabiki wanaotaka kufuatilia mtanange huu kwa ukaribu, mchezo utakuwa mubashara kupitia AzamSports1HD, hatua itakayowezesha mashabiki ndani na nje ya nchi kushuhudia kila tukio uwanjani.

2. Yanga SC vs Fountain Gate – Saa 10:00 Jioni, KMC Complex

Wapinzani wao wa jadi, Yanga SC, nao watashuka dimbani mapema leo majira ya saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa KMC Complex. Wananchi watakuwa wenyeji wa Fountain Gate kutoka Manyara katika mchezo unaotarajiwa kuwa mkali kutokana na kasi ambayo timu zote zimekuwa nayo msimu huu. Mchezo huu nao utarushwa mubashara kupitia AzamSports1HD, hivyo mashabiki wataweza kufuatilia kwa ukamilifu hatua kwa hatua jinsi mchezo utakavyoendelea.

Ratiba ya Mechi za Ligi Kuu NBC Leo 04/12/2025

Ratiba ya Mechi za Ligi Kuu NBC Leo 04/12/2025 inaweka wazi siku yenye ushindani na msisimko kwa mashabiki wa kandanda nchini. Simba na Yanga, baada ya majukumu yao ya kimataifa, wanarejea kwenye ligi wakiwa na lengo moja kuhakikisha wanapata pointi tatu muhimu. Mashabiki wanatarajiwa kushuhudia mechi zenye kiwango cha juu, motisha na ushindani, huku macho yote yakielekezwa kwenye viwanja vya Meja Jenerali Isamuhyo na KMC Complex.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Msimamo Wa Championship Ligi Daraja la Kwanza Tanzania 2025/2026
  2. Msimamo wa Kundi la Azam Kombe la Shirikisho CAF 2025/2026
  3. Simba Yachezea Kichapo cha Pili Mfululizo Makundi Klabu Bingwa
  4. Singida BS Yapata Pointi ya Kwanza Makundi Kombe la Shirikisho CAF
  5. Matokeo ya Stade Malien vs Simba leo 30/11/2025
  6. Kikosi cha Simba vs Stade Malien leo 30/11/2025
  7. Ratiba ya Ligi Kuu ya NBC Leo 30/11/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo