Makundi ya Kombe la Dunia 2026

Makundi ya Kombe la Dunia 2026

Droo ya makundi ya mechi za Kombe la Dunia la 2026 litakaloshirikisha jumla ya timu 48 imefanyika Ijumaa tarehe 5 Desemba 2025 mjini Washington, ambapo sherehe hiyo imeandaliwa katika ukumbi wa mikutano wa John F. Kennedy Center.

Ni hatua muhimu inayoashiria maandalizi ya mwisho ya mashindano makubwa zaidi katika historia ya FIFA, yatakayochezeshwa na wenyeji watatu: Marekani, Canada na Mexico. Mashindano haya ndiyo ya kwanza kufanyika katika muundo mpana wa timu 48, na hivyo kufanya mchakato wa kupanga Makundi ya Kombe la Dunia 2026 kuwa tukio linalofuatiliwa kwa karibu duniani kote.

Makundi ya Kombe la Dunia 2026

Muundo wa Droo ya Makundi ya Kombe la Dunia 2026 na Poti Zake

Katika droo ya mwaka huu, wenyeji watatu wamewekwa kwenye poti ya kwanza kama ilivyo utaratibu wa FIFA.
Vipira vyao vimetambulishwa kwa rangi maalum:

  • Mexico – A1 (kijani)
  • Canada – B1 (nyekundu)
  • Marekani – D1 (bluu)

Timu nyingine zimepangwa kwenye potizo nne kulingana na viwango vya ubora vya FIFA vya Novemba 19. Kwa mujibu wa utaratibu, hakuna kundi litakaloruhusiwa kuwa na zaidi ya timu moja kutoka bara moja, isipokuwa Ulaya kutokana na kuwa na wawakilishi 16. Hivyo, makundi yanaweza kuwa na timu mbili tu kutoka barani humo.

Aidha, mataifa manne yaliyo juu kwenye viwango—Hispania, Argentina, Ufaransa na England—yamepangwa kutotana katika hatua za awali. Lengo ni kuhakikisha uwiano wa ushindani na kuepuka mikutano mikubwa mapema.

Poti Rasmi za Droo ya Makundi ya Kombe la Dunia 2026

Pot 1: Canada, Mexico, USA, Hispania, Argentina, Ufaransa, England, Brazil, Ureno, Uholanzi, Ubelgiji, Ujerumani.

Pot 2: Croatia, Morocco, Colombia, Uruguay, Uswisi, Japan, Senegal, Iran, Korea Kusini, Ecuador, Austria, Australia.

Pot 3: Norway, Panama, Misri, Algeria, Scotland, Paraguay, Tunisia, Côte d’Ivoire, Uzbekistan, Qatar, Saudi Arabia, Afrika Kusini.

Pot 4: Jordan, Cabo Verde, Ghana, Curacao, Haiti, New Zealand pamoja na washindi wanne wa mchujo wa Ulaya na timu mbili za mchujo maalum wa FIFA.

Timu Bingwa na Mataifa Yenye Mashabiki Wengi

Argentina ya Lionel Messi inaingia kama mabingwa watetezi baada ya kutwaa taji la dunia Qatar 2022. Cristiano Ronaldo anatarajiwa kuiongoza Ureno katika kile alichokitaja kuwa Kombe lake la Dunia la mwisho. Mataifa yenye historia kubwa kama Brazil, Ufaransa, Ujerumani, Uingereza, Ubelgiji na Uhispania yanabaki kuwa kati ya wapinzani wanaotarajiwa kutoa ushindani mkali.

Kwa upande mwingine, upanuzi wa mashindano umefungua milango kwa mataifa kadhaa kushiriki kwa mara ya kwanza ikiwa ni pamoja na Cape Verde, Jordan na Curacao, hatua inayotajwa kuongeza msisimko wa Kombe la Dunia la 2026.

Haya Apa Makundi ya Kombe la Dunia 2026

KUNDI C

  1. Mexico
  2. South Africa
  3. Korea Republic
  4. Winner Play-Off D

KUNDI B

  1. Canada
  2. Winner Play-Off A
  3. Qatar
  4. Switzerland

KUNDI C

  1. Brazil
  2. Morocco
  3. Haiti
  4. Scotland

KUNDI D

  1. USA
  2. Paraguay
  3. Australia
  4. Winner Play-Off C

KUNDI E

  1. Germany
  2. Curaçao
  3. Côte d’Ivoire
  4. Ecuador

KUNDI F

  1. Netherlands
  2. Japan
  3. Winner Play-Off B
  4. Tunisia

KUNDI G

  1. Belgium
  2. Egypt
  3. IR Iran
  4. New Zealand

KUNDI H

  1. Spain
  2. Cape Verde
  3. Saudi Arabia
  4. Uruguay

KUNDI I

  1. France
  2. Senegal
  3. Winner Play-Off 2
  4. Norway

KUNDI J

  1. Argentina
  2. Algeria
  3. Austria
  4. Jordan

KUNDI K

  1. Portugal
  2. Winner Play-Off 1
  3. Uzbekistan
  4. Colombia

KUNDI 𝗟

  1. England
  2. Croatia
  3. Ghana
  4. Panama
Makundi ya Kombe la Dunia 2026
Haya ndio Makundi ya Kombe la Dunia 2026

Matukio Maalum na Wageni Mashuhuri Katika Droo

Sherehe ya kupanga Makundi ya Kombe la Dunia 2026 imehudhuriwa na viongozi wakuu wa nchi mwenyeji na wageni mashuhuri.
Marekani imewakilishwa na Rais wake ambaye pia anatarajiwa kuwa mtu wa kwanza kupokea Tuzo Maalum ya Amani ya FIFA. Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney na Rais wa Mexico Claudia Sheinbaum ni miongoni mwa viongozi waliokuwepo kwenye hafla hiyo.

Hafla imepambwa na burudani kutoka kwa wanamuziki wakubwa kama Andrea Bocelli na Robbie Williams.
Usimamizi wa droo umefanywa kwa kushirikisha mastaa wa michezo akiwemo Tom Brady wa NFL, Wayne Gretzky wa NHL, Aaron Judge wa MLB na Shaquille O’Neal wa NBA. Kwa upande wa soka, Rio Ferdinand ameongoza uwasilishaji akisaidiwa na Samantha Johnson, huku Eli Manning akiendesha tukio kwenye zulia jekundu.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2025/2026
  2. Yanga VS Fountain Gate Leo 04/12/2025 Saa Ngapi?
  3. Ratiba ya Mechi za Ligi Kuu NBC Leo 04/12/2025
  4. Simba vs Mbeya City Leo 04/12/2025 Saa Ngapi?
  5. TFF Yatangaza Kikosi cha Awali cha Taifa Stars kwaajili ya Fainali za AFCON 2025 Morocco
  6. Ratiba ya Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup 2025/2026
  7. Msimamo Wa Championship Ligi Daraja la Kwanza Tanzania 2025/2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo