NECTA Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025 | Form Two Results (FTNA)
NECTA Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025, yanayojulikana rasmi kama Form Two National Assessment (FTNA), ni matokeo ya kitaifa yanayosubiriwa na maelfu ya wanafunzi wa shule za sekondari nchini Tanzania pamoja na wazazi, walimu na wadau wa elimu. Matokeo haya hutolewa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) baada ya kukamilika kwa zoezi la upimaji wa kitaifa kwa wanafunzi wa Kidato cha Pili.
Mtihani wa FTNA 2025 ulifanyika rasmi kuanzia tarehe 10 Novemba 2025 hadi 20 Novemba 2025, kwa mujibu wa ratiba rasmi ya mitihani ya Form Two National Assessment (FTNA) iliyotolewa na NECTA.
Mtihani huo ulihusisha masomo ya nadharia na vitendo, pamoja na tathmini za mkondo wa kawaida na wa ufundi (Vocational Stream), ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa kitaifa wa kupima kiwango cha uelewa wa wanafunzi baada ya miaka miwili ya elimu ya sekondari.
Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025 yana nafasi muhimu katika mfumo wa elimu ya Tanzania, kwa kuwa hutumika kutathmini maendeleo ya mwanafunzi kitaaluma, kubaini maeneo ya nguvu na changamoto, na kutoa msingi wa maandalizi ya kitaaluma kuelekea Kidato cha Tatu.
…Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025 yana nafasi muhimu katika mfumo wa elimu ya Tanzania, kwa kuwa hutumika kutathmini maendeleo ya mwanafunzi kitaaluma, kubaini maeneo ya nguvu na changamoto, na kutoa msingi wa maandalizi ya kitaaluma kuelekea Kidato cha Tatu.
Muhtasari wa Haraka: Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025 (FTNA)
Ulisafanyika: 10 Novemba 2025 – 20 Novemba 2025
Uliandaliwa na: Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA)
Hali ya Matokeo: Bado hayajatangazwa rasmi
Yanatarajiwa Kutangazwa: Mwezi Januari 2026 (kwa kuzingatia utaratibu wa miaka ya nyuma)
Njia ya Kuangalia Matokeo: Kupitia tovuti rasmi ya NECTA — www.necta.go.tz
Maneno Muhimu: Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025, NECTA FTNA Results 2025
Kuhusu Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA)
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) ni taasisi ya serikali iliyoanzishwa kisheria chini ya Sheria ya Bunge Na. 21 ya mwaka 1973, ikiwa na jukumu la kusimamia, kuandaa na kuendesha mitihani yote ya kitaifa nchini Tanzania.
Kabla ya mwaka 1973, mitihani ya taifa ilisimamiwa na Curriculum and Examinations Section ya Wizara ya Elimu, baada ya Tanzania Bara kujiondoa katika East African Examinations Council (EAEC) mwaka 1971. Zanzibar ilijiondoa EAEC mapema zaidi mwaka 1970.
Baada ya kuanzishwa kwake, NECTA ilichukua jukumu la moja kwa moja la mitihani ya kitaifa, huku masuala ya mitaala yakiendelea kusimamiwa na Wizara ya Elimu hadi kuanzishwa kwa Institute of Curriculum Development (ICD) mwaka 1975, ambayo baadaye ilibadilishwa jina na kuitwa Tanzania Institute of Education (TIE) mwaka 1993.
Kwa sasa, NECTA ina zaidi ya watumishi 350, na makao makuu yake yapo Kijitonyama, Dar es Salaam, karibu na Mwenge. Taasisi hii ndiyo chanzo rasmi na cha kuaminika cha matokeo yote ya mitihani ya kitaifa ikiwemo FTNA.
Mtihani wa Upimaji wa Kidato Cha Pili (FTNA) ni Nini?
Mtihani wa Upimaji wa Kidato cha Pili, maarufu kama FTNA, ni mtihani wa kitaifa unaofanywa na wanafunzi wa shule zote za sekondari nchini Tanzania. Hufanyika kila mwaka na una nafasi kubwa katika mfumo wa elimu kwa kuwa hutathmini mafanikio ya mwanafunzi katika masomo ya msingi ya sekondari.
Kupitia Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025, wadau wa elimu akiwemo mwanafunzi, mzazi, mlezi na mwalimu huweza kutambua maeneo ya nguvu na changamoto, jambo linalosaidia kupanga mikakati bora ya ufundishaji na ujifunzaji kabla ya kuendelea na hatua inayofuata ya masomo.
Masomo Yanayofanyiwa Mtihani Kidato cha Pili
Mtihani wa Kidato cha Pili unahusisha masomo mbalimbali yanayolenga kukuza ujuzi na maarifa ya wanafunzi. Masomo hayo ni pamoja na:
- Kiswahili
- Basic Mathematics
- English Language
- Biolojia
- Fizikia
- Kemia
- Jiografia
- Historia
- Uraia
- Elimu ya Dini ya Kiislamu
- Bible Knowledge
- Masomo ya Ufundi kama Building Construction, Mechanical Engineering na Electrical Engineering
- Masomo ya Biashara kama Book-Keeping na Commerce
- Lugha za Kigeni kama Kifaransa na Kichina
Mchanganyiko huu wa masomo unaakisi malengo ya elimu ya sekondari katika kukuza maarifa ya kinadharia na ujuzi wa vitendo.
NECTA Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025: Nini cha Kutarajia
Matokeo ya mtihani huu huonesha kiwango cha ufaulu wa jumla pamoja na mgawanyo wa wanafunzi kulingana na jinsia. Takwimu hizi hutoa picha pana ya hali ya elimu kwa mwaka husika na hutumika kama rejea katika maboresho ya sera na mbinu za ufundishaji.
Kwa wanafunzi na wazazi, Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025 ni nyenzo muhimu ya kufanya maamuzi ya kitaaluma, hususan katika kuchagua mkondo wa masomo pindi mwanafunzi anapoanza Kidato cha Tatu.
Je, NECTA Imeshatangaza Matokeo ya Kidato cha Pili 2025?
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza rasmi Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili (FTNA) 2025 Leo 10/01/2026 baada ya kukamilisha taratibu zote za uchakataji, uhakiki na uthibitishaji wa matokeo hayo.
Tangazo hilo limetolewa kupitia taarifa rasmi ya NECTA, ikihusisha pia matokeo ya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne, ambapo ilielezwa kuwa mitihani hiyo ilifanyika kati ya tarehe 10 hadi 19 Novemba 2025 kwa Kidato cha Pili. Baada ya vikao husika, Baraza limeidhinisha kutolewa kwa matokeo hayo kwa matumizi ya umma.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ufaulu wa jumla wa Kidato cha Pili mwaka 2025 umefikia asilimia 86.93, ikiwa ni ongezeko ikilinganishwa na miaka iliyopita. Matokeo hayo yanajumuisha watahiniwa waliopimwa kwa mtaala wa awali pamoja na mtaala ulioboreshwa, ikiwemo kwa mara ya kwanza wanafunzi wa mkondo wa amali. NECTA imeeleza kuwa takwimu zinaonesha mwenendo chanya wa ufaulu kitaifa, licha ya changamoto chache zilizobainika katika baadhi ya masomo ya sayansi asilia.
Wanafunzi, wazazi na walezi wanashauriwa kupata matokeo kupitia tovuti rasmi ya NECTA (www.necta.go.tz) ili kuepuka taarifa zisizo sahihi. Aidha, inasisitizwa kuzingatia maelekezo ya Wizara ya Elimu kuhusu hatua zinazofuata kwa wanafunzi waliofaulu na wale ambao hawakufikia kiwango cha ufaulu.
Fuatilia Hapa Taarifa Kuhuau Matokeo ya Darasa la Nne 2025 (NECTA Standard Four Results)
Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025 Mtandaoni
Baada ya NECTA kutangaza rasmi Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025, wanafunzi, wazazi na walimu wataweza kuyapata matokeo hayo moja kwa moja kupitia tovuti rasmi ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA). Huduma hii hutolewa bila malipo na inapatikana kwa shule zote zilizosajiliwa kufanya Mtihani wa Upimaji wa Kidato cha Pili (FTNA).
Mwongozo wa Video: Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya FTNA 2025
Video ifuatayo inaelezea kwa hatua jinsi ya kuingia kwenye tovuti ya NECTA na kufikia matokeo ya Kidato cha Pili 2025 mara baada ya kutangazwa:
Hatua za Kuangalia Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025 Mtandaoni
1. Tembelea Tovuti Rasmi ya NECTA
Fungua kivinjari cha intaneti na nenda kwenye tovuti ya NECTA kupitia anwani www.necta.go.tz. Hakikisha una muunganisho mzuri wa intaneti ili kuepuka ucheleweshaji wa upakiaji.
2. Bofya Sehemu ya “Results”
Baada ya kufungua tovuti, chagua sehemu ya Results iliyo kwenye menyu kuu. Hapa utaona orodha ya mitihani yote ya kitaifa.
3. Chagua “FTNA”
Katika orodha ya mitihani, tafuta FTNA (Form Two National Assessment) na ubofye ili kufungua ukurasa wa matokeo ya Kidato cha Pili.
4. Chagua Mwaka wa Mtihani
Chagua mwaka 2025 ili kuendelea na matokeo ya mtihani husika.
5. Tafuta Jina la Shule
Baada ya kuchagua mwaka, orodha ya shule zote zilizoshiriki itaonekana. Tafuta jina la shule yako ili kuona matokeo ya wanafunzi wake.
6. Tafuta Jina la Mwanafunzi au Namba ya Mtihani
Ndani ya ukurasa wa shule, utaona majina ya wanafunzi pamoja na matokeo yao. Unaweza kutumia kipengele cha utafutaji (kama Ctrl + F kwenye kompyuta) kutafuta jina la mwanafunzi au namba ya mtihani. Taarifa zitakazoonekana ni pamoja na:
- Jina la mwanafunzi
- Alama za kila somo
- Jumla ya alama
- Daraja la ufaulu (Division)
Angalia Hapa Matokeo ya Kidato cha Pili 2025
Angalia Matokeo ya Kidato cha Pili 2025 kwa Shule Zote (NECTA FTNA)
Umuhimu wa Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025
Matokeo ya Kidato Cha Pili 2025 ni zaidi ya takwimu za ufaulu. Yanatoa msingi wa kupanga mustakabali wa kitaaluma wa mwanafunzi, ikiwemo uchaguzi wa masomo maalum kama Sayansi, Biashara au Sanaa katika Kidato cha Tatu. Aidha, matokeo haya hutumika na walimu kama chombo cha kutathmini ufanisi wa mbinu za ufundishaji na kufanya maboresho pale inapobidi.
Kwa kuzingatia umuhimu wake, ni vyema wanafunzi na wazazi kufuatilia taarifa rasmi na kutumia vyanzo sahihi pekee wakati wa kuangalia matokeo, ili kupata taarifa sahihi na kwa wakati.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Fomu za Kujiunga Vyuo Vya VETA 2026
- Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na Vyuo vya VETA 2026
- When will 2025 Matric Results Released Online?
- Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2025/2026 NECTA
- Ratiba ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2026
- Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato Cha Kwanza 2026
- Form One Selection 2026 | Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Kwanza 2026








Leave a Reply