Kikosi cha Yanga vs Singida Black Star Leo 09/01/2026
Kikosi cha Yanga leo kinatarajiwa kushuka dimbani katika pambano muhimu la nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi 2026 dhidi ya Singida Black Stars, mchezo unaotarajiwa kuchezwa Ijumaa usiku wa saa 2:15 kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Unguja.
Mechi hii inakuja ikiwa na mvuto wa kipekee kutokana na historia ya hivi karibuni ya timu hizo, mabadiliko ya vikosi, pamoja na ushindani mkali unaoendelea kushuhudiwa katika michuano hii ya heshima.
Baada ya jana Alhamisi kushuhudiwa nusu fainali ya kwanza kati ya Azam FC na Simba SC, macho na masikio ya mashabiki wengi sasa yameelekezwa kwenye pambano hili la pili, ambalo litatoa mshindi atakayekutana na mshindi wa mechi ya jana katika fainali itakayochezwa Januari 13, 2026, kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba.
Yanga SC ilijihakikishia nafasi ya kucheza nusu fainali baada ya ushindi mgumu wa bao 1-0 dhidi ya TRA United, matokeo yaliyoonesha uimara wa safu yao ya ulinzi na nidhamu ya kiufundi.
Kwa upande wa Singida Black Stars, walitinga hatua hii baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya URA FC, matokeo yaliyowatosha kuvuka na kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kufuzu nusu fainali katika michuano ya mwaka huu.
Kauli za Makocha Kabla ya Mchezo
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari kabla ya mchezo, Kocha Mkuu wa Yanga, Pedro Goncalves, alieleza imani yake kwa maandalizi ya kikosi chake huku akikiri ugumu wa mpinzani wao.
“Tunaingia katika mchezo huu tukiwa tumejiandaa vizuri. Wachezaji wamefanya kazi kubwa katika mazoezi, tumelenga maandalizi ya kiufundi na kimwili. Tunajua tunakutana na timu nzuri sana,” alisema Goncalves.
Kocha huyo raia wa Ureno aliongeza kuwa licha ya kukosa baadhi ya wachezaji muhimu kutokana na majeraha, bado anaamini kikosi chake kina uwezo wa kufikia lengo.
“Kuna wachezaji muhimu ambao hatutakuwa nao kwa sababu ya majeraha, lakini hii ni fursa kwa wengine kujitokeza. Malengo yetu ya maandalizi tumeyafikia na ninaamini tutashinda na kufuzu fainali,” alisisitiza.
Kwa upande wa Singida Black Stars, Kocha Mkuu David Ouma alibainisha kuwa nidhamu ya kiufundi itakuwa silaha yao kuu dhidi ya timu yenye ushambuliaji hatari.
“Tunajua Yanga ni timu inayoshambulia sana na ni hatari. Mkakati wetu ni kucheza kwa nidhamu, kufuata mpango wa mchezo na kudhibiti nguvu zao. Tukidhibiti mchezo vizuri, tunaamini tunaweza kufuzu fainali,” alisema Ouma.
Kikosi cha Yanga vs Singida Black Star Leo 09/01/2026
Hapa tutakuletea kikosi rasmi cha Yanga kitakachoanza leo dhidi ya Singida Black Stars mara tu kitakapotangazwa na kocha mkuu Pedro Goncalves, kuelekea mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi 2026 unaotarajiwa kuchezwa usiku wa leo kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Unguja.
Kikosi hicho kinatarajiwa kuwa na mabadiliko machache kutokana na majeraha ya baadhi ya wachezaji muhimu, huku nafasi ikifunguka kwa nyota wengine kujitokeza na kuthibitisha uwezo wao katika mchezo huu wa ushindani mkubwa. Yanga inaingia katika pambano hili ikiwa na rekodi nzuri ya ushambuliaji na ulinzi, hali inayoongeza matarajio kwa mashabiki wake kuona kikosi imara kitakachotumika leo.
Hiki Apa Kikosi cha Yanga Kinachoanza Leo
Mapendekezo ya Mhariri:








Leave a Reply