Matokeo ya Form Two 2025/2026 NECTA FTNA

Matokeo ya Form Two 2025/2026 NECTA FTNA

Dar es Salaam. Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza rasmi Matokeo ya Form Two 2025/2026 (NECTA FTNA), yakionesha kuimarika kwa ufaulu wa jumla, ushiriki mkubwa wa watahiniwa, na tofauti za ufaulu kati ya masomo na shule. Matokeo hayo yalitangazwa Januari 10, 2026, na Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Said Mohamed, mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Matokeo ya Form Two 2025/2026 NECTA FTNA

Usajili na Mahudhurio ya Watahiniwa

Kwa Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili mwaka 2025, jumla ya watahiniwa 889,264 walisajiliwa kufanya mtihani huo. Kati yao, wasichana walikuwa 492,856 sawa na asilimia 55, huku wavulana wakiwa 396,408 sawa na asilimia 45.

Mahudhurio yalifikia asilimia 91.3, sawa na watahiniwa 811,575, kutoka shule za sekondari 6,223. Watahiniwa 77,689 sawa na asilimia 8.7 hawakufanya mtihani licha ya kusajiliwa, hali iliyochangiwa zaidi na utoro na changamoto za kiafya.

Ufaulu wa Jumla wa Matokeo ya Form Two 2025/2026

NECTA imeripoti kuwa ufaulu wa jumla kwa watahiniwa wa shule umefikia asilimia 86.93, sawa na wanafunzi 759,091.
Kwa mgawanyo wa kijinsia:

  • Wavulana: 312,492 sawa na asilimia 88.28
  • Wasichana: 392,599 sawa na asilimia 85.89

Ufaulu huu umeongezeka kwa asilimia 1.52 ikilinganishwa na mwaka 2024, na unaonesha mwelekeo wa kuimarika ukilinganishwa na mwaka 2023.

Soma Pia 

  1. Matokeo ya Darasa la Nne 2025/2026 (NECTA SFNA Results)
  2. Matokeo ya Darasa La Nne 2025 Mkoa wa Dodoma
  3. Matokeo ya Darasa La Nne 2025 Mkoa wa Dar Es Salaam
  4. Matokeo ya Kidato cha Nne 2025/2026 (NECTA Form Four Results)

Ufaulu kwa Misingi ya Mitaala

Upimaji wa mwaka 2025 ulifanyika chini ya mitaala miwili:

  • Mtaala ulioboreshwa: Watahiniwa 1,975 sawa na asilimia 89.85 walifaulu
  • Mtaala wa awali: Watahiniwa 731,116 sawa na asilimia 86.93 walifaulu

Takwimu zinaonesha kuwa mtaala ulioboreshwa umeleta matokeo bora zaidi kwa kiwango cha ufaulu.

Ubora wa Ufaulu (Divisions)

Kwa kuzingatia madaraja ya ufaulu:

  • Watahiniwa 240,469 sawa na asilimia 29.64 walipata Divisheni ya Kwanza hadi ya Tatu
  • Divisheni ya Kwanza: Wanafunzi 78,309 sawa na asilimia 9.65

Idadi ya waliopata daraja la kwanza imebaki thabiti ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Ufaulu kwa Ngazi ya Shule

Kati ya shule 6,223 zilizopata matokeo:

  • Shule 6,198 sawa na asilimia 99.6 zilipata wastani wa daraja A hadi D
  • Shule zilizopata daraja A zimeongezeka hadi 177 mwaka 2025
  • Shule zilizopata daraja F zimepungua hadi 25

Hali hii inaashiria kuimarika kwa ubora wa matokeo kwa ngazi ya shule.

Ufaulu kwa Masomo

Masomo ya Lugha

  • Kiswahili: 94.31%
  • English Language: 73.16%

NECTA imeeleza kuwa ufaulu wa somo la English Language unaonesha kuimarika kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo.

Masomo ya Sayansi Jamii

  • History: 56.29%
  • Geography: 57.52%
  • Civics: 35.1% (ongezeko la asilimia 2 kutoka mwaka 2024)

Masomo ya Sayansi Asili

Masomo ya Physics, Chemistry, Biology na Basic Mathematics yameendelea kuwa na ufaulu wa chini ya wastani, kati ya 22.71% hadi 41.84%. Hata hivyo, Basic Mathematics imepanda hadi 22.87% kutoka 18.85% mwaka 2024.

Maana ya “Referred” Kwenye Matokeo ya FTNA

NECTA imefafanua kuwa neno “Referred” linamaanisha mwanafunzi hajafaulu kwa kiwango kinachomruhusu kuendelea na Kidato cha Tatu. Mwanafunzi mwenye matokeo haya anatakiwa kurudia Kidato cha Pili ili kuimarisha uelewa wa masomo yenye changamoto.

Ufafanuzi huu ni muhimu kwa wazazi na walezi katika kupanga hatua sahihi za kitaaluma kwa mwanafunzi.

Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Form Two 2025/2026

Matokeo ya FTNA 2025/2026 yanapatikana kupitia tovuti rasmi ya NECTA. Hatua ni:

  1. Tembelea tovuti ya NECTA https://necta.go.tz
  2. Bofya sehemu ya Results
  3. Chagua FTNA (Form Two National Assessment)
  4. Chagua mwaka 2025
  5. Tafuta jina la shule na namba ya mtihani ya mwanafunzi

Angalia Matokeo ya Form Two 2025/2026 (NECTA FTNA)

Aidha, wanafunzi, wazazi na walezi wanaweza kuangalia Matokeo ya Form Two 2025/2026 moja kwa moja kupitia kiungo kilichopo hapa chini, ambacho kitawapeleka kwenye ukurasa rasmi wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA). Kupitia ukurasa huo, mtumiaji atahitajika kutafuta jina la shule husika ili kuona matokeo kamili ya Kidato cha Pili kwa mwaka wa masomo 2025/2026.

➜ Fungua Ukurasa wa Matokeo ya FTNA 2025

Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo