Ratiba ya Nusu Fainali AFCON 2025
Michuano ya AFCON 2025 imefikia hatua nyeti na yenye mvuto mkubwa, ambapo mataifa manne makubwa ya soka barani Afrika yamefanikiwa kuvuka kizingiti cha robo fainali na sasa yanapambania nafasi ya kucheza fainali ya mashindano haya makubwa.
Baada ya safari ndefu iliyojaa ushindani mkali, timu za Misri, Nigeria, Morocco na Senegal ndizo zimebaki kwenye mbio za mwisho za kuwania taji la Afrika, huku ratiba ya nusu fainali AFCON 2025 ikionesha mabingwa hawa kurudi dimbani siku ya Jumatano, 14 Januari kusaka tiketi za kucheza katika fainali ya michuano hii na mwisho bingwa wa msimu wa 2025 kujulikana.
Ratiba ya Nusu Fainali AFCON 2025 ni kama ifuatavyo:
- Senegal vs Egypt – Jumatano, 14 Januari
- Morocco vs Nigeria – Jumatano, 14 Januari
Michezo hii miwili inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na historia, uzoefu na ubora wa kikosi cha kila timu.
Mapendekezo ya Mhariri:








Leave a Reply