Matokeo ya Azam VS Yanga Leo 13/01/2026 Fainali Mapinduzi Cup
Visiwa vya Zanzibar, hususan Pemba, vinashuhudia mvuto mkubwa wa soka la Tanzania leo Jumanne, Januari 13, 2026, ambapo macho na masikio ya mashabiki yanaelekezwa moja kwa moja katika Uwanja wa Gombani, fainali ya Kombe la Mapinduzi 2026 ikiwakutanisha mahasimu wakubwa wa soka la Tanzania Bara, Azam FC na Young Africans SC (Yanga).
Ni mechi yenye uzito mkubwa kihistoria, kiufundi na kimbinu, huku matokeo ya Azam vs Yanga leo 13/01/2026 fainali Mapinduzi Cup yakisubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa soka ndani na nje ya nchi.
Fainali hii inaingia kwenye vitabu vya historia kama mara ya kwanza kwa Azam na Yanga kukutana katika hatua ya mwisho ya michuano hii tangu Kombe la Mapinduzi lilipoanza kushirikisha rasmi timu za Bara mwaka 2007. Licha ya kila timu kuwa na rekodi ya kucheza na kubeba ubingwa hapo awali, safari hii ina ladha ya kipekee kutokana na mwenendo wa vikosi, mbinu za makocha na ubora wa wachezaji waliopo.
Historia ya Kipekee ya Fainali ya Azam VS Yanga Mapinduzi Cup
Tangu kuanzishwa kwa Kombe la Mapinduzi, fainali kadhaa zimewakutanisha timu kutoka Tanzania Bara. Azam FC imewahi kucheza fainali dhidi ya Simba SC pekee, huku Yanga ikiingia fainali dhidi ya Mtibwa Sugar na Simba. Hata hivyo, fainali ya leo ndiyo ya kwanza kabisa kwa Azam na Yanga kukutana uso kwa uso katika Mapinduzi Cup, jambo linaloifanya mechi hii kuwa ya kihistoria zaidi.
Mechi inatarajiwa kuanza saa 10:00 jioni, huku bingwa mpya wa Kombe la Mapinduzi 2026 akipatikana baada ya dakika 90 au zaidi za ushindani mkali.
Fuatilia Hapa Matokeo ya Azam VS Yanga Leo 13/01/2026
| Azam Fv | 0-0 | Yanga Sc |
| Pen (4-5) |
🏆 #mapinduzicupfinal
🆚 Azam FC
🗓️ 13 January 2026
🏟️ Gombani, Pemba
⏱️ Saa 10:30 Jioni
Mapendekezo ya Mhariri:
Rekodi, Ubingwa na Kisasi
Azam FC inasaka taji lake la sita la Kombe la Mapinduzi, baada ya kubeba miaka ya 2012, 2013, 2017, 2018 na 2019, jambo linaloifanya kuwa klabu iliyotwaa taji hili mara nyingi zaidi. Yanga, kwa upande wake, inatafuta ubingwa wa tatu, baada ya kushinda mwaka 2007 dhidi ya Mtibwa na 2021 dhidi ya Simba.
Hii ni fainali ya nne kwa Yanga (2007, 2011, 2021 na 2026), huku Azam ikiingia fainali ya saba, ikiwa imebeba mataji matano kati ya sita zilizopita, ikikosa moja pekee mwaka 2022 ilipopoteza dhidi ya Simba.
Rekodi zinaonyesha mara ya mwisho Azam na Yanga kukutana kwenye fainali ilikuwa Kombe la FA 2024, lililochezwa Zanzibar, ambapo Yanga ilishinda kwa penalti 6-5 baada ya sare ya 0-0. Fainali ya leo inampa Azam nafasi ya kulipa kisasi hicho.








Leave a Reply