Kikosi cha Yanga Vs Mashujaa Leo 19/01/2026
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya NBC, Yanga SC, leo wanarejea rasmi dimbani kuendelea na harakati za NBC Premier League kwa kuvaana na Mashujaa FC katika mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Mkutano huu wa leo, tarehe 19/01/2026, unatarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wengi wa soka nchini, huku Yanga wakisaka mwanzo mzuri katika mwendelezo wa ligi.
Kwa mujibu wa ratiba, mchezo huu utafanyika leo saa 10:00 jioni katika uwanja wa KMC Complex, ambapo Yanga SC watakuwa nyumbani wakiwakaribisha Mashujaa FC kutoka Kigoma. Uwanja huu unatarajiwa kushuhudia mahudhurio makubwa kutokana na uzito wa mchezo na hamu ya mashabiki kuwaona mabingwa watetezi wakirejea uwanjani.
Hiki Apa Kikosi cha Yanga Vs Mashujaa Leo 19/01/2026
Katika mchezo huu wa leo, Yanga SC wameingia uwanjani wakiwa na kikosi kilichochanganya uzoefu na nguvu mpya. Kikosi cha kuanza (Starting XI) kilichotangazwa kinaonyesha dhamira ya timu kuhakikisha inapata matokeo chanya mbele ya Mashujaa FC.
Starting XI ya Yanga SC:
- 16 Mshery
- 12 Kibwana
- 23 Boka
- 3 Mwamnyeto
- 5 Job
- 25 Damaro
- 7 Maxi
- 38 Abuya
- 29 Dube
- 10 Pacome
- 20 Okello
Wachezaji wa Akiba
Mbali na kikosi cha kwanza, Yanga SC pia wana wachezaji wa akiba ambao wanaweza kuingia na kubadilisha mwelekeo wa mchezo kulingana na hali ya uwanjani. Orodha ya wachezaji wa akiba ni: Masalanga, Hussein, Yao, Assinki, Mzungu, Abdullasir, Mudathir, Conde, Mwanengo na Depu.
Jinsi ya Kutazama Mchezo
Kwa mashabiki ambao hawataweza kufika uwanjani, mchezo huu utarushwa mbashara kupitia AzamSports1HD. Hii inatoa fursa kwa wapenzi wa soka kote nchini kufuatilia kwa karibu Kikosi cha Yanga Vs Mashujaa Leo 19/01/2026 na kuona matokeo ya pambano hili muhimu la ligi.
Mapendekezo ya Mhariri:









Leave a Reply