Matokeo ya Al Ahly Leo 23/01/2026

Matokeo ya Al Ahly Leo 23/01/2026

Wananchi wa Yanga SC leo Ijumaa Januari 23, 2026, wanashuka dimbani katika Uwanja wa Cairo International kuikabili Al Ahly kwenye mchezo wa tatu wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mchezo huu muhimu wa Kundi B unawakutanisha vigogo wawili wenye pointi nne kila mmoja baada ya kila timu kushinda mechi moja na kupata sare moja katika michezo miwili iliyopita.

Kwa mujibu wa ratiba, pambano hili linatarajiwa kuanza saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki na kurushwa mubashara kupitia AzamSports2HD, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kubwa kuona matokeo ya Al Ahly leo na athari zake kwenye msimamo wa kundi.

Matokeo ya Al Ahly Leo 23/01/2026

Mikakati Ya Yanga Kuusaka Ushindi Ugenini

Yanga SC imeweka wazi msimamo wake kuelekea mchezo huu wa ugenini dhidi ya Al Ahly, ikisisitiza kuwa haina mpango wa kujilinda licha ya ukubwa na historia ya mpinzani wake barani Afrika. Lengo kuu kwa mabingwa hao wa Tanzania ni kupata ushindi, na endapo haitafanikiwa, basi sare itakuwa matokeo yanayokubalika lakini si kupoteza.

Akizungumza wakati msafara wa timu unaondoka alfajiri kuelekea Misri, Kocha Mkuu wa Yanga, Pedro Goncalves, alieleza kuwa maandalizi ya kikosi chake yamefikia kiwango cha juu, hasa baada ya usajili uliofanyika kwenye dirisha dogo.

“Tupo tayari kukutana na Al Ahly. Ni timu ngumu na yenye rekodi kubwa Afrika. Tutawafuata tukijua taarifa zao lakini jambo zuri ni kwamba tuna timu imara,” alisema Pedro.

Kauli hiyo inaonesha wazi dhamira ya Yanga kutafuta matokeo chanya leo, hali inayofanya swali la matokeo ya Al Ahly leo 23/01/2026 kuwa gumzo kubwa kwa wadau wa soka Afrika Mashariki na Kaskazini.

Kocha Pedro alibainisha kuwa usajili uliofanywa umeleta uwiano sahihi ndani ya kikosi, ukiunganisha wachezaji wapya na wale waliokuwepo awali. Yanga imefanikiwa kuwasajili kipa Hussein Masalanga, viungo Mohammed Damaro na Allan Okello pamoja na washambuliaji Emmanuel Mwanengo na Laurindo Aurélio ‘Depu’.

Kwa upande mwingine, wachezaji Denis Nkane, Selestin Ecua na Mamadou Doumbia wametolewa kwa mkopo, huku Andy Boyeli aliyekuwa anacheza kwa mkopo akirejeshwa katika klabu yake ya Sekhukhune ya Afrika Kusini.

“Nina furaha na ubora wa wachezaji wangu na tutakwenda kutumia ubora wa kikosi chetu kutafuta matokeo ya aina mbili tu kushinda au kutoa sare,” aliongeza Pedro.

Matokeo ya Al Ahly Leo 23/01/2026

Al Ahly VS Yanga Sc

🏆 #CAFCL
🆚 Al Ahly
🗓️ 23 January 2026
🏟️ Borg El Arab
⏱️ 12:00 Jioni🇪🇬 | 1:00 Usiku🇹🇿

Ushindani wa Ndani Waongeza Nguvu ya Kikosi

Ujio wa wachezaji wapya umeongeza ushindani mkubwa ndani ya kikosi cha Yanga, hali inayowafanya wachezaji kujituma zaidi mazoezini wakipigania nafasi za kucheza. Kwa mujibu wa Pedro, hali hii inampa nafasi ya kufanya maamuzi sahihi kuhusu kikosi cha kuanza na pia kuwapumzisha wachezaji kutokana na ratiba yenye michezo mingi.

“Tuna timu pana ambayo sasa tunaweza kuchagua mifumo bora zaidi lakini kutoa nafasi kwa kila mchezaji kucheza,” alisema.

Ushindani huu wa ndani unatajwa kuwa moja ya silaha muhimu kwa Yanga katika pambano la leo dhidi ya Al Ahly.

Msimamo wa Kundi B Kabla ya Mchezo

Kabla ya mchezo wa leo, Al Ahly na Yanga zote zina pointi nne kila moja, lakini klabu ya Misri inaongoza kundi kwa tofauti ya mabao baada ya kufunga mabao matano na kuruhusu mawili. Yanga kwa upande wake imefunga bao moja na haijaruhusu nyavu zake kutikiswa.

Timu nyingine katika Kundi B ni FAR Rabat ya Morocco na JS Kabylie ya Algeria, ambazo zote zina pointi moja kila moja. Ushindi kwa Yanga leo ungeifanya iongoze kundi kwa kufikisha pointi saba, jambo linalofanya matokeo ya Al Ahly leo 23/01/2026 kuwa na umuhimu mkubwa katika mwelekeo wa kundi hili.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Yanga Yarejea Ligi Kuu Kwa Kishindo Baada ya Kuicharaza Mashujaa 6-0
  2. Cv ya Allan Okello Kiungo Mpya wa Yanga Sc 2025/2026
  3. Matokeo ya Yanga VS Mashujaa Leo 19/01/2026
  4. Kikosi cha Yanga Vs Mashujaa Leo 19/01/2026
  5. Ratiba ya Nusu Fainali AFCON 2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo