NECTA Kutangaza Matokeo ya Kidato cha Nne 2025 Januari 31
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limethibitisha rasmi siku ya kutangaza matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne (CSEE) kwa mwaka 2025. Kwa mujibu wa taarifa rasmi, NECTA Kutangaza Matokeo ya Kidato cha Nne 2025 Januari 31, hatua inayoweka wazi hatima ya maelfu ya wanafunzi waliokamilisha elimu ya sekondari nchini Tanzania.
Mtihani wa Kidato cha Nne 2025 ulifanyika kuanzia tarehe 17 Novemba 2025 hadi 05 Desemba 2025 katika shule zote za sekondari zilizosajiliwa, ukiwahusisha watahiniwa kutoka shule za serikali na binafsi.
Tangazo hili ni muhimu kwa wanafunzi, wazazi, walimu na wadau wa elimu kwa ujumla, kwani matokeo ya CSEE hutumika kama msingi wa maamuzi ya kitaaluma, ikiwemo kujiunga na elimu ya juu ya sekondari au taasisi za mafunzo ya ufundi na kati.
Taarifa Rasmi ya Kutangazwa kwa Matokeo
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na NECTA, kutangazwa kwa matokeo ya Kidato cha Nne 2025 kutafanyika kupitia mkutano maalum na waandishi wa habari utakaofanyika tarehe 31 Januari 2026 saa 5:00 asubuhi, katika Ofisi za Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dar es Salaam. Taarifa hiyo itaongozwa na Katibu Mtendaji wa NECTA, na itarushwa moja kwa moja kupitia YouTube ya NECTA Online ili kuwezesha wananchi wengi kufuatilia kwa wakati mmoja.
Tangazo hili linaweka ukomo wa sintofahamu iliyokuwepo miongoni mwa wanafunzi na wazazi kuhusu lini matokeo yangetolewa, hasa ikizingatiwa kuwa kwa miaka ya nyuma matokeo ya CSEE yamekuwa yakitangazwa mwezi Januari.
Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Kidato cha Nne 2025
Baada ya kutangazwa rasmi, wanafunzi wataweza kupata matokeo yao kupitia tovuti rasmi ya NECTA kwa kufuata hatua zifuatazo:
- Tembelea tovuti rasmi ya NECTA
Fungua kivinjari cha intaneti na andika anwani: www.necta.go.tz - Fungua sehemu ya “Results” au “Matokeo”
Sehemu hii hupatikana kwenye menyu kuu ya tovuti. - Chagua mtihani wa CSEE
Huu ndio mtihani wa Kidato cha Nne. - Chagua mwaka husika (2025)
Bonyeza kiunganishi (link) cha matokeo ya Kidato cha Nne 2025. - Tafuta matokeo kwa shule au namba ya mtihani
Watahiniwa wanaweza kuona matokeo kwa kutafuta jina la shule au kutumia Index Number yao. - Pakua au chapisha matokeo
Matokeo yanaweza kuhifadhiwa kwa matumizi ya baadaye au kuchapishwa.
Mapendekezo ya Mhariri:







Leave a Reply