Benfica vs Real Madrid Yasimama Kwa Dakika 10 Kufuatia Tuhuma za Ubaguzi wa Rangi kwa Vinicius Jr
Mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Real Madrid na Benfica ilisimamishwa kwa dakika 10 baada ya mshambuliaji Vinícius Júnior kudai kufanyiwa kitendo cha ubaguzi wa rangi, tukio lililozua mjadala mkubwa katika soka la Ulaya.
Katika mchezo huo wa mtoano wa play-off, Vinícius aliiandikia Real Madrid bao la kuongoza kabla ya kushangilia mbele ya mashabiki wa wenyeji. Muda mfupi baadaye, alikumbana na mzozo na winga wa Benfica, Gianluca Prestianni, hali iliyosababisha malalamiko rasmi kwa mwamuzi.
Tukio Lililosababisha Mechi Kusimamishwa
Baada ya kufunga bao, Vinícius alionekana kushangilia karibu na mashabiki wa Benfica, jambo lililomfanya apewe kadi ya njano. Hata hivyo, mvutano uliongezeka pale Prestianni alipomkabili na kuonekana kuvuta jezi yake juu ya mdomo wake kabla ya kusema jambo kwa mshambuliaji huyo wa Real Madrid.
Vinícius alikimbilia kwa mwamuzi Francois Letexier kueleza malalamiko yake. Mara moja, mwamuzi huyo alisimamisha mchezo na kuanzisha itifaki ya kupambana na ubaguzi wa rangi kwa kuvuka mikono yake mbele ya kifua – ishara rasmi ya kuamsha utaratibu wa FIFA dhidi ya ubaguzi.
Mchezo ulisimama kwa takribani dakika 10 huku mazungumzo yakifanyika kati ya wachezaji, makocha na waamuzi kabla ya kuendelea tena.
Soma Pia:
- Simba Yafuzu 32 Bora CRDB Federation Cup Baada ya Kuifunga Greenland 3-0
- Droo ya Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika 2025/2026
- Droo ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho Afrika 2025/2026
Kauli ya Vinícius Jr Baada ya Mchezo
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Vinícius aliandika kwa Kireno:
“Racists are, above all, cowards. They need to put their shirts over their mouths to demonstrate how weak they are.”
Aliongeza kuwa si mara ya kwanza kukumbana na hali kama hiyo katika maisha yake na ya familia yake, akisema:
“Nothing that happened here today was new in my life and my family’s.”
Aidha, alieleza kutofurahishwa na jinsi itifaki ilivyotekelezwa, akisema ilikuwa “poorly executed” na haikutoa matokeo aliyotarajia.
Msimamo wa Prestianni na Benfica
Kwa upande wake, Prestianni alikanusha vikali tuhuma hizo kupitia taarifa ya Instagram iliyoshirikiwa na Benfica, akisema:
“I want to clarify that at no time did I direct racist insults to Vini Jr, who regrettably misunderstood what he thought he heard.”
Alisisitiza kuwa hajawahi kuwa mbaguzi na alisikitika kwa vitisho alivyodai kupokea kutoka kwa wachezaji wa Real Madrid.
Benfica pia ilichapisha video ya tukio hilo ikisema kuwa kwa umbali uliokuwepo, wachezaji wa Real Madrid wasingeweza kusikia kile wanachodai kusikia.
Mbappé Afunguka Kuhusu Tukio
Mshambuliaji wa Real Madrid, Kylian Mbappe, alisema baada ya mechi kuwa alisikia maneno ya kibaguzi yakielekezwa kwa mwenzake.
“He put his shirt here [over his mouth] to say Vinicius is a ****** five times. I heard it,” alisema Mbappé, akiongeza kuwa tukio hilo halipaswi kuvumiliwa katika mashindano makubwa kama Ligi ya Mabingwa.
Alisisitiza kuwa mashindano hayo yanapaswa kuwa mfano bora kwa vijana na kwamba maadili ya soka hayapaswi kudhoofishwa kwa matukio ya aina hiyo.
Kauli za Makipa na Viongozi wa Soka
Kocha wa Benfica, Jose Mourinho, alionekana akizungumza na Vinícius wakati wa tukio hilo. Baadaye, alisema alijaribu kuwa “independent” katika tathmini yake na kudai kuwa klabu yake si ya kibaguzi, akimrejea Eusébio kama mchezaji mkubwa mweusi katika historia ya Benfica.
Hata hivyo, kauli zake zilipingwa vikali na wachambuzi akiwemo Clarence Seedorf, aliyesema kuwa kuhalalisha au kuhusisha sherehe ya bao na ubaguzi ni kosa kubwa.
Shirika la kupinga ubaguzi, Kick It Out, lilimshutumu Mourinho kwa kile lilichokiita “gaslighting”, likisema kuwa kipaumbele kinapaswa kuwa kumsikiliza anayelalamika na kuhakikisha anahisi kuungwa mkono.
Uchunguzi wa UEFA na Historia ya Matukio ya Awali
Mamlaka za UEFA zimemteua mkaguzi wa maadili na nidhamu kuchunguza madai ya tabia ya kibaguzi katika mchezo huo.
Tukio hili linaongeza kwenye orodha ya matukio ambayo Vinícius amewahi kuyakabili. Mwaka 2024, mashabiki watatu wa Valencia walihukumiwa kifungo cha miezi minane jela kwa kumfanyia vitendo vya kibaguzi katika mechi ya LaLiga hukumu ya kwanza ya aina hiyo nchini Hispania. Aidha, mashabiki wengine waliwahi kuhukumiwa kwa kosa la kuning’iniza sanamu yenye jina lake darajani Madrid, huku wengine wakipigwa faini na kupigwa marufuku kuingia viwanjani.
Matokeo ya Mchezo
Baada ya mechi kuendelea, Real Madrid ilishikilia ushindi wa 1-0. Hata hivyo, kulikuwa na kucheleweshwa tena mwishoni mwa muda wa nyongeza baada ya baadhi ya mashabiki kurusha vitu uwanjani wakati Vinícius akijiandaa kupiga kona.
Tukio hili limezua mjadala mpana kuhusu utekelezaji wa itifaki za kupambana na ubaguzi wa rangi katika soka la Ulaya, huku macho yote yakielekezwa kwenye uchunguzi unaoendelea.
Mapenedkezo ya Mhariri:








Leave a Reply