Dodoma Jiji vs Simba SC Leo 25/02/2026 Saa Ngapi?
Ligi Kuu ya NBC 2025/2026 inaendelea kupamba moto leo Jumatano, 25/02/2026 huku ushindani ukiwa mkubwa katika kila kona ya msimamo. Miongoni mwa michezo inayosubiriwa kwa hamu ni Dodoma Jiji vs Simba SC, pambano litakalopigwa katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, ambapo timu zote zinashuka dimbani zikitafuta pointi tatu muhimu.
Dodoma Jiji vs Simba SC Leo Saa Ngapi?
Kwa mujibu wa ratiba, mchezo kati ya Dodoma Jiji vs Simba SC utaanza saa 1:00 usiku katika Dimba la Jamhuri jijini Dodoma.
Huu ni mchezo wa Ligi Kuu ya NBC unaotarajiwa kuwa wenye ushindani ya aina yake na mvuto wa kipekee unaotarajiwa kufuatiliwa na mashabiki wengi kutokana na historia ya timu hizi mbili zinapokutana.
Rekodi ya Mikutano: Simba Atamba, Dodoma Jiji Wapambana
Takwimu zinaonyesha kuwa katika michezo 10 ya Ligi Kuu iliyowakutanisha Dodoma Jiji na Simba, Simba imeibuka na ushindi katika michezo yote 10. Katika kipindi hicho:
- Simba imefunga mabao 18
- Dodoma Jiji imefunga mabao mawili pekee
Rekodi inaipa Simba hadhi ya kuwa na historia bora kwenye mechi hizi, lakini Dodoma Jiji wanaamini kuwa kila mchezo una hadithi yake.
Kauli ya Kocha wa Dodoma Jiji: “Hatuogopi”
Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji, Amani Josiah, amesema maandalizi ya timu yake yamekuwa mazuri katika nyanja zote muhimu.
Amesema maandalizi ya kimbinu, kiufundi na kisaikolojia yamefanyika kwa umakini, huku akisisitiza kuwa wanaiangalia mechi hiyo kama fursa ya kihistoria badala ya kuingiwa na hofu.
Kwa mujibu wa Josiah, timu ya msimu huu ni tofauti na ile ya msimu uliopita, na wanaingia uwanjani wakiwa na dhamira ya kubadili taswira ya matokeo yaliyopita. Amesisitiza kuwa wamepitia mazingira magumu zaidi ya changamoto ya kukutana na Simba, hivyo hawana sababu ya kuihofia mechi hiyo.
Kauli yake inaashiria kuwa Dodoma Jiji inalenga kuandika ukurasa mpya licha ya rekodi iliyopo.
Simba Watoa Heshima, Lakini Wanalenga Ushindi
Upande wa Simba, Kocha Mkuu Steve Barker amesema kikosi chake kimejiandaa vizuri kwa wiki yenye michezo kadhaa ya ugenini.
Barker ameweka wazi kuwa licha ya kuanza kuonyesha muendelezo mzuri wa ushindi, hawapaswi kuonyesha dalili za kuridhika. Amesisitiza kuwa wanaiheshimu Dodoma Jiji na wanatarajia mchezo mgumu.
Ameongeza kuwa kila mpinzani ana changamoto zake na kwamba Dodoma Jiji wanatoka kupata ushindi katika mechi zilizopita, jambo linalohitaji umakini wa hali ya juu kutoka kwa wachezaji wake.
Kwa mujibu wa Barker, mechi iliyo mbele yao ndiyo muhimu zaidi, hivyo atalazimika kupanga kikosi imara kwa ajili ya kuhakikisha wanapata matokeo chanya.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Ratiba ya Mechi za Leo 25/02/2026 Ligi Kuu ya NBC
- Ratiba ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la CRDB FA CUP 2025/26
- Kocha Steve Barker Aeleza Mkakati wa Simba Katika Mechi Tatu Zijazo
- Kocha Yusuf Chipo Alia na Mabeki Baada ya Mtibwa Kufungwa 3-1 na Singida BS
- Droo ya Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la CRDB Kufanyika Februari 24
- Mgombea Urais Barcelona Victor Font Aahidi Kumrejesha Messi Camp Nou









Leave a Reply