Ratiba ya Ligi Kuu ya NBC Leo 18/03/2026
Mbio za kumsaka bingwa wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania msimu wa 2025/2026 zinaendelea kupamba moto leo, huku timu mbalimbali zikiingia uwanjani kuwania alama muhimu katika hatua hii ya ushindani mkali. Mashabiki wa soka wanatarajia kushuhudia michezo miwili yenye ushindani, kila timu ikisaka matokeo chanya ili kujiimarisha kwenye msimamo wa ligi.
Michezo ya Ligi Kuu NBC Leo (18 Machi 2026)
Ratiba ya leo inahusisha michezo miwili muhimu itakayochezwa katika viwanja tofauti hapa nchini:
TRA United vs Yanga SC
- Saa 10:00 jioni
- Uwanja: Sheikh Amri Abeid, Arusha
Katika mchezo huu, TRA United watakuwa nyumbani wakijaribu kutumia faida ya uwanja wao kuwazuia Yanga SC, ambao ni miongoni mwa timu zenye ushindani mkubwa kwenye ligi msimu huu.
Tanzania Prisons vs Singida Black Stars
- Saa 2:00 usiku
- Uwanja: Jamhuri, Dodoma
Maafande wa Tanzania Prisons watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Singida Black Stars, maarufu kama “Wakulima wa Alizeti”, katika pambano linalotarajiwa kuwa na ushindani mkali.
Wapi Kuangalia Michezo Hii
Kwa mashabiki watakaoshindwa kufika viwanjani, michezo yote ya leo itaonyeshwa mubashara kupitia kituo cha televisheni cha AzamSports1HD, kinachorushwa katika jukwaa la Azam TV.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Yanga Yathibitisha Majeraha ya Depu, Bacca na Wachezaji Wawili Zaidi
- Malindi Katika Hatari ya Kushuka Daraja Ligi Kuu Zanzibar Baada ya Matokeo Mabaya
- Kiungo Mghana Enock Aingia Kwenye Radar ya Singida BS
- Yanga Yashindwa Kulenga Lango Dhidi ya Azam FC Licha ya Uwepo wa Depu na Dube
- Bilioni 388.8 Kujenga AFCON City Unguja
- Tanzania Yatoa Zaidi ya Sh80 Bilioni CAF Ili Kuwa Mwenyeji wa AFCON 2027








Leave a Reply