Yanga Vs TRA United Leo 18/03/2026 Saa Ngapi?
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC, leo wanashuka dimbani kuendelea na kampeni ya kutetea ubingwa wao, wakikabiliana na wenyeji TRA United katika mchezo muhimu wa kufunga mzunguko wa kwanza.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na malengo ya kila timu, huku Yanga wakisaka kuendelea kubaki kileleni na TRA United wakihitaji kupanda nafasi kwenye msimamo.
Yanga Vs TRA United Leo 18/03/2026
Mchezo kati ya Yanga SC dhidi ya TRA United utachezwa leo Jumatano, tarehe 18 Machi 2026, katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.
- Muda wa kuanza: Saa 10:00 jioni
- Uwanja: Sheikh Amri Abeid, Arusha
- Matangazo: AzamSports1HD (moja kwa moja)
Huu ni miongoni mwa michezo muhimu ya NBC Premier League inayovuta hisia za mashabiki wengi kutokana na ushindani wa timu hizi mbili.
Yanga SC wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa na pointi 36, wakilenga kufikisha pointi 39 iwapo watapata ushindi leo. Hata hivyo, kikosi hicho kinakabiliwa na changamoto ya majeruhi wa baadhi ya wachezaji muhimu.
Wachezaji watakaoukosa mchezo huu ni pamoja na:
- Clement Mzize
- Dickson Job
- Ibrahim Abdullah ‘Bacca’ (jeraha la nyonga)
- Laurindo Dilson ‘Depu’ (majeraha ya paja)
- Chadrack Boka (jeraha la enka)
- Edmund John (jeraha la bega)
Licha ya hali hiyo, Yanga bado wanaendelea kuonyesha ubora wao msimu huu na wanabaki kuwa timu yenye ushindani mkubwa.
Kwa upande wa TRA United, timu hiyo inalenga kupata ushindi ili kufikisha pointi 22, hatua itakayowasaidia kupanda kutoka nafasi ya kumi hadi ya sita kwenye msimamo wa ligi.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Yanga Yathibitisha Majeraha ya Depu, Bacca na Wachezaji Wawili Zaidi
- Malindi Katika Hatari ya Kushuka Daraja Ligi Kuu Zanzibar Baada ya Matokeo Mabaya
- Kiungo Mghana Enock Aingia Kwenye Radar ya Singida BS
- Yanga Yashindwa Kulenga Lango Dhidi ya Azam FC Licha ya Uwepo wa Depu na Dube
- Bilioni 388.8 Kujenga AFCON City Unguja
- Tanzania Yatoa Zaidi ya Sh80 Bilioni CAF Ili Kuwa Mwenyeji wa AFCON 2027








Leave a Reply