Kikosi cha Yanga Vs TRA United Leo 18/03/2026
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Young Africans SC (Yanga), leo Jumatano Machi 18, 2026 wanarejea dimbani kuendeleza kampeni ya kutetea ubingwa wao, wakikabiliana na TRA United katika mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza. Pambano hilo linatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuanzia saa 10:00 jioni.
Mchezo huo ni sehemu ya ratiba ya ligi ambapo pia Tanzania Prisons watakuwa wenyeji wa Singida Black Stars katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, kuanzia saa 2:00 usiku, huku michezo yote ikirushwa mubashara kupitia AzamSports1HD.
Yanga yatinga ugenini ikiwa na majeruhi sita
Yanga inaingia katika mchezo huu ikiwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara na pointi 36, lakini ikikabiliwa na changamoto ya wachezaji majeruhi. Kikosi hicho kitawakosa Clement Mzize na Dickson Job, huku wengine wanne waliopo nje ya uwanja wakiwa ni Ibrahim Abdullah ‘Bacca’ (jeraha la nyonga), Laurindo Dilson ‘Depu’ (nyama za paja), Chadrack Boka (enka ya mguu wa kushoto) na Edmund John (bega).
Pamoja na hali hiyo, ushindi wa leo utaifanya Yanga kufikisha pointi 39 na kumaliza mzunguko wa kwanza ikiwa kinara wa msimamo wa ligi.
Hiki Apa Kikosi cha Yanga Vs TRA United Leo 18/03/2026
Historia ya mechi za Yanga dhidi ya TRA United
Takwimu zinaonyesha kuwa timu hizi zimekutana mara tano tangu TRA United ilipoanza kutumia jina hilo, zikiwemo mechi nne za Ligi Kuu Bara na moja ya Kombe la FA. Yanga imeshinda mechi tatu, huku TRA United ikishinda moja.
Katika jumla ya mechi hizo, mabao 14 yamefungwa, ambapo Yanga imefunga mabao 11 na TRA United mabao matatu. Aidha, Yanga ina rekodi ya kucheza mechi nne bila kuruhusu bao dhidi ya wapinzani hao.
Mara ya mwisho kukutana ilikuwa Novemba 7, 2024, ambapo TRA United iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Yanga, matokeo yanayoongeza uzito wa mchezo wa leo.
Malengo ya kila timu
TRA United, ambayo ipo nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi, inaingia katika mchezo huu ikiwa na lengo la kufikisha pointi 22 na kupanda hadi nafasi ya sita. Kwa upande wa Yanga, ushindi ni muhimu ili kuendelea kubaki kileleni na kumaliza vyema mzunguko wa kwanza.
Kauli za makocha kabla ya mchezo
Kocha wa TRA United, Ettiene Ndayiragije, alisema timu yake imejiandaa vizuri kwa mchezo huo:
“Tumerejea mazoezini baada ya kukosa mechi dhidi ya Simba na tumebadilisha mipango kwa ajili ya Yanga. Wachezaji wote wapo tayari na tunaamini tutapambana kupata pointi tatu.”
Kwa upande wake, kocha wa Yanga, Pedro Goncalves, alikiri kuwa mchezo huo utakuwa na ushindani mkubwa:
“Itakuwa mechi ngumu dhidi ya timu nzuri. Tumetoka kwenye mchezo mgumu dhidi ya Azam na sasa tunakutana na TRA ambao wamekuwa na muda mrefu wa kujiandaa. Hii itaongeza ushindani, lakini tunaamini katika ubora wa timu yetu licha ya majeruhi.”
Mapendekezo ya Mhariri:
- Yanga Yathibitisha Majeraha ya Depu, Bacca na Wachezaji Wawili Zaidi
- Malindi Katika Hatari ya Kushuka Daraja Ligi Kuu Zanzibar Baada ya Matokeo Mabaya
- Kiungo Mghana Enock Aingia Kwenye Radar ya Singida BS
- Yanga Yashindwa Kulenga Lango Dhidi ya Azam FC Licha ya Uwepo wa Depu na Dube
- Bilioni 388.8 Kujenga AFCON City Unguja
- Tanzania Yatoa Zaidi ya Sh80 Bilioni CAF Ili Kuwa Mwenyeji wa AFCON 2027









Leave a Reply