Matokeo ya TRA United Vs Yanga Leo 18/03/2026

Matokeo ya TRA United Vs Yanga Leo 18/03/2026

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC, leo Machi 18, 2026 wanashuka dimbani kuendeleza harakati za kutetea ubingwa wao, huku wakikabiliwa na kibarua kizito dhidi ya TRA United katika mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Kikosi hicho kinachoongoza msimamo wa ligi kinahitaji matokeo chanya ili kuimarisha nafasi yake kileleni, licha ya kukumbwa na changamoto ya majeruhi kwa baadhi ya nyota wake muhimu. Mchezo huu wa kukatana shoka unatarajiwa kukimua vumbi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha, kuanzia saa 10:00 jioni, ukiwa ni sehemu ya michezo ya NBC Premier League inayopigwa leo Jumatano. Mashabiki watapata fursa ya kufuatilia pambano hili moja kwa moja kupitia Azam Sports 1 HD.

Matokeo ya TRA United Vs Yanga Leo 18/03/2026

Yanga SC

Yanga inaingia katika mchezo huu ikiwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 36. Ushindi katika mechi hii utaiwezesha kufikisha pointi 39 na kumaliza mzunguko wa kwanza ikiwa juu zaidi.

Hata hivyo, kikosi hicho kinakabiliwa na changamoto ya majeruhi kwa wachezaji kadhaa muhimu. Miongoni mwa wachezaji watakaokosekana ni pamoja na:

  • Clement Mzize
  • Dickson Job
  • Ibrahim Abdullah ‘Bacca’ (jeraha la nyonga)
  • Laurindo Dilson ‘Depu’ (misuli ya paja)
  • Chadrack Boka (enka ya mguu wa kushoto)
  • Edmund John (jeraha la bega)

Kocha wa Yanga, Pedro Goncalves, alielezea ugumu wa mchezo huo akisema:

“Tutakuwa na mechi ngumu sana. Tunakutana na timu ambayo imejiandaa vizuri na inashambulia. Pia tuna changamoto ya majeruhi ndani ya kikosi chetu.”

Aliongeza kuwa licha ya changamoto hizo, timu yake inaendelea kujiamini kutokana na kiwango kizuri walicho nacho ligi.

TRA United

Kwa upande wa TRA United, timu hiyo inaingia katika mchezo huu ikiwa na lengo la kujiimarisha katika msimamo wa ligi. Kwa sasa ipo nafasi ya 10, lakini ushindi katika mchezo huu utaifanya kufikisha pointi 22 na kupanda hadi nafasi ya sita.

Kocha wa TRA United, Ettiene Ndayiragije, alizungumzia maandalizi ya timu yake akisema:

“Tumekuwa na muda mzuri wa kujiandaa, tumebadilisha mipango na wachezaji wote wapo tayari. Tunaamini tutapambana kupata pointi tatu.”

Matokeo ya TRA United Vs Yanga Leo 18/03/2026

TRA United 0-0 FULL TIME Yanga Sc

Rekodi ya Mikutano ya Hivi Karibuni

Historia inaonyesha kuwa Yanga ina ubora mkubwa katika michezo dhidi ya TRA United. Katika jumla ya mikutano mitano:

  • Yanga imeshinda mara 3
  • TRA United imeshinda mara 1
  • Mechi zote zimekuwa na angalau bao moja

Kwa ujumla:

  • Yanga imefunga mabao 11
  • TRA United imefunga mabao 3

Hata hivyo, kumbukumbu ya msimu uliopita bado iko hai, ambapo TRA United iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Yanga katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Novemba 7, 2024.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kikosi cha Yanga Vs TRA United Leo 18/03/2026
  2. Yanga Vs TRA United Leo 18/03/2026 Saa Ngapi?
  3. Ratiba ya Ligi Kuu ya NBC Leo 18/03/2026
  4. Hakim Ziyech Apunguza 75% ya Mshahara Ili Kujiunga na Wydad AC
  5. Depu wa Yanga Abeba Tuzo ya Mchezaji Bora wa Februari Ligi Kuu Ya NBC
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo