Kikosi cha Tanzania Taifa Stars vs Liechtenstein Leo 26 Machi 2026
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, leo tarehe 26 Machi 2026 inashuka dimbani kuanza safari yake katika mashindano ya FIFA Series kwa mchezo muhimu dhidi ya Liechtenstein national football team. Mchezo huu utakaopigwa majira ya saa 11:30 jioni unatarajiwa kuwa kipimo muhimu kwa kikosi cha Tanzania katika kujenga ushindani wa kimataifa na kuimarisha viwango vya wachezaji wake.
Maandalizi ya Taifa Stars kuelekea mchezo wa leo
Taifa Stars imeingia katika mchezo huu ikiwa imefanya maandalizi ya kina yaliyoanza hapa Dar es Salaam kabla ya kusafiri kuelekea Kigali kwa ajili ya michuano hiyo. Kikosi hicho kilianza kambi rasmi Machi 22 na baadaye kuondoka kuelekea Rwanda kushiriki mashindano ya FIFA Series 2026.
Kocha mkuu wa timu hiyo, Miguel Gamondi, alieleza kuwa maandalizi yamefanyika kwa umakini mkubwa yakilenga kujenga msingi imara wa timu.
“Tumeanza maandalizi kwa umakini mkubwa, tukijenga msingi imara wa timu,” alisema Gamondi.
Aliongeza kuwa maandalizi hayo yanajumuisha mbinu za kiufundi, nidhamu ya wachezaji pamoja na kuimarisha mshikamano wa kikosi – mambo ambayo ni muhimu katika mashindano ya kimataifa.
Kikosi cha Taifa Stars vs Liechtenstein Leo 26 Machi 2026
Kikosi rasmi cha kwanza cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, kitakachoanza katika mchezo wa leo dhidi ya Liechtenstein kinatarajiwa kutangazwa rasmi saa moja kabla ya mchezo kuanza. Hata hivyo, kutokana na orodha ya wachezaji walioitwa kambini na kocha mkuu Miguel Gamondi, tayari kuna mwanga wa kikosi kilichoandaliwa kwa ajili ya pambano hilo la FIFA Series 2026.
Gamondi amechagua kikosi chenye mchanganyiko wa wachezaji wa ligi ya ndani pamoja na wale wanaocheza soka la kimataifa, hatua inayolenga kuongeza ushindani na ubora wa timu. Orodha hii ya wachezaji waliopo kambini ndiyo msingi wa maandalizi ya Taifa Stars kuelekea mchezo wa leo, huku majina ya wachezaji 11 wa kwanza yakisubiriwa kwa hamu kubwa kabla ya kipenga cha kuanza kupulizwa.
Orodha ya Wachezaji Walioitwa Kikosi cha Taifa Stars:
- Aishi Manula (Azam FC)
- Yona Amos (Pamba Jiji)
- Zuberi Foba (Azam FC)
- Mohamed Mussa (Mashujaa FC)
- Twalib Nuru (Azam FC)
- Bakari Msimu (Coastal Union)
- Elias Lameck (Azam FC)
- Haji Mnoga (Salford City, Uingereza)
- Nickson Kibabage (Simba SC)
- Bakari Mwamnyeto (Young Africans)
- Mohamed Hussein (Young Africans)
- Ibrahim Abdulla (Young Africans)
- Yusuph Kagoma (Simba SC)
- Kelvin Nashon (Pamba Jiji)
- Mudathir Yahya (Young Africans)
- Novatus Dismas (Göztepe FC, Uturuki)
- Alphonce Mabula (Shamakhi, Azerbaijan)
- Feisal Salum (Azam FC)
- Saimon Msuva (Al-Talaba, Iraq)
- Kelvin John (Aalborg BK, Denmark)
- Idd Suleiman (Azam FC)
- Charles M’mombwa (Floriana FC, Malta)
- Tarryn Allarakhia (Rochdale AFC, Uingereza)
- Paul Peter (JKT Tanzania)
- Suleiman Mwalimu (Simba SC)
Kwa msingi wa kikosi hiki, benchi la ufundi lina nafasi ya kuchagua kikosi bora kitakachoweza kuhimili ushindani wa mchezo dhidi ya Liechtenstein, huku mashabiki wakisubiri kuona nani ataanza katika kikosi cha kwanza.
Pigo kwa Taifa Stars: Msuva Kukosekana
Katika kuelekea mchezo huu, Taifa Stars imepata pigo baada ya mshambuliaji nyota Simon Msuva kukosekana kikosini kutokana na changamoto za usafiri zinazohusishwa na mgogoro wa kimataifa.
Kutokana na hali hiyo, benchi la ufundi lililazimika kufanya mabadiliko ya haraka kwa kumjumuisha Morice Abraham kuziba nafasi hiyo.
Licha ya changamoto hiyo, wachezaji wanaocheza nje ya nchi akiwemo Kelvin John, Haji Mnoga na Tarryn Allarakhia wanatarajiwa kuungana na timu jijini Kigali kuongeza nguvu katika kikosi hicho.
Umuhimu wa mchezo wa Tanzania vs Liechtenstein
Mchezo huu wa Kikosi cha Tanzania Taifa Stars vs Liechtenstein Leo 26 Machi 2026 una umuhimu mkubwa kwa pande zote mbili, hasa kwa Tanzania inayotafuta kupima uwezo wake dhidi ya timu kutoka bara la Ulaya.
Mbali na ushindani wa kawaida, mechi hii pia ni sehemu ya mchakato wa:
- Kupima mbinu mpya za kocha
- Kutathmini kina cha kikosi
- Kuangalia uwezo wa wachezaji kuhimili mazingira tofauti ya mchezo
Ikiwa Taifa Stars itaibuka na ushindi, itatinga fainali ya Machi 29 ambapo itacheza dhidi ya mshindi kati ya Aruba au Macau. Endapo itapoteza, itacheza mechi ya mshindi wa tatu dhidi ya timu itakayopoteza mechi hiyo nyingine.
Gamondi azungumzia ushindani na malengo ya timu
Kocha Gamondi alikiri kuwa mchakato wa kuchagua kikosi ulikuwa na changamoto kubwa, lakini alisisitiza kuwa kila mchezaji aliyechaguliwa ana uwezo wa kuitumikia timu kwa kiwango cha juu.
“Tumelazimika kufanya maamuzi magumu mara kwa mara ili kupata kikosi sahihi kitakachoiwakilisha nchi.”
Aliongeza kuwa ushindani ndani ya kikosi ni jambo chanya kwani unawasukuma wachezaji kujituma zaidi ili kupata nafasi ya kucheza.
Mapendekezo ya Mhariri:









Leave a Reply