Matokeo ya Simba SC vs Coastal Union leo 02/04/2026

Matokeo ya Simba SC vs Coastal Union leo 02/04/2026

Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, leo wanashuka dimbani kuwakabili Coastal Union katika mwendelezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kuona matokeo ya Simba SC vs Coastal Union leo 02/04/2026 baada ya mapumziko ya kalenda ya FIFA.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo majira ya saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Kikosi cha Simba SC leo dhidi ya Coastal Union

Simba SC wameweka wazi kikosi chao cha kwanza (Starting XI) kitakachoanza mchezo huu muhimu. Kikosi hicho kinaonyesha mchanganyiko wa uzoefu na nguvu mpya katika safu zote.

Kikosi cha kwanza (Starting XI):

Kipa: Abel
Mabeki: Kapombe (C), Kibabage, Toure, De Reuck
Viungo: Kante, Gueye, Maema, Mwalimu
Washambuliaji: Chama, Dura

Wachezaji wa akiba (Subs): Alexander, Duchu, Mligo, Mbegu, Kagoma, Semfuko, Naby, Bashiri, Morice, Chasambi

Matokeo ya Simba SC vs Coastal Union leo 02/04/2026

Kikosi hiki kinaonyesha dhamira ya Simba SC kutafuta ushindi muhimu katika mchezo huu.

Simba SC wanavyoingia kwenye mchezo

Simba SC wanaingia katika pambano hili wakiwa katika nafasi ya juu kwenye msimamo wa ligi, huku wakibeba rekodi nzuri dhidi ya Coastal Union.

Katika historia ya mikutano yao:

  • Simba SC wameshinda mechi 16
  • Coastal Union wameshinda mechi 1
  • Sare zikiwa 6

Takwimu hizi zinaonyesha wazi ubabe wa Simba SC wanapokutana na wapinzani wao hawa.

Fuatilia Hapa Matokeo ya Simba SC vs Coastal Union leo 02/04/2026

Simba Sc 2-0 Coastal Union

Matokeo ya mechi za Simba vs Coastal Union zilizopita

Rekodi za nyuma zinaendelea kuipa Simba SC kujiamini kuelekea mchezo wa leo:

  1. 01/03/2025: Coastal Union 0-3 Simba SC
  2. 04/10/2024: Simba SC 2-2 Coastal Union
  3. 09/03/2024: Coastal Union 1-2 Simba SC
  4. 21/09/2023: Simba SC 3-0 Coastal Union
  5. 09/06/2023: Simba SC 3-1 Coastal Union
  6. 03/12/2022: Coastal Union 0-3 Simba SC
  7. 07/04/2022: Coastal Union 1-2 Simba SC
  8. 31/10/2021: Simba SC 0-0 Coastal Union
  9. 11/07/2021: Simba SC 2-0 Coastal Union
  10. 21/11/2020: Coastal Union 0-7 Simba SC

Kauli za makocha kabla ya mchezo

Kocha msaidizi wa Simba SC, Selemani Matola, alieleza kuwa licha ya rekodi nzuri, Coastal Union si wapinzani wa kubeza.

“Hakuna mechi rahisi dhidi ya Coastal Union tunapokutana. Tumejiandaa vizuri, na lengo letu ni kupata matokeo chanya.”

Aliongeza kuwa kikosi kiko katika hali nzuri:

“Maandalizi yetu yamekuwa mazuri, wachezaji wote wako fiti na tayari kwa mchezo. Kilicho muhimu sasa ni kupigania pointi tatu.”

Kwa upande wa Coastal Union, kocha mkuu Mohammed Muya alionyesha kujiamini:

“Tunatambua ubora wa Simba, lakini tumekuja kupambana na kutafuta pointi tatu muhimu. Wachezaji wako katika hali nzuri kimwili.”

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya Ligi Kuu ya NBC Leo 02/04/2026
  2. Makundi ya Kombe la Dunia 2026
  3. Tottenham Hotspur Yaachana na Igor Tudor Baada ya Mfululizo wa Matokeo Mabaya
  4. Taifa Stars yaichakaza Macau 6-0 FIFA Series
  5. Tanzania Football Team Player Squad: National Football Guide
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo