Ratiba ya Kombe la Shirikisho CRDB FA Cup Leo 11/04/2026

Ratiba ya Kombe la Shirikisho CRDB FA Cup Leo 11/04/2026

Ligi Kuu Bara imesimama kwa muda, na ushindani sasa umehamia kwenye Kombe la Shirikisho la CRDB FA Cup, ambapo bingwa mtetezi Yanga anarejea uwanjani kuendeleza harakati za kulinda taji lake. Timu hiyo itakuwa mwenyeji wa TMA Stars katika mchezo wa hatua ya 16 bora utakaopigwa Uwanja wa KMC Complex.

Ratiba ya Kombe la Shirikisho CRDB FA Cup Leo 11/04/2026

Yanga dhidi ya TMA Stars

Yanga inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na kumbukumbu ya ushindi mkubwa wa mabao 7-1 dhidi ya Polisi Tanzania katika hatua ya 32 bora. Katika mchezo huo, mshambuliaji Laurindo Aurelio ‘Depu’ alifunga hat trick, huku kikosi kikionyesha ubora mkubwa wa ushambuliaji.

Hata hivyo, Yanga inatarajiwa kufanya mabadiliko madogo kikosini kutokana na uwepo wa majeruhi. Kocha Pedro Goncalves amesema licha ya changamoto hizo, timu yake imejipanga kuhakikisha inapata ushindi.

Upande wa TMA Stars, timu hiyo imefika hatua hii baada ya kuifunga Prisons bao 1-0. Ikiwa chini ya benchi la ufundi linaloifahamu vizuri presha ya michezo mikubwa, TMA inalenga kutoa ushindani mkali.

Mshambuliaji Ernest Baltazari anatajwa kuwa mchezaji muhimu kufuatiliwa, baada ya kufunga bao la ushindi katika mchezo uliopita.

Coastal Union vs Pamba Jiji

Katika mchezo mwingine, Coastal Union itakuwa mwenyeji wa Pamba Jiji mjini Tanga. Coastal Union inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na morali ya juu baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Stand United.

Katika ushindi huo, Cleofas Mkandala alifunga mabao mawili, huku Shiza Kichuya na Abdulkarim Segeja wakiongeza mabao mengine.

Hata hivyo, timu hiyo itacheza bila kocha mkuu Mohammed Muya aliyeondoka klabuni.

Kwa upande wa Pamba Jiji, wanatafuta kurejea kwenye ubora baada ya kupoteza mchezo wa ligi nyumbani. Walifuzu hatua hii kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Transit Camp, mabao yakifungwa na Henry Lutonja na John Nakibinge.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya Kombe la Shirikisho CRDB FA Cup Leo 10/04/2026
  2. Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2025/2026
  3. AFCON 2027 Kufanyika Mwezi Juni na Julai
  4. Harry Maguire Asaini Mkataba Mpya Manchester United Hadi 2027
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo