Kikosi cha Yanga VS TMA Star Leo 11/04/2026

Kikosi cha Yanga VS TMA Star Leo 11/04/2026

Timu ya wananchi, Yanga SC, leo Aprili 11, 2026, inashuka dimbani katika mwendelezo wa michuano ya Kombe la Shirikisho la CRDB (CRDB Federation Cup), ikiwa na dhamira ya kulinda ubingwa wake. Mchezo huo utapigwa katika Uwanja wa KMC Complex majira ya saa 12:30 jioni, ambapo watakutana na TMA Stars kutoka Arusha katika hatua ya 16 bora ya mashindano hayo.

Katika kipindi ambacho Ligi Kuu Bara imesimama kwa muda, ushindani mkali sasa umehamia kwenye michuano hii ya mtoano, huku macho ya mashabiki wengi yakielekezwa kwenye pambano hili muhimu.

Kikosi cha Yanga VS TMA Star Leo 11/04/2026

Rekodi ya Yanga Kabla ya Mchezo wa Leo

Yanga wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na kumbukumbu ya ushindi mkubwa walioupata katika hatua ya 32 bora, walipoifunga Polisi Tanzania kwa mabao 7-1 kwenye Uwanja wa KMC Complex, Machi 8, 2026.

Katika mchezo huo, mshambuliaji Laurindo Aurelio ‘Depu’ alifunga hat trick yake ya kwanza msimu huu, ikiwa ni moja ya dalili za uimara wa safu ya ushambuliaji ya timu hiyo kuelekea hatua za mtoano.

Kocha Pedro Goncalves ameendelea kuonyesha msimamo wa kutumia kikosi chenye mchanganyiko wa wachezaji wake muhimu, akilenga kuhakikisha timu inabaki kwenye ushindani wa taji hilo.

Fuatilia Hapa Matokeo ya Yanga VS TMA Star Leo 11/04/2026

Kikosi cha Yanga VS TMA Star Leo 11/04/2026

Kuelekea mchezo wa leo, Yanga wanaweza kufanya mabadiliko machache katika kikosi chao kutokana na hali ya majeruhi inayowakabili baadhi ya wachezaji. Hatua hiyo inalenga kulinda afya za kikosi huku wakihakikisha wanapata matokeo chanya.

Akizungumza kabla ya mchezo huo, kocha wa Yanga, Pedro Goncalves, alisema:

“Tunakwenda kukutana na TMA, timu inayotoka daraja la kwanza. Tunafahamu inapitia changamoto kwenye ligi yao, lakini nasi pia tuna changamoto ya kuwakosa baadhi ya wachezaji. Hata hivyo, tunapaswa kujituma na kuwajibika ili kupata matokeo mazuri.”

Kauli hiyo inaonyesha kuwa licha ya changamoto zilizopo, Yanga bado wanaingia uwanjani wakiwa na tahadhari na dhamira ya kusonga mbele.

Hiki Apa Kikosi cha Yanga Kilichotangazwa Leo dhidi ya TMA Star

Kikosi cha Yanga VS TMA Star Leo 11/04/2026

TMA Stars Wakiwa na Morali ya Ushindi

Kwa upande wa TMA Stars, timu hiyo imefika hatua hii baada ya kuiondoa Prisons kwa ushindi wa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa jijini Mbeya. Bao pekee la ushindi lilifungwa na mshambuliaji Ernest Baltazari.

TMA inayofundishwa na kocha Omary Matiko inaelekea kwenye mchezo huu ikiwa na matarajio ya kufanya ushindani mkali dhidi ya mabingwa watetezi, licha ya kucheza ligi ya daraja la kwanza.

Matiko alisema:

“Tumejiandaa vizuri tukijua ukubwa wa Yanga na tofauti ya ligi wanazocheza. Huu ni mchezo wa mtoano, hivyo tunapaswa kuwa makini na kutumia mpango kazi wetu kuhakikisha tunapata matokeo.”

Mchezo wa leo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, ukihusisha timu yenye uzoefu mkubwa wa mashindano kama Yanga dhidi ya TMA Stars ambao wanaonekana kuwa na ari ya kufanya vizuri katika mechi za mtoano.

Yanga wataingia wakiwa na rekodi nzuri ya ushambuliaji kutoka hatua iliyopita, huku TMA wakitegemea nidhamu ya mchezo na uwezo wa kutumia nafasi chache wanazopata.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya Kombe la Shirikisho CRDB FA Cup Leo 10/04/2026
  2. Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2025/2026
  3. AFCON 2027 Kufanyika Mwezi Juni na Julai
  4. Harry Maguire Asaini Mkataba Mpya Manchester United Hadi 2027
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo