Timu Zilizofuzu Robo Fainali Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup 2025/2026

Timu Zilizofuzu Robo Fainali Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup 2025/2026

Hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho la CRDB Federation Cup msimu wa 2025/2026 imefikia tamati rasmi leo Aprili 12, baada ya michezo kadhaa ya ushindani mkubwa iliyotoa taswira halisi ya ubora wa timu mbalimbali nchini.

Baada ya dakika 90 za mapambano makali na baadhi ya mechi kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti, sasa timu nane zilizofanikiwa kusonga mbele hadi hatua ya Robo Fainali zimejulikana, zikijiandaa kuendelea na vita ya kusaka taji hilo muhimu.

Mashindano haya, yanayodhaminiwa na CRDB Bank, yameendelea kuonyesha ushindani mkubwa huku timu kubwa na zile zinazochipukia zikionyesha kiwango cha juu katika kila hatua.

Timu Zilizofuzu Robo Fainali Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup 2025/2026

Orodha ya Timu Zilizofuzu Robo Fainali CRDB Federation Cup 2025/2026

Timu zilizofanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ni:

  1. Mashujaa FC
  2. JKT Tanzania
  3. Coastal Union
  4. Yanga SC
  5. Simba SC
  6. Singida Big Stars
  7. TRA United
  8. Azam Fc

Matokeo Muhimu ya Hatua ya 16 Bora

Mashujaa FC Yaibuka Kidedea Baada ya Ushindi wa Mikwaju ya Penalti

Katika mchezo uliopigwa Nyankumbu, Geita, Mashujaa FC ililazimika kutumia mikwaju ya penalti baada ya kutoka sare ya bila kufungana na Geita Gold ndani ya dakika 90. Mashujaa walionyesha utulivu mkubwa na kushinda kwa penalti 4-2, matokeo yaliyowapa tiketi ya robo fainali.

JKT Tanzania Yafuzu Baada ya Kuirarua Mbuni Fc

JKT Tanzania iliweka wazi dhamira yake ya kutwaa ubingwa baada ya kuichapa Mbuni FC mabao 3-0. Mchezo huo ulionyesha tofauti ya kiwango, huku JKT wakitawala kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mchezo.

Simba SC Yapindua Meza na Kuibuka na Ushindi Dhidi ya Dodoma Jiji

Simba SC ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Dodoma Jiji. Mabao kutoka kwa Khelfin Hamdun na Seleman Mwalimu (aliyefunga mawili), pamoja na Anicet Oura, yalihakikisha timu hiyo inasonga mbele.

TRA United Yatinga Robo Fainali Baada ya Kuichapa Namungo

TRA United iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo FC, kupitia mabao ya Ally Ng’anzi na Denis Nkane, na hivyo kujihakikishia nafasi katika hatua inayofuata.

Singida Big Stars Watinga Kwa Kishindo Cha 5-0 Dhidi ya Mbeya City

Singida Big Stars waliandika ushindi mkubwa wa mabao 5-1 dhidi ya Mbeya City. Ushindi huo uliakisi ubora wa safu yao ya ushambuliaji, iliyofunga kupitia Khalid Aucho, Lamine Jarjou, Ibrahim Imoro (mabao mawili) na Horso Muaku.

Yanga SC Yaendelea Kutetea Taji

Bao pekee la Max Nzengeli lilitosha kuipa Yanga SC ushindi wa 1-0 dhidi ya TMA FC katika dimba la KMC Complex. Ushindi huo unaendelea kuiweka Yanga kwenye njia ya kutetea ubingwa wao wa mashindano haya.

Coastal Union Yajikatia Tiketi ya Robo Fainali Baada ya Kuichapa Pamba Jiji

Coastal Union iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Pamba Jiji FC katika uwanja wa CCM Mkwakwani, Tanga. Matokeo hayo yanaonyesha uthabiti wa timu hiyo msimu huu.

Kwa ujumla, hatua ya 16 Bora ya CRDB Federation Cup 2025/2026 imekuwa na ushindani mkubwa, ikipelekea baadhi ya timu kuonyesha ubora mkubwa huku zingine zikiondoka kwa matokeo ya kushtukiza.

Ushindi wa Mashujaa FC kwa penalti na mabao mengi ya Singida Big Stars ni miongoni mwa matukio yaliyoibua hisia kali kwa mashabiki. Timu kubwa kama Simba SC na Yanga SC zimeendelea kudhihirisha uzoefu wao, wakati timu kama Mashujaa FC na TRA United zikionyesha kuwa zina uwezo wa kushindana katika ngazi za juu.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Matokeo ya Yanga VS TMA Star Leo 11/04/2026
  2. Yanga VS TMA Star Leo 11/04/2026 Saa Ngapi?
  3. Ratiba ya Kombe la Shirikisho CRDB FA Cup Leo 11/04/2026
  4. Ratiba ya Kombe la Shirikisho CRDB FA Cup Leo 10/04/2026
  5. Matokeo ya TRA United vs Simba Leo 09/04/2026
  6. Ratiba ya Ligi Kuu Ya NBC Leo 09/04/2026
  7. Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2025/2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo