Afrika Kusini vs Taifa Stars Leo 06/06/2025 Saa Ngapi?
Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Tanzania almaarufu kama Taifa Stars leo itashuka dimbani katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya wenyeji wao Bafana Bafana ya Afrika Kusini kwenye dimba la Peter Mokaba, mjini Polokwane. Mchezo huu umepangwa kuanza majira ya saa 2:30 usiku kwa saa za Tanzania (20:30 TZ), sawa na saa 1:30 usiku kwa saa za Afrika Kusini (19:30 SA).
Kikosi cha Taifa Stars tayari kimewasili salama nchini Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo huu wa kirafiki unaotambuliwa na FIFA.
Wakiwa chini ya nahodha wao Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, wachezaji wa Tanzania wana nia ya kupata matokeo mazuri dhidi ya wapinzani wao wakongwe, Bafana Bafana.
Wachezaji wa Taifa Stars waliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa OR Tambo jijini Johannesburg saa 2:00 asubuhi kwa saa za Afrika Kusini, ikiwa ni saa moja mbele ya muda wa nyumbani Tanzania.
Hata hivyo, kikosi hicho kilikuwa hakijakamilika kikamilifu kwani beki mahiri wa Simba SC, Shomari Kapombe, hakusafiri kutokana na matatizo ya kiafya, huku winga Suleiman Mwalimu ‘Gomez’ wa Wydad Athletic ya Morocco akitarajiwa kuungana na wenzake baadaye.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Mkuu wa msafara, James Mhagama, timu iko tayari kupambana si tu katika mechi ya leo, bali pia kuendeleza rekodi nzuri kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya COSAFA inayotarajiwa kuanza Juni 7, 2025.
Nini Maana ya Mchezo Huu kwa Taifa Stars?
Licha ya kuwa mchezo wa kirafiki, huu ni mtihani muhimu kwa Taifa Stars kuelekea michuano ya COSAFA. Nahodha Tshabalala ameeleza kuwa morali ya wachezaji iko juu, na wanaamini wanaweza kutoka na ushindi kutokana na ubora wa kikosi kilichopo.
Hii ni nafasi nzuri kwa benchi la ufundi la Tanzania kupima uimara wa timu yao dhidi ya wapinzani wa daraja la juu kabla ya kuingia vitani kwenye mechi za mashindano.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Herry Sasii Afungiwa Soka Miezi 6 Kisa Mechi ya Simba na Singida
- Seif Karihe Acharazwa Faini na Kufungiwa Michezo Mitatu kwa Kurusha Chupa
- Ronaldo Aipeleka Ureno Fainali UEFA Nations League 2024/2025
- Matokeo ya Germany Vs Portugal Leo 04/06/2025
- Wachezaji wa Soka U-21 Waliofanya Vizuri Msimu wa 2024/2025
- Mabekio Waliochangia Magoli Mengi Ligi Kuu ya NBC 2024/2025
- Siku ya Kuripoti Chuo cha Polisi Moshi 2025 kwa Vijana Waliochaguliwa
- Michezo ya Yanga Sc Iliobaki Msimu wa 2024/2025
- Wachezaji wa Yanga Walioitwa Kwenye Kikosi cha Timu ya Taifa June 2025
Leave a Reply