Andika Barua ya Kuomba Kazi Tanzania | Mfano Bora wa Barua ya Kazi
Kuandika barua ya kuomba kazi ni hatua ya kwanza muhimu kwa mtu yeyote anayetafuta ajira Tanzania. Barua ya kazi iliyopangwa vizuri inaweza kukupa nafasi ya kuitwa kwenye usaili hata kama una uzoefu mdogo wa kazi.
Ukurasa huu umekuandaliwa kukusaidia:
- Kuelewa barua ya kazi ni nini
- Kujua muundo sahihi wa barua ya kuomba kazi
- Kupata mfano wa barua ya kazi
- Kuandika barua yako ya kazi papo hapo kwa kutumia mfumo wetu wa uandishi wa barua
Barua ya Kuomba Kazi ni Nini?
Barua ya kuomba kazi ni barua rasmi ambayo mwombaji hutuma kwa mwajiri ili kuonyesha nia ya kuomba nafasi ya kazi iliyotangazwa. Barua hii huambatana na wasifu binafsi (CV) au hutumika peke yake kulingana na mahitaji ya mwajiri.
Kwa waajiri wa Tanzania, hasa:
- Serikali
- Taasisi za Umma
- Mashirika ya Kijamii (NGO)
barua ya kazi hupewa uzito mkubwa sana.
Muundo Sahihi wa Barua ya Kuomba Kazi Tanzania
Barua ya kazi Tanzania inapaswa kufuata muundo ufuatao:
- Anuani ya Mwombaji
- Tarehe ya Kuandika Barua
- Anuani ya Mwajiri au Ofisi
- Kichwa cha Barua (YAH: MAOMBI YA KAZI…)
- Utangulizi wa heshima
- Elimu ya Mwombaji
- Uzoefu wa Kazi
- Ujuzi na Uwezo
- Hitimisho la heshima
- Jina Kamili la Mwombaji
Kutofuata muundo huu kunaweza kufanya barua yako ikataliwe hata kabla ya kusomwa.
Mfano wa Barua ya Kuomba Kazi (Kwa Ufupi)
HABARIFORUM TANZANIA
S.L.P 35091,
Dar es Salaam
06-06-2022
KATIBU,
Ofisi ya Rais,
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma,
S.L.P 2320,
Dodoma.
YAH: MAOMBI YA KAZI NAFASI YA MCHUMI DARAJA LA II
Tafadhali rejea kichwa cha barua hapo juu. Ninaandika barua hii kuomba nafasi ya kazi ya Mchumi Daraja la II kama ilivyotangazwa katika tovuti ya ajira. Nimehitimu shahada ya uchumi na biashara katika kilimo na maliasili kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2019.
Baada ya kuhitimu, nimepata uzoefu wa kazi katika sekta binafsi ambapo nimewahi kufanya kazi kama mtunza fedha na meneja, nikihusika na ukusanyaji wa mapato, usimamizi wa mauzo, maandalizi ya ripoti za kifedha na usimamizi wa wafanyakazi. Kupitia majukumu haya nimejijengea ujuzi wa usimamizi na uhasibu.
Aidha, nina ujuzi wa matumizi ya kompyuta ikiwemo Microsoft Word, Microsoft Excel na programu nyingine muhimu kazini. Mimi ni mwajibikaji, mchapakazi na mwenye uwezo wa kufanya kazi kwa kushirikiana na wengine ili kufikia malengo ya taasisi.
Niko tayari kutumia elimu, ujuzi na uzoefu nilionao kwa manufaa ya taasisi na ujenzi wa Taifa kwa ujumla.
Wako katika ujenzi wa Taifa,
Habariforum Tanzania
- Mfano Wa Barua Ya Kuomba Kazi Afisa Muuguzi Msaidizi II
- Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la Magereza
Andika Barua ya Kuomba Kazi Haraka na Kwa Usahihi (Bila Stress)
Badala ya kuandika barua ya kazi kwa kubahatisha, unaweza kutumia mfumo wetu wa kisasa uliyopo hapa chini kuandika barua yako ya kuomba kazi kwa dakika chache tu.
Mfumo Huu wa Uandishi wa barua:
- Unafuata muundo rasmi wa Tanzania
- Unazingatia aina ya kazi (Serikali, NGO, Binafsi)
- Unatumia taarifa zako binafsi
- Inakutengenezea barua tayari kwa kuchapishwa au kutumwa
👇 Tumia mfumo hapa chini kuandika barua yako sasa
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQ )
Barua ya kuomba kazi iandikwe kwa lugha gani?
Kwa kazi za Tanzania, barua nyingi huandikwa kwa Kiswahili rasmi, isipokuwa kama tangazo limeelekeza Kiingereza.
Barua ya kazi iwe na kurasa ngapi?
Barua ya kazi inapaswa kuwa ukurasa mmoja tu.
Je, barua moja inaweza kutumika kuomba kazi tofauti?
Hapana. Kila kazi inahitaji barua yake maalum.
Mapendekezo ya Mhariri
