Azam VS Simba Leo 08/01/2026 Saa Ngapi?
Wana rambaramba wa Azam FC leo wanashuka dimbani kuivaa Simba SC katika pambano kubwa la nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi 2026, mchezo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini. Dabi hii ya Mzizima inapigwa leo Alhamisi tarehe 08 Januari 2026, katika Uwanja wa New Amaan Complex, Unguja, kuanzia saa 2:15 usiku.
Taarifa Muhimu za Mchezo
- Mchezo: Azam FC vs Simba SC
- Mashindano: Nusu Fainali – NMB Mapinduzi Cup 2026
- Tarehe: 08 Januari 2026
- Muda: Saa 2:15 usiku
- Uwanja: New Amaan Complex, Unguja
Viingilio
- Orbit & Saa: 3,000/=
- Urusi: 5,000/=
- VIP: 10,000/=
Dabi ya Mzizima Yarejea Mapinduzi Cup
Ni takribani mwezi mmoja umepita tangu timu hizi zikutanishe nguvu kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo Azam FC iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Simba SC. Leo usiku, dabi hiyo inarudi tena, safari hii ikiwa na uzito mkubwa zaidi kwani ni hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi 2026.
Mashindano ya mwaka huu yamebeba simulizi za kisasi, kwani mechi zote za nusu fainali zinawakutanisha wapinzani waliokutana kwenye hatua muhimu hapo awali. Kwa Simba, huu ni mtihani wa kurejesha heshima mbele ya Azam, huku Azam ikilenga kuendelea kudhihirisha ubabe wake kwenye michuano hii.
Mapendekezo ya Mhariri:







Leave a Reply