Bei Mpya ya Petroli Dar es Salaam October 2024 | EWURA Yashusha Bei za Mafuta
Bei Mpya ya Petroli Dar es Salaam October 2024
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta ambazo zitaanza kutumika rasmi kuanzia mwezi oktoba 2024. Bei ya petroli na dizeli ya rejareja kwa Oktoba 2024 imeshuka nchini, ikilinganishwa na Septemba, huku sababu kadhaa zikitajwa, ikiwamo kushuka kwa gharama za soko la Uarabuni. Taarifa hii ilitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dk. James Mwainyekule, na inahusisha mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, na Mtwara.
Bei Kikomo za Rejareja
Kulingana na taarifa ya EWURA, bei kikomo za rejareja kwa mafuta katika bandari ya Dar es Salaam ni kama ifuatavyo:
- Petroli: 3,011 TZS kwa lita
- Dizeli: 2,846 TZS kwa lita
- Mafuta ya Taa: 2,943 TZS kwa lita
Kwa mikoa mingine:
- Tanga:
- Petroli: 3,016 TZS
- Dizeli: 2,859 TZS
- Mafuta ya Taa: 2,989 TZS
- Mtwara:
- Petroli: 3,016 TZS
- Dizeli: 2,862 TZS
- Mafuta ya Taa: 3,016 TZS
Bei Kikomo za Jumla
Pia, bei kikomo za jumla kwa mafuta katika bandari ya Dar es Salaam ni kama ifuatavyo:
- Petroli: 2,880.15 TZS kwa lita
- Dizeli: 2,714.83 TZS kwa lita
- Mafuta ya Taa: 2,812.20 TZS
Kwa mikoa mingine:
- Tanga:
- Petroli: 2,884.77 TZS
- Dizeli: 2,728.21 TZS
- Mtwara:
- Petroli: 2,884.93 TZS
- Dizeli: 2,730.38 TZS
Maelekezo kwa Wafanyabiashara
Dk. Mwainyekule amekumbusha wafanyabiashara wa mafuta ya rejareja na jumla kuhusu umuhimu wa kuzingatia bei kikomo zinazotangazwa. Wafanyabiashara wanaweza kupata bei hizi kwa urahisi kwa kutumia huduma ya simu kwa kupiga namba 15200# na kufuata maelekezo. Huduma hii inapatikana bila malipo kwenye mitandao yote ya simu nchini.
Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166, bei za bidhaa za mafuta zitaendelea kuwekwa na soko. EWURA itahakikisha ushindani wa bei na kutangaza bei kikomo ili kuzuia udanganyifu katika soko. Kampuni za mafuta zinaweza kuuza bidhaa zao kwa bei ya ushindani, lakini bei hizo haziwezi kuwa chini au juu ya bei kikomo iliyotangazwa.
Wote wanatakiwa kuchapisha bei zao za mafuta katika mabango yanayoonekana wazi. Hii ni hatua muhimu ambayo itawasaidia wateja kufanya uchaguzi mzuri. Ni muhimu kwa vituo vya mafuta kutekeleza sheria hii, na kutokufuata matakwa haya kunaweza kupelekea adhabu kali.
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti