Bei Ya Friji Za Boss 2024 | Friji Za Boss Na Bei Zake
Je, unatafuta friji bora na ya kudumu kwa ajili ya matumizi yako ya nyumbani? Kama ndio basi fiji za boss zinaeza kua suluhisho kwako. Boss ni chapa inayoongoza katika tasnia ya vifaa vya nyumbani nchini Tanzania, ikijulikana kwa ubora, ubunifu, uimara wa bidhaa zake na kikubwa bei nafuu ambazo zimekua mkombozi kwa mtanzania mwenye kipato cha chini. Katika chapisho hili, tuta tazama kwa undani bei ya friji za Boss mwaka 2024, sifa zake za kipekee, na kwa nini zinastahili kuwa chaguo lako la kwanza.
Kwa Nini Uchague Friji ya Boss?
Kampuni ya Boss ni miongoni mwa kampuni chache ambazo zinasambaza friji bora zaidi zinazokidhi mahitaji ya kila familia ya Kitanzania kwa gharama nafuu. Friji zao zinakuja na teknolojia ya kisasa na muundo wa kuvutia, zikitoa thamani kubwa kwa pesa yako. Kama upo katika harakati za kutafuta friji kwa ajili ya matumizi ya nyumbanio basi hizi apa chini ni sababu za kukufanya uchague friji za boss.
Ubora wa Kudumu: Friji za Boss zinatengenezwa kwa vifaa vya ubora wa hali ya juu, zikihakikisha uimara na ufanisi wa muda mrefu. Ukiwa na friji ya Boss, una uhakika wa kupata kifaa kitakachokutumikia kwa miaka mingi ijayo.
Teknolojia ya Kisasa: Boss imewekeza katika teknolojia ya kisasa ili kuhakikisha friji zao zinakupa matumizi bora zaidi. Kuanzia mfumo wa kupoeza wa haraka hadi teknolojia ya kuzuia barafu, friji za Boss zitakupa hali ya utumiaji isiyo na usumbufu.
Muundo Wa Kuvutia: Friji za Boss zinapatikana katika miundo mbalimbali, kuanzia friji za mlango mmoja hadi zile za milango miwili na freezer chini. Hii inamaanisha kuwa unaweza kupata friji inayolingana kikamilifu na muundo wa jikoni yako.
Sifa Muhimu za Friji za Boss
Teknolojia ya Frost-Free: Sema kwaheri usumbufu wa kusafisha barafu kwa friji za Boss zisizo na barafu.
Muundo wa Kisasa: Furahia muonekano wa kisasa na wa kuvutia wa friji ya Boss jikoni au sebuleni mwako.
Bei Ya Friji Za Boss 2024 | Friji Za Boss Na Bei Zake
Bei ya friji za Boss hutofautiana kulingana na ukubwa, aina ya friji (model), na muuzaji. Kwa wastani, unaweza kupata kwa bei kati ya Tsh 300,000 hadi Tsh 2,000,000 kwa friji mpya ya Boss kulingana na ukubwa. HIzi apa chini ndizo bei za friji za boss kwa ukubwa
Ukubwa | Bei | Muuzaji (Instagram Name) |
BS70 FRIDGE LITA 60 | 345,000 | kariakoo_mall |
Fridge Boss BS LITA 70 | 380,000 | kariakoo_mall |
BS70 FRIDGE LITA 90 | 410,000 | Friji_Beipoa |
BS70 FRIDGE LITA 100 | 450,000 | og_electronixtz |
BS70 FRIDGE LITA 145 | 620,000 | kariakoo_mall |
Fridge Boss BS 185 | 650,000 | og_electronixtz |
Ni wapi unaweza Kununua Friji za Boss
Friji za Boss zinapatikana katika maduka makubwa ya vifaa vya elektroniki kote Tanzania. Pia unaweza kuzinunua mtandaoni kupitia tovuti za maduka hayo au tovuti za biashara za mtandaoni.
Mapendekezo Ya Mhariri:
Weka Komenti