Coastal Union vs Yanga Leo 07/12/2025 Saa Ngapi?

Coastal Union vs Yanga Leo 07/12/2025 Saa Ngapi?

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC, leo watakua ugenini kusaka pointi tatu muhimu watakaporejea Uwanja wa Jamhuri, Dodoma kuvaana na wenyeji Coastal Union katika mchezo unaoanza saa 1:15 usiku. Hii inakuwa mechi muhimu kwa pande zote mbili, hasa ikizingatiwa historia ndefu ya ushindani na matokeo yaliyopita.

Coastal Union vs Yanga Leo 07/12/2025 Saa Ngapi?

Coastal Union wanalazimika kutumia Jamhuri baada ya Uwanja wa Mkwakwani kufungiwa, na mechi ya leo inakuja wakati “Wagosi wa Kaya” wakijaribu kuvunja uteja uliodumu tangu 2022. Rekodi zinaonyesha timu hizo zimekutana mara 24 tangu 2011—Coastal ikiwa na ushindi mara tatu, Yanga 16, huku tano zikiisha sare. Mara ya mwisho Coastal kushinda ikiwa nyumbani ilikuwa Machi 4, 2021.

Katika misimu minne iliyopita, Coastal imekuwa ikipoteza kila inapokutana na Yanga, jambo lililosababisha viongozi wa klabu kuapa kwamba “leo ni leo.” Hata hivyo, Yanga inaingia na rekodi bora msimu huu, ikiwa haijapoteza katika mechi tano ilizocheza, ikishinda nne na kutoka sare moja. Coastal, kwa upande mwingine, imeshinda mchezo mmoja, imetoka sare tatu na kupoteza mmoja.

Kocha wa Yanga, Pedro Gonçalves, akizungumza juu ya mchezo huu alisema:
“Namba za wapinzani wetu hazidanganyi… tunajua haitakuwa mechi rahisi lakini tuna kikosi bora na tunahitaji pointi tatu.”
Mlinzi Offen Chikola aliongeza kuwa kikosi kimejiandaa kupambana kikamilifu.

Kwa upande wa Coastal Union, Kocha Mohammed Muya alibainisha kuwa wanaheshimu ubora wa Yanga lakini wamedhamiria kufanya vizuri:
“Mungu akileta kheri na wachezaji kufuata maelekezo, mashabiki watapata furaha.”
Nahodha Bakar Msimu naye alisisitiza umuhimu wa mchezo huu, akisema wamejipanga kupata pointi tatu nyumbani Dodoma.

Uwanjani, Yanga itaendelea kumtegemea Djigui Diarra pamoja na safu ya ulinzi ya Dickson Job na Bakar Mwamnyeto, huku washambuliaji Pacome Zouzoua, Prince Dube, Maxi Nzengeli na Duke Abuya wakitarajiwa kuongoza mashambulizi. Coastal itawategemea Maabad Maulid, Athumani Masumbuko na nahodha Msimu katika juhudi za kuivunja rekodi ya Yanga ambayo haijapoteza karibu mechi 25 mfululizo.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kikosi cha Simba vs Azam Leo 07/12/2025
  2. Matokeo ya Simba vs Azam Leo 07/12/2025
  3. Simba vs Azam Leo 07/12/2025 Saa Ngapi?
  4. Ratiba ya Mechi za Leo 07/12/2025 Ligi Kuu ya NBC
  5. Makundi ya Kombe la Dunia 2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo